GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine kupiga kura?

  • Wana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Hawana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Sijui

  • Sijali


Results are only viewable after voting.
Kwenye harakati zozote wahanga wa kwanza wanakuwaga ni "collaborators." Wakati mwingine ndiyo huwa wahanga wakubwa au hata wahanga pekee. Umkhoto wa Sizwe wakati wanapigania uhuru waliua raia weusi wenzao wengi kuliko hata kuua wazungu. Walikuwa na haki ya kuwadhuru na kuwazuia hao wenzao "wasiuhalalishe" utawala wa makaburu? Binafsi kura yangu-sijali.
 
Demokrasia sio kulazimishana.
Sasa tueleze ni nani anamlazimisha mwenzake katika hiyo "demokrasia" unayoitetea wewe katika hali hii tuliyo nayo hapa, chini ya Samia..

Toka lini kuzuia uhalifu kukawa ni kosa?

Hao watakaokwenda kushiriki kwenye uhalifu; matokeo ya uhalifu huo yawe ni halali? Hii mantiki inatoka wapi?

Yaani hao watu watakaokwenda kupiga kura ndio wawe na HAKI ya kuwachagulia viongozi waTanzania wote, ikiwa ni pamoja na hao walionyimwa HAKI ya kushiriki kwenye uchaguzi?

Hapa kuna "demokrasia" ya aina gani hapa?
 
Mfano.

Ukipiga mabomu kituo cha uchaguzi, kisiweze kutumika kupiga kura, ukisema utapiga mabomu watu watakaojitokeza kupiga kura, unaweza kuwa umewalazimisha watu wanaotaka kupiga kura wasipige kura.

Huelewi wapi hapo.
 
Je, wanaharakati H, wakiona uongozi wa nchi K ni mbaya, unaharibu mchakato wa kura, wana haki ya kuwanyima
"---kuharibu mchakato wa kura---"; siyo UHALIFU?
Kwa nini watu washiriki katika uhalifu, badala ya kuuzuia? Unazungumzia 'falsafa" sijui ni falsafa za mambo gani hizi!

Kama kundi lenu mmeamua kushirikiana na wahalifu; kwa nini kundi lisilo penda uhalifu lisiuzuie uhalifu huo.

Unaamua kwenda kuwaweka madarakani kwa niaba yetu wote wahalifu; sisi tubaki tu tukichekelea na kukubali kuendelea kutawaliwa na wahalifu?
 

To be honest, Chadema hawajasudua uchaguzi vali wameondolewa kwenye uchaguzi ba seriksli kwa kutumia mbinu zao.

Vilevile sidhani kama kuba kundi smbalo mpaka sasa linana mpango wa kuwazuia wengine wasipige kura. Kibachofanywa ni kuwainfluence wadipige kura same kama CCM wanavuofanya kuwataka watu wapige kura. Kumbuka kupiga kura Tanzania ni hiari ya mtu siyo lazima.
 
Ondoa CHADEMA, ondoa CCM, ondoa siasa za Tanzania.

Zinaleta complications za watu kutoweza kujadili mada na hoja kifalsafa na kuishia kwenye politics.

Swali la msingi, bila kujali CHADEMA, bila kujali CCM, bila kujali siasa za Tanzania, ni hili.

Je, wanaharakati wa kikundi kimoja wanaoona uchaguzi si halali, si wa haki, wana haki ya kuwazuia watu wengine wasipige kura katika uchaguzi huo?

Au kuwazuia watu wengine kutumia haki yao ya kupiga kura si haki?

Kwa nini?

