Vifo vya wanaume kwenye ndoa vimekuwa vingi sana,lakini kwa namna moja au nyingine wanawake wamekuwa wakichangia vifo hivyo baba kama kichwa cha familia anahitajika kupambana kwa kila namna ili familia yake ipate kustawi na ni fahari kwa baba anayejali akiona familia yake ikistawi katika namna iliyonyooka.
Lakini kwa bahati mbaya wanawake kwa makusudi kabisa wamekuwa wakizihujumu juhudi hizi kwa kutufanyia hujuma kama vile kutubambikia watoto ambao sio wetu huku tukiwalea kwa moyo mmoja tukidhani kuwa ni damu zetu kwa sababu sisi hatuwezi kuwabambikia wao watoto ambapo mwisho wa siku juhudi zetu zinaonekana hazina maana mbele ya mwanamke baada ya baba mzazi halisi kujitokeza na kudai mwanae hali inayopelekea baba kuvunjika moyo na kuanza kuugua presha na visukari na hatimaye kifo.
Vile vile asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa hawana shukrani hawathamini juhudi anazozionyesha mumewe katika kuitimizia familia mahitaji yake muhimu,badala yake wamekuwa wakizibeza juhudi hizo kuanza masimango ndani ya nyumba inayopelekea baba kukosa amani na kupata mshituko wa moyo na kupelekea kifo chake. Kwani wanawake wengi wamekuwa hawajui ni jinsi gani mwanaume amehangaikia kile ambacho kimepatikana hapo nyumbani kabla ya kuanza kulalamika kuwa hakitoshi ndio ,aana familia nyingi zimebakiwa na wajane pekee.