Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Ujasiri wa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati pamoja na umasikini tulionao....
 
B1264FBE-147B-4C19-A676-B1989D637D86.jpeg
 
Leo kijiweni katika hali ya kushangaza mzee mmoja ambaye alikuwa akipingana sana na utawala wa hayati. Amedondosha machozi na kumuomba hayati amsamehe.

Mzee huyu ni kada wa kutupwa wa chama ambacho chairman wake yuko ndani sasa. Siku za nyuma hapa kijiweni alikuwa akiponda kila alichofanya hayati ila leo amebadili gia anasema "HAKIKA MTU YULE ALIKUWA MWEMA"

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Acha uongo...we jamaa Unatumia nguvu nyingi kuleta porojo ..zitumie hizo nguvu kulima...HAKIKA NJAA KALI YAJA
 
Magufuli nakataaa. Mjamaa alitengeneza chuki baina ya watz. Miladi aliyoifanya na deni alilolitengeneza wala hayaendani. Jiwe ametuachia msala wa madeni makubwa
Matokeo tungeyaona kama angeendelea kuongoza, miradi mingi huoni faida mwanzoni. Wengi waliopita wameiba, mpaka wajukuu zao hawatafaidika. Kuhusu democracy, ilibidi iwe vile, it was a u turn for tanzania. Nchi ilikuwa inaenda kaskazini ( kutegemea misaada tuu) akaipindisha kusini, ili tujitegemee wenyewe, nchi yetu ni tajiri.
 
Sikumbuki ulikua mwezi wa ngap ila korona mjini Wuhan ilikua inaupiga mwingi kila siku unasikia watu 300 au 400 wamefarik ilikua kawaida tu.
Baada ya kupita siku nyingi mgonjwa wa kwanza akaingia bongo mjini arusha kwa sisi ambao tunategemea tutoke ili tule tukaingiwa na unyonge ukizingatia ugonjwa ule unaendana na lokdaun.
Mungu na wanadamu Mzee Pombe aka bulldoza akatuhakikishia kuwa hakutakuwa na kujifungia ndan hata iweje na tuendelee na harakat km kawa.
Kuna kipind kulikua ambulans mpya zilikua zinatutesa sana maana halipit lisaa bila kuisikia inapita lkn nazo akawapiga stop waache michezo.

Ingawaje kuna waliofarik na wengine waliumwa na kupona lkn kwa msimamo ule jamaa alijitendea haki kwa kuhakikisha kuwa hatuf tukiwa tumejifungia ndani.
 
He is well known as a covid-19 skeptic Tanzanian president, after fruits (pawpaw and jack fruit) being tested positive. Not mentioning his assassins, how they feel now, after the whole truth being out?
 
Back
Top Bottom