Je, waandishi wa Biblia hawakuona aibu kufanya ‘Plagiarism’ ya wazi wazi kwenye ‘Vibao vya Sumeria’ na kufanya editing bila aibu kabisa?

Umeandika kitu kizuri
 
Kweli
 
Hili swali hata Mimi juu hapo nimemtaka aweke ulinganifu na Quran maana Kuna mfanano wa vitabu
 
Sina hakika na ulichouliza, ila kipindi vibao vya Sumeria vinaandikwa hapakuwa hata na karatasi, walichonga mawe ili kuandika (engraving), ni miaka 3,000 kabla ya kitabu chochote cha bible kuandikwa.
Mkuu amri za Mungu nazo ziliandikwa kwenye mawe je,nikisema amri hizo ziliandikwa kabla ya hadithi hiyo nitakuwa sawa ?
 
Mkuu amri za Mungu nazo ziliandikwa kwenye mawe je,nikisema amri hizo ziliandikwa kabla ya hadithi hiyo nitakuwa sawa ?
Tunapima umri wa vitu kwa kutumia mbinu za kisayansi, mfano vitu vilivyokuwa na asili ya uhai (organic) tunatumia Carbon dating, vitu kama mawe pia vina ‘method yake’ . hivyo vibao vimetambulika kwa mbinu hizo kuwa na miaka 3,000 zaidi ya kipindi cha kuandikwa kwa biblia. Maana hata sasa kuna mashahidi ya kaburini yanaandikwa kwenye mawe, ila haimaanishi mashahidi haya yana umri zaidi ya vibao vya sumeria
 
Mkuu ebu Leta hizo hadithi tujifunze kuhusu maswali nitarudi baadaye
 
Oya mwana ukiweka ni nistue fasta
 
Ukigusia sumeria moja kwa moja utakua unaenda kugusia theolojia ya unajimu sayansi takatifu ya kale huku ndio utakuta wa akina ANNUNAK ELOHIM ENK n.k uko unakotaka kugusia sijui kama kuna mtu atakuelewa maana inahtaji akili ya ziada
Kuna mdau anadai ushahidi, sasa sijui nimpe ushahidi wa namna gani
 
Hapo sasa unamaanisha na msaafu una plagarism pia.. usiamini kila kitu unachosoma kwenye mtandao mkuu


Sasahivi tawala za wazungu wanafanya social engineering kubadili watu wasiamini katika uwepo wa Mungu.. ili iwe rahis kwao kufanya mambo yao bila kupingwa na jamii husika
 
Shida ni kwamba, hivyo vibao vipo maelfu kwa maelfu, na vipo vingi vinaendelewa kufukuliwa, sasa utasema walivipandikiza hivyo vibao miaka 3000 iliyopita? Pia nani kasema hivyo vibao vinaashiria kutokuwepo kwa Mungu? Sana sana vina-reinforce hiyo belief
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…