OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Haya mijadala inaendelea kuhusu uwekezaji wa bandari, hoja nyingi zikitolewa kutokana na masharti ya mkataba huo ambao unaonekana utaathiri uchumi wa Tanzania badala ya kuuendeleza.
Kampuni ya Dubai inayosimamia bandari Zaidi ya 78 katika nchi 40 duniani imekuwa na kashfa kadhaa za ukwepaji kodi na rushwa. Mwaka 2008, Kampuni ya DP World ambayo ni kampuni ya tatu kwa ukubwa katika kampuni zinazoendesha bandari duniani iliingia Mkataba na Jamhuri ya Djibout wa miaka thelathini (30) kuendesha bandari ya Dorahel (Dorahel Container Terminal-DCT).
Mwaka 2014, kulitokea mgogoro kutokana na madai kwamba Kampuni ilitoa rushwa kwa mkuu wa Mamlaka ya Bandari wa wakati huo na hivyo kusababisha kuwepo Mkataba wenye masharti yanayoipendelea Kampuni ya DP World.
Serikali ya Djibout kwa kuona kuwa Mkataba huo ni tishio kwa mamlaka ya nchi (sovereignty of the state) na tishio kwa uchumi wa nchi (economic independence), iliamua mnamo tarehe 22 Februari, 2018 kuvunja huo Mkataba na kuichukua bandari ya Djibout.
Kampuni hiyo ilifungua kesi kudai fidia ya dola milioni 148 kupitia usuluhishi dhidi ya Jamhuri ya Djibouti baada ya mzozo huo.