Je, waandishi wa Biblia hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?

Je, waandishi wa Biblia hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Imekuwa Ikifahamika kwa watu wa chache sana wenye maarifa na ujuzi katika miaka ya hivi karibuni (20th century), kwamba biblia ni masimulizi ya ‘Vibao vya mawe vya Sumeria’ vilivyo ‘ghoshiwa’ na wajanja wachache (hasa Warumi) katika kukamata na kupumbaza akili raia katika himaya zao, hii iliwarahisishia kujitanua na kutawala kwa uhakika zaidi.

Vibao vya mawe vya kale vya ‘Sumeria’ vinakadiriwa kuandikwa takriban miaka 3,000 kabla ya kuandikwa kwa biblia, na Biblia inakadiriwa kuandikwa miaka 2,000 baada ya kuandikwa kwa vibao vya mawe vya Sumeria.

Vibao vya Sumeria viligundulika miaka ya 1800 na watafiti wa mambo ya kale toka Uingereza katika ukanda wa ‘Assyria’; idadi ya hivyo vibao bi maelfu kwa maelfu, na kwakuwa lugha hiyo ni ya kale sana na imeshabadilika sana, ilichukua miaka mingi kuweza kutafsiri vilivyoandikwa kwenye vibao hivyo.

Miaka ya 1900 idadi kubwa ya vibao hivyo, ambavyo hadi miaka ya hivi karibuni tu vilikuwa vimefanywa siri na kufichwa katika majumba ya makumbusho ya uingereza, viliweza kutafsiriwa kwa ufasaha mkubwa sana, kilichokuwa kimeandikwa humo kilikuwa ni tishio na aibu kubwa kwa wezi wa maandiko walioandika biblia, hivyo kwa miongo yote hiyo hakuna aliyeweza kuambiwa kilichomo.

Miaka ya hivi karibuni watu wengi sana huko ulaya na Marekani walianza kupoteza hamu ya mambo yahusuyo kanisa na Ukristo kwa ujumla, hivyo hofu ya kuviweka hadharani vibao hivyo ikapungua, na baadhi japo ni vichache (vile ambavyo sio tishio sana) vimeanzwa kiwekwa wazi kwenye majumba ya makumbusho huko uingereza, kiasi hata kama wewe ni paroko wa kanisa flani, unaweza kuwachangisha waumini wako pesa ya tiketi na ukaenda kujionea mwenye kwa macho yako.

Hadithi zilizofanyiwa ‘plagiarism’ na ‘kughoshiwa’ na biblia ni nyingi, na nitazichambua nyingi kadri niwezavyo, ila moja iliyonipagawisha ni ile ya ‘Shetani’ kumshawishi Eva wafanye ngono na Adam, kitendo kilichomwogopesha na kumkera ‘Creator wa kwanza’ , Adam , Eva, na ‘Shetani walimchukiza sana.

Nyingine ni ile ya ‘Shetani’ kuwa muumbaji wa mwisho wa binadamu (alifanya kazi ya finishing) kwa kutagawia ‘DNA’ yake ya kimungu na kuwafanya binadamu kuwa na’Umungu ndani yao, hili pia lilimkera sana ‘Creator wa kwanza’, maana liliwapa binadamu uMungu na kumpa wivu sana, ni mungu mwenye wivu sana, shetani alimkera sana kwa kitendo hichi, na inawezekana adhabu yake na ya kwetu itakuwa kali sana mwishowe.

Nakunyw amaji nianze kuweka Hadithi kwa hadithi tena kwa undani.
==============================
Hadithi ya kwanza: Post no. 44
============================

View: https://www.instagram.com/reel/DCg_mj_Il44/?igsh=ZjFrMWRwdXg5bGxn
 
Ignorance is Bliss. wewe mada zako hua ni za kijinga jinga tu, sijawai kukuona umeandika jambo la maana humu.

Sawa ni hadithi za kughushi lakini je Ukristo unatoa impact gani kwenye jamii? Ukristo ndio dini pekee iliyo hai hapa duniani, zingine zote ni mfu, ndo maana mamilion ya watu walipaswa wawe wameshakufa lakini ukristo uliwaokoa kutoka kwenye vitanda vya vifo vyao.

Mungu akurehemu wewe ignorant.
 