Hilo ndilo swali la kifalsafa na kidhahania ambalo watu wengi wanshindwa kulijibu kwa kuwa wanaishia kuangalia siasa.
 
kama uchaguzi unaendeshwa isivyo halali maana yake walioandaa uchaguzi usio halali wamefanya uhalifu kwa vile waliondaa uchaguzi wapo kwenye nagzi za juu ambapo raia wa kawaida hawakua na uwezo wa kuwazuia waandaaji wa uchuguzi kuandaa uchaguzi usio halali tuna muhesabia huyu anaye kwenda kushiriki uchaguzi kwamba ameungana na wahalifu walio kwenye ngazi za juu kufanya uhalifu kwahiyo tuna haki ya kumzuia muhalifu wa karibu ambaye tunamuweza sisi kama raia na ameamua kushirikiana na wahalifu walio kwenye ngazi za juu kufanya uhalifu
 
Nini maana ya haki ?
Na ungeelezea njia wanazotumia kuzuia ?
Maana kuna tofauti kati ya kuzuia na kushawishi.
Sasa wewe tuelezee jinsi wanavyozuia watu wasipige kura .
 

Sawa.

Tuendeleze mjadala.

Wewe unapata wapi haki ya kuhukumu huyu muhalifu na huyu si muhalifu?

Unahakikishaje ni muhalifu na si mjinga tu?

Unahakikishaje ni muhalifu, na si mtu mliyepishana mtazamo kifalsafa tu?

Kwani haiwezekani mtu akapiga kura kwa ujinga tu (kutokujua tu kuwa uchaguzi ni fake), bila ya kuwa muhalifu ( mtu anayejua uchaguzi ni fake na kuanua kuuhalalisha kwa makusudi)?

Unahakikishaje wewe mwenyewe si mjinga tu uliyekosea, na pengine yeye anayepiga kura yuko sawa kwa namna ambayo hujaielewa tu pengine anapiga kura kwa nia ya kuandaa ushahidi wa kuupeleka mahakama za kimataifa na taasisi za nje kuwatia hatiani viongozi na wewe ndiye umezembea hujafanya kazi hiyo ya kukusanya ushahidi tu?

Vipi kama unakosea wewe?

Kwani Demokrasia inakataza haki za wajinga kupiga kura kijinga?

Kwani mtu akitaka kuiharibu kura yake, una haki ya kumuingilia asiiharibu anavyotaka yeye?

Kwani haiwezekani mtu akajua uchaguzi huu una matatizo, lakini akawa hajakubaliana na wewe matatizo ni ya kiasi gani na yeye akaamua kushiriki ili ayamalize hayo matatizo, kwa kupiga kura, bila ya kuwa muhalifu, ila kwa sababu anaamini kabisa kifalsafa njia sahihi ya kumaliza matatizo ni kupitia kupiga kura.

Hapo huoni kuwa ukimkataza kushiriki uchaguzi utakuwa umemnyima haki yake ya kujiamulia mwenyewe anachotaka kufanya, umemuamulia wewe afanye nini, kwa namna ambayo wewe ukilazimishwa ufanye usichotaka hutafurahia?

Katika demokrasia, mfumo unaotoa haki sawa kwa wote, kwa nini wewe unajiona una haki ya kumpangia mwingine apige au asipige kura, na huyo mwingine hana haki ya kukupangia wewe kwenye jambo hilo hilo?
 
Hii mada yako ungeweka hukonhuko Clubhouse.

Nyie ndio mtaua hii nchi.

Sasa kama kura haina msaada, mahakama haija msaada,polisi wala bunge halina msaada mnataka watu wapate haki kwa njia gani??

Mnafikiri mtaemdelea kuteka watu kama nyumbu FOREVER??
 
Cha kwanza watakao zuia watu wasipige kura siyo wanaharakati bali ni sisi wananchi na tarehe 29 tunakiwasha

Tumeshaandaa mipango yote ya kuchoma kituo cha kura kilichopo hapa mtaani na hata mwenyekiti wa mtaan anajua
Kila kituo Cha KUPIGA kura kuchomwe moto
 
Una mtazamo gani kuhusu ANC kushughulika na Waafrika collabarotors wakati wa harakati za kupambana na makaburu wa apartheid Africa Kusini?
 
