Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Kadi ya mke wangu ikae vizurikwani hakika nitaiiba ili nikampe kura mbili za uhakika. Uliza yanayotokea nchi jirani waliojifanya kujifungia ndani
Kwanini tuulize wakati wewe unajua yanayotokea huku,tuambie
 
Yaani Janga la Dunia la CORONA ambalo limewashinda hata Marais wanaosifika Duniani ndiyo leo hii lifanye Rais Dkt. Magufuli hafai? Sasa naanza Kuamini kuwa Great Thinkers wameshapungua nchini Tanzania.
Mkuu wewe unadhani Magufuli anapaswa kupimwa kwa kuokota vichwa vya treni kule bandarini au kwa kuwadhibiti Chadema? Tusaidie mkuu ili na sisi tujue anafaa kwa lipi?
 
Kwa mbali nakumbuka ile siku nduli Idi Amin alipotushambulia na kuteka sehemu ya Jamhuri yetu huku akitishia kuongeza mashambulizi hadi Bandari yetu ya Salama. Jemadari wetu Mkuu wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakutafuta pa kukimbilia kujificha na kututaka tusali, hapana.

Baada ya kutangaza tu kwamba tuko vitani, aliingia kazini kuwahamasisha wananchi na kuliongoza Jeshi la wananchi, JWTZ, kwa kazi moja tu, kumpiga adui. Na kweli nduli alitandikwa. Alipigwa hadi akaikimbia si tu ardhi yetu na mambo yakaishia hapo, hapana, alizidi kutandikwa hadi akaikimbia na nchi yake Uganda.

Naam, hivyo ndivyo ilivyo, Kamanda na Jemadari Mkuu hakimbii uwanja wa vita akawaacha askari wake mikononi mwa wahuni kama Bashite.

View attachment 1425268
Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na makamanda wa Jeshi.

View attachment 1425269
Hapa Kamanda wa kweli na Jemadari Mkuu, Mwalimu Nyerere, yupo juu ya tanki la jeshi, kifaru, uwanja wa vita!
Tukumbuke tunapomchagua Rais, tunamchagua Kamanda na Jemadari Mkuu ambaye atakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya adui anayeonekana na asiyeonekana na si anayejificha mapambano yakipamba moto...ni hayo tu!
Wa kwetu wa leo, ni wa kuoenda kuvaa kombati kuelekea kwenye kumbi za mikutano na siyo kuelekea kwenye uwanja wa mapambano.
 
Habari za mda huu.
Corona ni hatari kufata taratibu zilizoweka na wizara ya afya kujilinda na kuwalinda tuwapendao.

Niende kwenye mada chap chap.
Kumpa kura yangu ni Big No!

Vipi wewe ndugu yangu utampa kura yako??

Sent using Jamii Forums mobile app
Wadau amani iwe nanyi

Leo nimekaa na kutafakari msitakabali wa nchi yetu nimekuja na ugunduzi wa mambo kadha wa kadha.
Kwenye siasa za nchi yetu kuna kundi la watu ambalo kazi yao ni kuwaaminisha wananchi kwamba kiongozi fulani hafai hivyo wasifuate maagizo yake lakini wananchi ndiyo kwanza wanazidi kumfuata na kumsikiliza huyo kiongozi !

Chadema wamekuwa wakimwandama sana RC Makonda na kujaribu kumfubaza mbele ya wananchi tangu kipindi kile amtaje Mbowe kwenye genge la wauza madawa ya kulevya nchini na kupelekea madawa kuisha kabisa mitaani na mateja kupungua mno nchini kote, tangu hapo kila atakachoagiza Makonda Chadema lazima wapinge.
Mfano tarehe 20/April Makonda alitaka kila mwana Dares salaam kuanza kuvaa barakoa ili kujikinga na na hivi virus vya Corona lakini Chadema walipinga agizo hilo kwa nguvu zote!
Chadema walipinga agizo hilo kwa kisingizio kwamba anayetakiwa kutoa agizo la kuvaa barakoa ni waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Lakini cha kushangaza pamoja na Chadema kuwataka wananchi wasivae barakoa lakini wananchi wameitikia kweli kweli wito wa Makonda kila kona ya jiji wananchi wameva barakoa, hii ina maana gani kwa Chadema?
Je ina maanisha chadema haisikilizwi tena na wananchi? Mvuto wa chadema umekwisha? Je ni laana ya kuuza madawa ya kulevya au damu ya Akwilina?

Nini kimetokea chadema iliyokuwa inaagiza watu watoke nje kuandamana na wanatoka kweli licha ya mabomu leo imekuwaje hawafuati maagizo ya chadema? Ni laana ya Dk Slaa? Kwa hali hii Chadema itashinda uchaguzi wowote?
Yetu macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatopata ila atashinda. Lakini utakuwa ni msimu mgumu sana kwake. Uchumi wa Dunia utakuwa chini, Dollar zitaingia kwa uchache sana, itabidi abadili shilingi kwenda Dollar ili alipe wakandarasi, kuagiza mafuta n.k Miradi mikubwa itamsumbua kichwa sana kuimaliza.

2020-2025 ni kipindi ambacho kinahitaji strategy ya kutosha na ni wakati ambayo tutahitaji misaada ya Mabeberu kuliko wakati wowote.

Sina hakika kama Raisi wetu atakubali kumpigia goti Beberu apewe msaada au ataendelea kukopa aiweke nchi kwenye madeni zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wafanyakazi wa hivyo vyombo ni watanzania pia sasa whether wanakiona hiki ambacho Mimi na wewe tunaona au wamepigwa upovu na mishahara na marupurupu ya muda mfupi Mungu ndo anajua,Ila tuendelee kuwaombea,Kama Mungu anaweza simamisha corona dhidi ya Tanzania anashindwaje kwa mtu anaiharibu Tanzania?
Niseme tu wa kulaumiwa ni viongozi wa dini wamejifichia kwenye unafiki wa njaa.Wanashindwa vipi kuwatenga waumini wao ambao ni wahuni wasiriharibu taifa Bali uwakumbatia Hadi kuwaruhusu wakanyage mimbali wamkufuru Mungu.Watu waovu wasipotengwa katu awatoacha uovu wao wataendelea kutesa na kuumiza watu.Nawakubali viongozi wa dini wa Congo na Kenya walisimama na jamii wakawapinga wahuni wasibomoe nchi zao.Viongozi wa dini Wana nguvu Sana Kama wataamua kusimamia kweli ili kuliponya taifa,check Leo hata sadaka na michango imepungua sababu ya unafiki wao wa kukaa kimya.
 
Mkuu wafanyakazi wa hivyo vyombo ni watanzania pia sasa whether wanakiona hiki ambacho Mimi na wewe tunaona au wamepigwa upovu na mishahara na marupurupu ya muda mfupi Mungu ndo anajua,Ila tuendelee kuwaombea,Kama Mungu anaweza simamisha corona dhidi ya Tanzania anashindwaje kwa mtu anaiharibu Tanzania?
Awajaongezwa mishahara miaka plus kikotoo kitarudi cha ajabu yatakosea tu.Kuwa maiti ni mzigo
 
Back
Top Bottom