Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mwezi Juni 2019,"Nilimsikia Mwalimu Julius Nyerere akizungumzia mradi wa bwawa la Umeme la Stieglers Gorge nikiwa shule ya msingi miaka ya 1970 mpaka namaliza Chuo kikuu cha Dar es Salaam bwawa hilo bado halijajengwa,Mimi nitalijenga"maneno timilifu ya Hayati Rais John Pombe Magufuli yalikwenda kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka Mto Rufiji uliofanywa wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,

Rais Magufuli alisema Serikali yake inatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 2.9 sawa na shilingi trilioni 6.5 za Kitanzania kujenga bwawa hilo."Natambua kuwa pamekuwepo na maneno, kuwa mradi huu utaharibu mazingira lakini kiukweli mradi huu unayajenga mazingira. Upinzani huo ulianza mara tu tulipotangaza kuanza kutekeleza mradi huu mwezi Juni 2017. Hata hivyo kwa kuwa nchi yetu ni huru na sio maskini, narudia nchi yetu huru na wala siyo maskini kama baadhi ya watu wanavyodhani. Tuliamua ni lazima tuutekeleze mradi huu, sisi hakuna mtu wa kutufundisha katika suala hili Tanzania. Tanzania ni kinara katika kuhifadhi mazingira", alisema rais Magufuli wakati akizindua mradi huo.

-Maoni yangu,na tunajua maoni hayapigwi rungu.

Kwa sasa Tanganyika inatumia takribani Megawatt 1,500 za umeme, ukijumlisha na zile Megawatt 100 wanazopewa bure wala urojo inakuwa MW 1,600.Bwawa la Nyerere likikamilika litazalisha Megawatt 2,100, na kufanya jumla ya Megawatt kwenye Gridi ya Tanganyika kuwa 3,700,kwa kuwa umeme unaozalishwa kwenye bwawa hauwezi kutunzwa kwenye battery kama za gari, inabidi utumike wote na kuisha, kufanikisha hili itabidi mambo kadhaa yatokee.

1.) Kushusha bei ya umeme ili viwamda na wananchi watumie umeme mwingi zaidi sababu ni wa bei nafuu AU

2.) Umeme ugawiwe bure kwa sekta maalum kama wanavyopewa bure wala urojo.

Sekta hizo ni

1.) Afya - Mahospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya wapewe umeme bure kama Zanzibar.

2.) Elimu - Mashule yote ya kutwa na bweni wapewe umeme bure kama Zanzibar

3.)Barabara - Taa zote za barabarani zipewe umeme bure kama Zanzibar

-Treni ya Umeme,taarifa ya habari September 2016.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo,Pia Rais Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini,hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara,aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.

-Nukuu mbalimbali siku ya uzinduzi wa bwawa la Umeme la Julius Nyerere,Julai 26 2019.

Rais ulipotuita Ikulu kutueleza ndoto yako kuhusu mradi huu, wengi hatukuelewa lakini sasa tumeanza kukuelewa. Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 42 na mpaka sasa umeshatekelezwa kwa miezi 6

Dkt. Kalemani: Mradi huu utakapokamilika utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitatumika kuendesha treni ya umeme. Umeme huu pia utasafirishwa hadi Chalinze na baadaye Dar es Salaam na Dodoma. Tunatazamia utasaidia sana kuendesha viwanda hapo baadaye

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kampuni hizi zinazojenga mradi huu zimefanya maajabu makubwa kule nchini Misri. Pacha wako Rais wa Misri, Fattah al-Sisi amejenga Mfereji wa Suez mwingine ndani ya kipindi kifupi. Nyie Marais nyieeee

Rais Magufuli:
Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo‬. Napenda kumshukuru Waziri wa Nishati kwa kunialika, nawashukuru pia Mabalozi na wageni wetu kutoka Misri. Hiki ni kielelezo cha urafiki‬

Hapa kwetu umeme unauzwa zaidi ya senti 11, gharama za umeme zinafanya kupanda kwa bei ya bidhaa na mwisho haziwezi kushindana kwenye soko. Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni Taifa huru, mradi huu umepata upinzani kutoka nje na ndani.