Una mtazamo gani kuhusu ANC kushughulika na Waafrika collabarotors wakati wa harakati za kupambana na makaburu wa apartheid Africa Kusini?
I am more interested in the abstract, philosophical conversation than politics.

Lakini hata tukisema tuangalie mfano, mfano wako katika mada hii ni logical non sequitur fallacy.

Collaborator ni nani? Na unamjuaje huyu ni collaborator kweli si mtu anayedhaniwa kuwa collaborator tu wakati kiukweli si collaborator?

Mfano wako, kwenye muktadha hapa, ni logical non sequitur fallacy katika hoja hii.

Kwa sababu, tukirudi kwenye mifano concrete, mfano Tanzania, si kila anayepiga kura ni collaborator wa CCM. Kuna watu, kwa ujinga, ama kwa kuamini kifalsafa kuwa kupiga kura ndilo jambo sahihi, na l8naweza kuiondoa CCM, wanapiga kura.

Hawa si collaborators wa CCM.

Na inawezekana wao wakawa sahihi, na wanaopinga kupiga kura wakawa hawako sahihi usiondoe uwezekano huu.

Pengine wanacheza some long strategy game ambayo nyie hamjaielewa mnawaona collaborators kwa sababu hamjaelewa strategy yao.

Nimetoa nfano wa mtu anayetaka kupiga kura ili akusanye ushahidi wa uchaguzi kuvurugwa na kushitaki mahakama za nje na taasisi za kimataifa.

Huyo si collaborator.

Huo ni mfano abstract, sisemi mtu huyo yupo. Lakini uwezekano tu wa mtu huyo kuwapo unakunyima haki ya kumkataza asitumie haki yake ya kupiga kura.

Hata kwa practical terms tu civil disobedience yako itakuwa inaharibu long term strategy ya kufikia lengo lile lile unalolitaka wewe.

Hapo ndipo utaona mfano wako ni logical non sequitur fallacy kwa sababu mfano wako unaleta habari ya kuwalinganisha wanaopiga kura wote na collaborators wakati that need not necessarily be the case.
 
Mkuu hujajibu swali, huko juu umewalazimisha watu wajibu swali lako bila kujali muktadha, uhalisia au contradictions za swali lenyewe sasa na wewe kuwa muungwana pia ujibu swali.

Una mtazamo gani kuhusu ANC kushughulika na Waafrika collabarotors wakati wa harakati za kupambana na makaburu wa apartheid Africa Kusini?
 
Uchaguzi uliokiuka vigezo ni haramu hata kwa yule anaetaka kupiga kura mana Sion uhalali wa tukio husika kuitwa uchaguzi.

Limepoteza taswira nzima hivyo ni dhulma kuu na uhaini mana wametumia rasilimali za raia kwaajili ya matakwa na manufaa yao binafsi na wale wanaowataka wao na SI nchi Wala Taifa kiujumla.

Nawaunga mkono.
 
Swali lako ni logical non sequitur fallacy.

Kwanza kabisa South Africa watu weusi karibu wote walikuwa wameungana kupinga utawala dhalimu wa makaburu, kulikuwa na ubaguzi wa rangi, hakukuwa na argumentative debate kuhusu mtu mweusi anayewaunga mkono na kuwasaidia makaburu kuwa ni mtu mbaya.

Tanzania mambo hayako clearcut hivyo.

Kuna very complex issues, kuna Watanzania wanaona CCM imeleta mabadiliko despite matatizo mengi kuwa yapo, wanataka kuichagua CCM kwa sababu wao wanaona kuwa, kwa mujibu wao, kuna afadhali.

Inawezekana hawa hawana high standards kama zako za kukataa utekaji, kukataa ufisadi, lakini wanaona wamejengewa daraja, wameletewa umeme.

Hawa hujaungana nao kwenye mambo mnayoyataka, wanayoyataka wao ni mambo simple na wewe unayoyataka pengine ni makubwa sana kwao.

