Imepita miezi minne tokea chuma kitangulie mbele za haki huku watawala wamesahau kabisa kama kulikua na mtu anaitwa John ila umebaki ndani ya mioyo ya watanzania kama ulivosema baba tumeanza kukukumbuka.
Tanzania ni vilio kila kona hakuna aliye na tabasamu ndani ya nyuso yake maisha yanaenda kuwa magumu sana ndani ya tanzania tunakukumbuka sana baba,ulitunyima demokrasia ukatupa uzalendo na ujasiri wa kutamba mbele za watu na kusema mimi ni mtanzania na tulifanya kazi kweli hata alipokuja corona ulitupa ujasiri tukasimama imara.
Baba mimi nimeajiriwa nina makato kama yote kwenye mshahara
1. PAYE 9%
2. HESLB 15%
3. NHIF 1%
4. NSSF 10%
5. WCF
Pamoja na yote hayo baba mshahara wangu lazima upitie bank huko napo nakutana na makato kila nikitaka kutoa pesa zangu , baba yule yule waziri uliyemkataa leo hii amepewa dhamana kubwa sana na anatutesa kweli baba,
Baba huku bunge limeamua kumnyonya raia maskini aka mnyonye ambae ulipambana kuhakikisha anaishi vizuri leo eti pamoja na kulipa
1. Vat 18%
2. Transaction charge
Bado tumeanzishia kifo kipya kilichojificha ndani ya kodi ya uzalendo na kutuumiza sisi raia sisi wanyonge ambao mzigo wote tunaubeba sisi wakati wanaofanya biashara wakiachwa .
Baba leo hii bia ina thamani sana kuliko diesel na petrol - mafuta yanatumika kwenye machine mbali mbali hadi hospital na pia hata umeme unazalishwa kwa mafuta hii itasababishwa kuongezeka kwa gharama za kuishi ambazo zote izo zitamtesa raia wa chini
Baba tunakuomba uamke uje kuona haya yanayoendelea kwenye nchi uliyoipambania kwa jasho na damu