Nimalizie kwa kusema,Mungu akurehemu Hayati Rais John Pombe Magufuli,neema ya Mungu ikakulipe sawa sawa na upendo wako kwa Watanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Nimeipenda hiii 👇👇

Ukweri ni lazima usemwe

Kama siyo huyu baba tusingekua na hili bwawa

Nyerere alishindwa

Mwinyi alishindwa

Mkapa akashindwa

Kikwete akashindwa

Magufuri shujaa wetu akaweza

Mama kakamilisha bwawa ile tu kwamba hana jinsi na angeacha wazalendo wasingemuelewa lakini ingekua ni yeye asingeweza

Ngosha ni shujaa
Ngosha ni baba wa pili wa taifa
Ngosha ni baba wa mfano
Ngosha ni baba mlezi
Ngosha ni dira
Ngosha ni role model wa kila mtu

Hivi kama sio Mungu kuturetea huyu shujaa tungekua na hali gani?Magufuri alikua shujaa

Na hili bwawa pongezi zote ziende kwake Magufuri huko ulipo wewe ni shujaa na baba wa taifa hiri

Hakuna kama magufuli
Tumpongeze mama… at least yeye anakamilisha miradi

Haifungi na kuitelekeza… tuna experience ya watangulizi waliokua wanaacha miradi ya watangulizi

Hata ile ya gesi na wind
 
Mwezi Juni 2019,"Nilimsikia Mwalimu Julius Nyerere akizungumzia mradi wa bwawa la Umeme la Stieglers Gorge nikiwa shule ya msingi miaka ya 1970 mpaka namaliza Chuo kikuu cha Dar es Salaam bwawa hilo bado halijajengwa,Mimi nitalijenga"maneno timilifu ya Hayati Rais John Pombe Magufuli yalikwenda kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka Mto Rufiji uliofanywa wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,

Rais Magufuli alisema Serikali yake inatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 2.9 sawa na shilingi trilioni 6.5 za Kitanzania kujenga bwawa hilo."Natambua kuwa pamekuwepo na maneno, kuwa mradi huu utaharibu mazingira lakini kiukweli mradi huu unayajenga mazingira. Upinzani huo ulianza mara tu tulipotangaza kuanza kutekeleza mradi huu mwezi Juni 2017. Hata hivyo kwa kuwa nchi yetu ni huru na sio maskini, narudia nchi yetu huru na wala siyo maskini kama baadhi ya watu wanavyodhani. Tuliamua ni lazima tuutekeleze mradi huu, sisi hakuna mtu wa kutufundisha katika suala hili Tanzania. Tanzania ni kinara katika kuhifadhi mazingira", alisema rais Magufuli wakati akizindua mradi huo.

-Maoni yangu,na tunajua maoni hayapigwi rungu.

Kwa sasa Tanganyika inatumia takribani Megawatt 1,500 za umeme, ukijumlisha na zile Megawatt 100 wanazopewa bure wala urojo inakuwa MW 1,600.Bwawa la Nyerere likikamilika litazalisha Megawatt 2,100, na kufanya jumla ya Megawatt kwenye Gridi ya Tanganyika kuwa 3,700,kwa kuwa umeme unaozalishwa kwenye bwawa hauwezi kutunzwa kwenye battery kama za gari, inabidi utumike wote na kuisha, kufanikisha hili itabidi mambo kadhaa yatokee.

1.) Kushusha bei ya umeme ili viwamda na wananchi watumie umeme mwingi zaidi sababu ni wa bei nafuu AU

2.) Umeme ugawiwe bure kwa sekta maalum kama wanavyopewa bure wala urojo.