Sasa unalazimishaje kuwaita hawa collaborators? Wengine hawajioni kuwa wanapigia kura CCM iwateke, wengine wajinga hawaamini CCM inateka watu. Hawajui ufisadi unaoanikwa na Mange. Hawajui hata kufuatikia mambo.

Sasa utawaitaje collaborators watu hawana hata information, hawana priorities kama zako?

Don't you see tgat you could be blaming the victim here?

Haya, kuna wengine wanaamini kuishinda CCM ni lazima uingie kwenye uchaguzi. Bila kujali hoja hiyo ni sahihi au si sahihi, ni hoja yao, wana haki ya kuitumia haki yao ya kupiga kura kuitimiza hoja hii.

Sasa hao wanaoamini wanaweza kuitoa CCM kwenye uchaguzi, wrongly or rightly does not matter. What matters is wanaamini hivyo, utawaitaje collaborators?

Unamhita mtu collaborator kwa sababu ana falsafa tofauti na wewe?

Na yeye akikuita wewe collaborator wa CCM kwa sababu unaisaidia CCM kushinda uchaguzi kirahisi bila hata kufanya kazi kubwa kwa sababu umesusia uchaguzi, utasemaje?
 
Mkuu,

Let's keep it a bit abstract.

Vipi kama kuna mtu mmoja kanyooka. Wa upinzani.

Huyu anajua kiujumla uchaguzi una figisu nyingi, unakosa uhalali.

Lakini hataki kwenda kwa kukariri.

Anajua yeye anakubalika sana na watu wa jimboni kwake, wapiga kura wake ni wengi sana kiasi kwamba hawezi kufanyiwa figisu, watampigia kura na kuzilinda.

Mtu huyu anataka kushiriki uchaguzi, apate ubunge, aende kuwanyoosha ma CCM bungeni.

Yani awe yule mbunge jeshi la mtu mmoja ukija mjadala kama ule wa kuuza bandari machawa wa CCM wote wakiupitisha yeye ndiye awe yuke mbunge pekee wa kuwasemea wananchi maneno yao na kuonesha kuwa kuna sauti tofauti na hawa machawa wa CCM.

Ukijua yote haya, huyu mbunge pamoja na wapiga kura wake nao utawalazimisha wasishiriki uchaguzi?
 
Lakini swali la mjadala si wanaharakati watazuia uchaguzi au hawatazuia.

Swali la mjadala si uchaguzi utakuwapo au hawatakuwapo.

Swali la mjadala ni, je, wanaharakati wana haki ya kuzuia watu kupiga kura katika uchaguzi?

You are missing the point as you go into the politics.
 
Me naona ni sahihi
Kama mwanaharakati atazuia Kwa ushawishi watu wasipige kura na kuhamasisha maandamano

Mbona hao CCM wanashawishi watu wapige kura na wasiandamane. Na mnachukulia poa

Me naona huu uchaguzi ni hatari ni sawa na sumu, kwaiyo hatuwezi kuwaona Watanganyika wanaenda kulamba sumu tukawaacha, tutawazuia
 
Kwanza kuweka rekodi sawa ni kwamba South Africa kulikuwa na collaborators wengi tu wa makaburu wakati wa apartheid, baadhi ya hao collaborators walikuwa ni machifu kama Zwelithini, watumishi na umma, jamii kama za Transkei, Ciskei, Venda and Bophuthatswana waliopewa uhuru ili wasipambane na makuburu.
Collaborators wa wakandamizaji huwa wanakuwepo katika kila harakati, iwe Zimbabwe wakati wa vita vya ukombozi, Kenya wakati Maumau movement au US katika harakati za civil rights movement.
Collaborators pia hutokana na mambo mengi ikiwemo maslahi ya kazi au biashara, uoga, ujinga, indoctrination, propaganda, ukabila, udini n.k Hata hivyo kuunga mkono oppressors kwa sababu zozote zile bado haiwezi kuwa justified hata kwa utetezi uliouweka hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…