I feel you bro..
Basi niambie Yakobo,Yusufu, simoni na yuda pamoja na dada zake walikuwa ni wa Mama yupi?
Tuanzie hapo kwanza..
Ukisoma vizuri injili ya Marko, wametumia neno 'ndugu'....kibibilia (hata sasa) sio lazima muwe wa tumbo moja au baba mmoja ili muitwe ndugu hata mtoto wa baba yako mmoja au mama yako mdogo ni ndugu yako vile vile.
Marko 15:39
Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Marko 15:40
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Huo mstari wa 40 hapo juu unatuambia hao kina Yakobo walioitwa 'ndugu' walikuwa watoto wa mama yupi, ila hautambii kama walikuwa wa Yusufu Ila wamemtaja mama yao.
Hapo utaona kuna Mariamu watatu hapo yaani Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yesu na Mariamu mama yao kina Yakobo.
Hebu angalia na Yohana anasemaje....
Yohana 19:25
Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
Yohana 19:26
Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.
Yohana 19:27
Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
Ukisoma injili ya Yohana amesema alikuwapo mama yake Yesu, Umbu la mamaye (ndugu wa mamaye), mariamu wa kleopa na mariamu Magdalena.
Hapo ukichunguza utaona yule Mariam mama yao kina Yakobo huenda akawa ni Mariam wa Kleopa ingawa Marko hakutaja jina lake.