Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Uzao wa Nyoka huwezi kuthibitisha BIBLIA kitabu kitakatifu,Pumzi ya Mungu!!

Jikite kwenye Mada. Rudi kusoma heading ya thread.
Kuna kitu nimegundua wewe ni mtu wa Blah blah sana na huna ulijualo kuhusu biblia we ni mfata mkumbo kama wengine..Nilitka uende kwenye biblia nikuone maana huko kwangu sidhani kama ntakuacha salama...

Halafu kingine nikusaidie Nyoka hazai anataga mayai 😅😅😅
 
Jikite kwenye mada.

Unazuia wenye Nia njema kutaka kujua umuhimu wa Kuoa mke au Kuolewa na mtu sahihi, Kutoka Kwa MUNGU!
 
Dah, so brain cracking!! Nakumbuka nikiwa nawafundisha wanafunzi wangu kuwa moja ya resolutions za Berlin conference ilikuwa "send more missionaries to Africa to prepare them for colonization and reduce opposition/rejection......" Hii ndio ile ulimwengu hadaaa...
 
Ila basi tu. Bora watu weusi tusingekuwepo. Mtu anakalilishwa uongo wa kudanganya wenzie na kuwatapeli na anaona raha. Huu ujinga waliojazwa,wangejazwa akili za maendeleo tugekuwa mbali sana. Wengine Wine eti ni damu ya msela. Vijidude flani vya ngano,eti vimeombea na mwili wa mtu ukaja humo. Kweli?! Hapana aise,hapana
 
Na watu wote ni wa Bwana pia, hata walevi, waasherati, waongo..wote ni wa Bwana...mnapofundisha watu msiwafundishe katika hali ya matananio ya kibinadamu..kuwa atapata mwenza mtakatifu, mpole, n.k..WAAMBIENI wafuasi wenu Mungu anaweza mpa mwenza, mkorofi, mlevi, mbishi, asiyeabudu, muasherati n.k na kupitia wote wawili wasaidiane madhaifu yao.wabadirishane, wafundishane..waishi maisha mema Duniani na wasaidiane kufika mbinguni.....

Na huu ndo uhalisia...au nyie wenzetu..mnaojiita walokole..mambo yeny yamenyooka na wenza wenu ni kama malaika????
 
Hata Biblia haijalazimisha kuoa ila imesema uwe towashi, usifanye zinaa...
 
Hii quote watairuka watajifanya hawajaiona
 
Danganyaneni tu. Hakuna cha kahaba wala nini. Tunachosikiaga,japo uhakika hatuna. Nae alikuwa anasubiri giza liigie ndo aende kuwashughulikia Maria na Marita. Sasa leo hii unamsifia na kumsafisha kwa lipi?
Hili la wanawake kuwa karibu na Yesu, kinawasumbua sana wanadamu wa kale hata sasa...

Ni kwakuwa mwanamke anaimani sana, ndio maana Maria alipoambiwa kuwa utachukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu hakukataa...

Mariamu Makdalena naye alipoponywa tu na Yesu hakuacha kutembea naye, Biblia inasema popote alipokuwa Yesu alienda.

Ni Imani tu, hata dada yake Mariamu Makdalena Matha hakuwa na Imani, ndio maana alilalamika mbona dada yake anakuwa karibu na Yesu.

Hili tunaliona mpaka sasa ukiwa na Imani sana unaonekana kuwa unamahusiano na mtume au Nabii, ni kwakuwa ukishamjua Yesu popote neno linahubiriwa utalifuata...

Ni ngumu sana kuelewa haya kama haupo kiroho zaidi. ..
 
Hilo 🙄ndilo swali lako!!

Nijibu, walipokutana bar na kuanza mahusiano, walioana au hawakuoana Hadi wanafikisha miaka 8 ya mahusiano na kupata watoto wawili?
Hakuna ndoa wanaishi tu na miaka nane imetimia na watoto wawili hawa walijazwa roho mtakatifu?
 
Biblia haijasema kama Yusufu alikuwa na mke mwingine na hata kama ni kweli lazima ukumbuke agano jipya na hata Kanisa lilizaliwa baada ya Kristo kufufuka.
 
Biblia haijasema kama Yusufu alikuwa na mke mwingine na hata kama ni kweli lazima ukumbuke agano jipya na hata Kanisa lilizaliwa baada ya Kristo kufufuka.
 
Biblia haijasema kama Yusufu alikuwa na mke mwingine na hata kama ni kweli lazima ukumbuke agano jipya lilizaliwa hasa baada ya Kristo kufufuka na Kanisa kuzaliwa rasmi.
I feel you bro..
Basi niambie Yakobo,Yusufu, simoni na yuda pamoja na dada zake walikuwa ni wa Mama yupi?

Kingine unafahamu Yusuf alikuwa ana miaka mingapi kipindi anamuoa mariam?

Tuanzie hapo kwanza ili nisije nikakubebesha mzigo mzito!
 
I feel you bro..
Basi niambie Yakobo,Yusufu, simoni na yuda pamoja na dada zake walikuwa ni wa Mama yupi?
Tuanzie hapo kwanza..
Ukisoma vizuri injili ya Marko, wametumia neno 'ndugu'....kibibilia (hata sasa) sio lazima muwe wa tumbo moja au baba mmoja ili muitwe ndugu hata mtoto wa baba yako mmoja au mama yako mdogo ni ndugu yako vile vile.

Marko 15:39
Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Marko 15:40
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;

Huo mstari wa 40 hapo juu unatuambia hao kina Yakobo walioitwa 'ndugu' walikuwa watoto wa mama yupi, ila hautambii kama walikuwa wa Yusufu Ila wamemtaja mama yao.

Hapo utaona kuna Mariamu watatu hapo yaani Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yesu na Mariamu mama yao kina Yakobo.

Hebu angalia na Yohana anasemaje....

Yohana 19:25
Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.

Yohana 19:26
Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.

Yohana 19:27
Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.

Ukisoma injili ya Yohana amesema alikuwapo mama yake Yesu, Umbu la mamaye (ndugu wa mamaye), mariamu wa kleopa na mariamu Magdalena.

Hapo ukichunguza utaona yule Mariam mama yao kina Yakobo huenda akawa ni Mariam wa Kleopa ingawa Marko hakutaja jina lake.
 
nime like mara tano!! si umeona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…