Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Utawala wake uliniathiri kiasi Fulani,ila jambo moja alilokuwa ananifurahisha ni kuwakomesha wahindi kumzoea kingese.

Wahindi nadhani huko waliko Leo kila nyumba kunapikwa kachori na kucheza kuchukuchu hotae.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16]

We huwapendi wahindi
 
Kikwete alikuta bia 500 mpaka anaondoka akaacha 2500.
Magufuli alikuta bia 2500 mpaka anakufa kaacha 1800,hili wengi hawalioni kabisa.

Sikuwahi kupanda treni toka nizaliwe ila mwaka 2020 nimepanda Deluxe kwenda Moshi,hili umuhimu wake utaonekana baada ya treni kufa na kuanza nauli za 80k kwenda Moshi.

Kabla ya 2015 ilikua ni kawaida kusikia matukio ya ujambazi tena karibu na vituo vya polisi,ila toka 2015 mpaka sasa sijaskia jambazi aliesalimika kwenye ujambazi,na matukio yamekuwa machache sana.
Kikwete aliacha sh3000= kwa mwananchi kulipia kupita kwa usafiri wa basi Ngorongoro na Serengeti kama sisi kwetu Tarime, leo Magufuli kaacha 18000\= kwa mwananchi kupita mbugani kama unaenda huko kwenu, kwa kigezo kuwa unafanya utalii wa ndani haya kama unaenda msibani.
 
2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).
Hovyo.

Sio kufuata mkumbo kama ulivyoliweka hapa.

Huu ni udhaifu mkubwa sana aliouonyesha, pengine unaokaribiana na uvunjaji wa HAKI.

Dunia haikuwa inafuata mkumbo. Dunia ilifuata taratibu za kisayansi zinazojulikana katika kukabiri janga la ugonjwa wa mlipuko.
Huwezi kujipangia/kujichagulia njia zako juu ya kitu usichokifahamu, huku ukihatarisha maisha ya watu wako.

Bahati yetu ni kwamba kwa sababu zisizojulikana bado, corona huku Afrika haikushambulia kwa nguvu kama ilivyoshambulia kwingine. Ingekuwa hivyo toka mwanzo hali yetu ingekuwa mbaya sana.

Huu uamzi wa kujifanyia lake, eti kutofuata mkumbo, ulikuwa ni moja ya uamzi wa hovyo sana kwa kiongozi wa nchi.

Alichotakiwa kufuata juu ya hili, angekaa na wataalam na kujadili njia bora kufuatana na hali yetu.
Kwa mfano: msukumo mkubwa wa uamzi wa kutofuata 'guidelines' za WHO ni kulinda uchumi, hasa kutokana na madhara ya LOCKDOWN.

Basi angeshauriana na wataalam wake, wafuate yaliyomo kwenye 'guideline' hiyo, na kurekebisha kwa kiasi walichoona hayo matakwa ya 'Lockdown'.

Kutofuata mkumbo?, unapingana na sayansi? Chanjo unazikataa eti hufuati mkumbo?

Acha Bhwaanah!

Kuna mambo kadhaa ninayompa hongera juu yake kwa kuyafanya, hata kama wakati mwingine njia alizotumia kuyafanya hazikuwa sahihi.
 
Mi Sina Hata lakumkumbuka mwenzenu....

Nachosema NI Tengeneza KESHO YAKO.... kifo kipo na KITAKUSHTUKIZA

Huyo kashakuwa historia...

Tunawaombea, utulivu,Amani,busara na Uongozi Imara viongozi WAJAO....

What a time to be alive..

Mwenyezi Mungu Humpa rehma zake amtakae bila ya hesabu.
 
Kwa kumpoteza Ben Saanane.
Risasi 32 alizopigwa Tundu lisu bado zimenikaa kwenye akili yangu kila nikilikumbuka lile tukio nafika mbali sana na kujiuliza ni baba gani anaweza kumfanyia mwanae hata kama ni mtoto wa kambo (upinzani) that not humanity but all i can say neda zako magufuli umeumaliza mwendo over!!!!!!!!!
 
Namuomba Mwenyezi Mungu ampe hekima Mama atukuze na kujenga udugu kwa Watanzania.
 
Udhalimu, dhuluma, kudharau Katiba, Bunge, raia, Mahakama, kujichotea trillions za walipa kodi bila idhini ya Wabunge, ununuzi wa wanasiasa malaya, kugomea ukaguzi wa mahesabu ATCL na kwingineko ili kuficha uozo/wizi, kuifanya Tanzania kudharaulika na kuwa kichekesho/kituko kwa majirani zetu na dunia nzima na kuangusha uchumi wa Nchi.
 
Labda hayo mambo alikufanyia kipekee wewe na familia yako ndio maana unashindwa kuyataja,lakini ukija kwa Taifa huyu mtu alikuwa Kirusi cha umoja na mshikamano wa Taifa letu,na hata kama kuna machache aliyofanya alifanya kwa faida yake binafsi na kikundi chake kichomzunguka. Huyu ni Sadist, alifurahia maumivu na mateso ya wengi. Aende Jehanamu.
Duuuu pole kwa kufiwa mkuu ,punguza hasiraa
 
Alikuwa mchapa kazi sana alifanya mambo yakaonekana wakati mwingine alikuwa na upendo sana
 
Hovyo.

Sio kufuata mkumbo kama ulivyoliweka hapa.

Huu ni udhaifu mkubwa sana aliouonyesha, pengine unaokaribiana na uvunjaji wa HAKI.
Tena Mwana Sayansi ulie soma vyema na Phd juu!!! unapinga uchunguzi wa kisayansi kweli???? sasa asiye mwana sayansi je?? Alielewa anachofanya shuleni au alikuwa anaibia kwa wenzake na kukariri kariri tu! bora apite mitihani tu aende zake!! ... yaani!!! kayumbishwa na kina gwajima sasa hivi wako wapi!

eti aliposikia nasema hivi akanitumbua!! jamani
 
Nidhamu ipi Serikalini wakati utendaji umeshuka sana kutokana na go slow attitude ya Wafanyakazi wengi kwa kutoongezewa mishahara? Nidhamu ipi ya kufukuza watu kiholela bila kufuata taratibu husika ambazo zinalinda haki ya Wafanyakazi?
Wafanyakazi hewa + Vyeti feki. Ila ninampongeza kwa kuleta nidhamu serikalini na kuwakomesha wauza sembe.
 
Back
Top Bottom