Mkuu biblia ni mkusanyiko wa vitabu je unaweza kutuambia vitabu vilivyo kusanywa na kufanywa biblia vimeandika miaka gani? Au Uwepo wake niwa miaka mingapi ili tuje kupata ulinganifu na hizo hadithi kwa ulinganifu wa miaka je,kama nikisema hadithi hizo zime-copy na paste hadithi za kwenye vitabu vilivyo unda biblia nitakuwa sawa?
 
Mkuu ni vema apewe muda alete hizo hadithi zake na tutamtaka alete na ulinganifu na kitabu kitakatifu Cha Islamic maana Kuna mfanano wa baadhi ya vitabu
 
Ignorance is Bliss. wewe mada zako hua ni za kijinga jinga tu, sijawai kukuona umeandika jambo la maana humu.

Sawa ni hadithi za kughushi lakini je Ukristo unatoa impact gani kwenye jamii? Ukristo ndio dini pekee iliyo hai hapa duniani, zingine zote ni mfu, ndo maana mamilion ya watu walipaswa wawe wameshakufa lakini ukristo uliwaokoa kutoka kwenye vitanda vya vifo vyao.

Mungu akurehemu wewe ignorant.
Daah, kwani shida nini mzee...? Kwani hivyo vibao vya Sumeria mimi ndio nimeviandika? Nioneeni huruma muda mwingine basi..
 
Mkuu biblia ni mkusanyiko wa vitabu je unaweza kutuambia vitabu vilivyo kusanywa na kufanywa biblia vimeandika miaka gani? Au Uwepo wake niwa miaka mingapi ili tuje kupata ulinganifu na hizo hadithi kwa ulinganifu wa miaka je,kama nikisema hadithi hizo zime-copy na paste hadithi za kwenye vitabu vilivyo unda biblia nitakuwa sawa?
Sina hakika na ulichouliza, ila kipindi vibao vya Sumeria vinaandikwa hapakuwa hata na karatasi, walichonga mawe ili kuandika (engraving), ni miaka 3,000 kabla ya kitabu chochote cha bible kuandikwa.
 
Vibao vya Sumeria viligundulika miaka ya 1800 na watafiti wa mambo ya kale toka Uingereza katika ukanda wa ‘Assyria’; idadi ya hivyo vibao bi maelfu kwa maelfu, na kwakuwa lugha hiyo ni ya kale sana na imeshabadilika sana, ilichukua miaka mingi kuweza kutafsiri vilivyoandikwa kwenye vibao hivyo.
Kama vibao vimeandikwa kwa lugha ya kale we ukienda utaweza kufasiri leo ay unaenda kuangalia hayo mawe tu
 
Kwa maandiko ayo usiseme biblia tu bali sema "Je, waandishi wa vitabu vya dini (Biblia na Quran) hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?" Maana naona wote wameenda tofauti na ayo maandiko.
 
Kama vibao vimeandikwa kwa lugha ya kale we ukienda utaweza kufasiri leo ay unaenda kuangalia hayo mawe tu
Hivyo vibao vya Sumeria wameweza kuvitafsiri vyote..., sasa hayo mengine sijaelewa unamaanisha nini.., maana kuna factors nyingi zinahusika katika kuweza au kushindwa kutafsiri
 
Ignorance is Bliss. wewe mada zako hua ni za kijinga jinga tu, sijawai kukuona umeandika jambo la maana humu.

Sawa ni hadithi za kughushi lakini je Ukristo unatoa impact gani kwenye jamii? Ukristo ndio dini pekee iliyo hai hapa duniani, zingine zote ni mfu, ndo maana mamilion ya watu walipaswa wawe wameshakufa lakini ukristo uliwaokoa kutoka kwenye vitanda vya vifo vyao.

Mungu akurehemu wewe ignorant.
Ungejiuliza kwanza Wwe hiyo Akili yako

,Ukristo wa Leo umewagawanya Watu na Kuwafamya Wawe na Chuki Kati Yao ,Mkatoliki hawawezi kuoana na Msabato, Msabato hataki kuolewa na Anglicana.

Mmegawanyika Hamna Umoja Wowote ule maana Mnasimamia Kitu kisicho na Ukweli ndani yake.
 
Back
Top Bottom