Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Chadema hata wakimsimamisha Mdude kuwa mgombea urais nitampa kura.
Seriously, kwa yeye kuendelea kuongoza nchi baada ya haya yote, Tanzania itakuwa ni nchi ya kipekee sana.

Upekee wake utaanzia kwenye chama chake kitakachoruhusu aendelee kukiongoza na kupewa ridhaa ya kugombea urais.

Upekee wake utatokana na vyama vya upinzani vitakavyoshindwa kushawishi wananchi kutumia njia zote walizo nazo wananchi hao kukataa kuongozwa naye, hata kama atataka kutumia mabavu kuwaongoza.

Upekee wa Tanzania kama nchi utakuwa ni kwa wananchi wake, wapiga kura kukubali aendelee kuwa kiongozi wao; hata kama ikiwa ni kwa kuwalazimisha kwa mabavu awaongoze, na wao wabaki kimya na kukubali aendelee.

Tanzania hii itakuwa nchi ya kipekee sana.
 

Jemedari wa vita anapigana ili kuokoa kikosi chake, hata kwa kupunguza ratio yake ya chakula ili wengine wapate. Jemedari wetu atapokea mshahara wake kamili wakati madaktari na manesi hawana vitendea kazi.
 
Kwani kampeni za urais zimeanza tayari..
 
Hapa Kamanda na Jemadari Mkuu yupo juu ya tanki la jeshi, kifaru, uwanja wa vita!
Mkuu Mag3, usishangae kabla uzi huu haujachacha, au hata ukichacha na kuelekea kwenye 'archive', mpya utaanzishwa ukimwonyesha 'jemadari' wetu kwenye magwanda ya kijeshi.

Picha zimo humu - zitatafutwa ili zionyeshe jemedari wetu huyu mpya alivyo mkakamavu.

Kikwete pamoja na kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi, sikumwona kwenye magwanda hayo akiwa rais. Kama aliyavaa, sikumwona.

Mkapa, hata sijui kama alishawahi kuvaa hata t-shirt za kijeshi. Mwinyi je? Wote sikuwaona; au inawezekana taarifa nyingi za nchi yangu na viongozi wake zilikuwa zikinipita pembeni mara kwa mara. Au wapambe wao hawakutaka waonekane katika hali hiyo.

Za huyu 'Jemedari', huhangaiki sana kuziona, kwa sababu yeye ni mtu wa kujionyesha zaidi.
 
Seriously, kwa yeye kuendelea kuongoza nchi baada ya haya yote, Tanzania itakuwa ni nchi ya kipekee sana.
Huyu kwa kura halali hapiti ila atapita kwa kura haramu!
 
Kadi ya mke wangu ikae vizurikwani hakika nitaiiba ili nikampe kura mbili za uhakika. Uliza yanayotokea nchi jirani waliojifanya kujifungia ndani


Corona kaingia mpaka Bungeni BAADA ya KUSHINDWA KUZUIA MIKUSANYIKO ISIYOKUWA YA LAZIMA.

SASA KUCHAPA KAZI NI KUCHAPWA NA KAZI.
 
simpi kura ingawa 2015 nilimpa...sababu ya kwanza, kulazimisha nchi yetu kuwa ya chama kimoja.
sababu nyingine kudhuru watu woote wanaompinga na kumkosoa.

kuna mambo kafanya vzr hasa kurejesha nidhamu kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu wa sasa anavaa zile gwanda za jesh kma urembo tu. Mwalimu yuko vtani na kaunda suti yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshapiga kura yangu Mkuu..
Huyu HATUFAI hata kidogo..
Na kwasababu amekimbia mwenyewe Ikulu..
Asirudi.
 
Mtaji mkubwa wa ccm ni wazee nawashangaa wameleta corona ili iangamize wazee

Sasa ngoja wazee waishe na corona tubaki vijana watupu tuwafundishe adabu mwezi October

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…