Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Mwezi Juni 2019,"Nilimsikia Mwalimu Julius Nyerere akizungumzia mradi wa bwawa la Umeme la Stieglers Gorge nikiwa shule ya msingi miaka ya 1970 mpaka namaliza Chuo kikuu cha Dar es Salaam bwawa hilo bado halijajengwa,Mimi nitalijenga"maneno timilifu ya Hayati Rais John Pombe Magufuli yalikwenda kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka Mto Rufiji uliofanywa wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,
Rais Magufuli alisema Serikali yake inatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 2.9 sawa na shilingi trilioni 6.5 za Kitanzania kujenga bwawa hilo."Natambua kuwa pamekuwepo na maneno, kuwa mradi huu utaharibu mazingira lakini kiukweli mradi huu unayajenga mazingira. Upinzani huo ulianza mara tu tulipotangaza kuanza kutekeleza mradi huu mwezi Juni 2017. Hata hivyo kwa kuwa nchi yetu ni huru na sio maskini, narudia nchi yetu huru na wala siyo maskini kama baadhi ya watu wanavyodhani. Tuliamua ni lazima tuutekeleze mradi huu, sisi hakuna mtu wa kutufundisha katika suala hili Tanzania. Tanzania ni kinara katika kuhifadhi mazingira", alisema rais Magufuli wakati akizindua mradi huo.
-Maoni yangu,na tunajua maoni hayapigwi rungu.
Kwa sasa Tanganyika inatumia takribani Megawatt 1,500 za umeme, ukijumlisha na zile Megawatt 100 wanazopewa bure wala urojo inakuwa MW 1,600.Bwawa la Nyerere likikamilika litazalisha Megawatt 2,100, na kufanya jumla ya Megawatt kwenye Gridi ya Tanganyika kuwa 3,700,kwa kuwa umeme unaozalishwa kwenye bwawa hauwezi kutunzwa kwenye battery kama za gari, inabidi utumike wote na kuisha, kufanikisha hili itabidi mambo kadhaa yatokee.
1.) Kushusha bei ya umeme ili viwamda na wananchi watumie umeme mwingi zaidi sababu ni wa bei nafuu AU
2.) Umeme ugawiwe bure kwa sekta maalum kama wanavyopewa bure wala urojo.
Sekta hizo ni
1.) Afya - Mahospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya wapewe umeme bure kama Zanzibar.
2.) Elimu - Mashule yote ya kutwa na bweni wapewe umeme bure kama Zanzibar
3.)Barabara - Taa zote za barabarani zipewe umeme bure kama Zanzibar
-Treni ya Umeme,taarifa ya habari September 2016.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo,Pia Rais Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini,hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara,aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.
-Nukuu mbalimbali siku ya uzinduzi wa bwawa la Umeme la Julius Nyerere,Julai 26 2019.
Rais ulipotuita Ikulu kutueleza ndoto yako kuhusu mradi huu, wengi hatukuelewa lakini sasa tumeanza kukuelewa. Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 42 na mpaka sasa umeshatekelezwa kwa miezi 6
Dkt. Kalemani: Mradi huu utakapokamilika utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitatumika kuendesha treni ya umeme. Umeme huu pia utasafirishwa hadi Chalinze na baadaye Dar es Salaam na Dodoma. Tunatazamia utasaidia sana kuendesha viwanda hapo baadaye
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kampuni hizi zinazojenga mradi huu zimefanya maajabu makubwa kule nchini Misri. Pacha wako Rais wa Misri, Fattah al-Sisi amejenga Mfereji wa Suez mwingine ndani ya kipindi kifupi. Nyie Marais nyieeee
Rais Magufuli:
Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo. Napenda kumshukuru Waziri wa Nishati kwa kunialika, nawashukuru pia Mabalozi na wageni wetu kutoka Misri. Hiki ni kielelezo cha urafiki
Hapa kwetu umeme unauzwa zaidi ya senti 11, gharama za umeme zinafanya kupanda kwa bei ya bidhaa na mwisho haziwezi kushindana kwenye soko. Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni Taifa huru, mradi huu umepata upinzani kutoka nje na ndani.
Nimalizie kwa kusema,Mungu akurehemu Hayati Rais John Pombe Magufuli,neema ya Mungu ikakulipe sawa sawa na upendo wako kwa Watanzania.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.