Sekta hizo ni

1.) Afya - Mahospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya wapewe umeme bure kama Zanzibar.

2.) Elimu - Mashule yote ya kutwa na bweni wapewe umeme bure kama Zanzibar

3.)Barabara - Taa zote za barabarani zipewe umeme bure kama Zanzibar

-Treni ya Umeme,taarifa ya habari September 2016.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo,Pia Rais Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini,hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara,aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.

-Nukuu mbalimbali siku ya uzinduzi wa bwawa la Umeme la Julius Nyerere,Julai 26 2019.

Rais ulipotuita Ikulu kutueleza ndoto yako kuhusu mradi huu, wengi hatukuelewa lakini sasa tumeanza kukuelewa. Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 42 na mpaka sasa umeshatekelezwa kwa miezi 6

Dkt. Kalemani: Mradi huu utakapokamilika utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitatumika kuendesha treni ya umeme. Umeme huu pia utasafirishwa hadi Chalinze na baadaye Dar es Salaam na Dodoma. Tunatazamia utasaidia sana kuendesha viwanda hapo baadaye

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kampuni hizi zinazojenga mradi huu zimefanya maajabu makubwa kule nchini Misri. Pacha wako Rais wa Misri, Fattah al-Sisi amejenga Mfereji wa Suez mwingine ndani ya kipindi kifupi. Nyie Marais nyieeee

Rais Magufuli:
Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo‬. Napenda kumshukuru Waziri wa Nishati kwa kunialika, nawashukuru pia Mabalozi na wageni wetu kutoka Misri. Hiki ni kielelezo cha urafiki‬

Hapa kwetu umeme unauzwa zaidi ya senti 11, gharama za umeme zinafanya kupanda kwa bei ya bidhaa na mwisho haziwezi kushindana kwenye soko. Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni Taifa huru, mradi huu umepata upinzani kutoka nje na ndani.

Nimalizie kwa kusema,Mungu akurehemu Hayati Rais John Pombe Magufuli,neema ya Mungu ikakulipe sawa sawa na upendo wako kwa Watanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
R.I.P #CHUMAJPM#
 
.
JamiiForums1442669155.jpg
 
Vijana mkoje siku hizi mbona mnapenda kulia lia?
 
Daima tutamkumbuka JPM. Naamini Mungu atatupatia kiongozi mwingine kama JPM au zaidi yake.
 
Hakuna matatizo ya maji kupungua ni wahuni wanafungulia maji ili mabwawa yashindwe kuzalisha umeme wauze majenereta uzuri ni kwamba magu alitufumbua macho Kwa uhuni wenu wa kulihujumu hili taifa
Aliwafumbua macho au aliwajaza ujinga?
 
Katika mambo ambayo hayati Mkapa alijitahidi kwenye Uongozi wake ni kufanya Teuzi kwa kuangalia taranta ya muhusika

Magufuli alipoingia tu bungeni Mkapa akamteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi chini ya mama Anna Abdallah na baadae akampandisha kuwa Waziri kamili

Kwa kifupi Utume wa John Magufuli hapa Duniani ulikuwa ni " Kujenga Miundombinu"

Hata sasa tunaenjoy Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere

Mungu wa Mbinguni awarehemu Ben Mkapa na John Magufuli

Wazee wa Legacy tunagonga Wine tu 😂🔥
 
Rubbish, njia ya kupiga hela na kuwapa ndugu zake miradi ya ujenzi na yeye mwenyewe (Manyanga construction company). Think wide, magufulia alikuwa sacred Looter
 
Bora anaye kula huku anawayengenezea wengine wengi kit kitakacho wakomboa.
Fikiria Morogoro road na umeme wa bwawa la Nyerere vinasaidia wangapi?
Linganisha na walaji wanao tuzimia umeme.
 
Attractive your theory might be, it defies the 8th commandment of God's commandments
 
Back
Top Bottom