Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Majukumu yao mengi so presha nje nje.Unamkuta mtu kaoa na watoto wake bado ana michepuko zaidi ya mitatu ambayo pia inahitaji matumizi bado wazazi na ndugu.Kwa hiyo unakuta kichwa kila saa kina mawazo.Ila sio kwa wote msije niponda mawe buree

Hapo kama unaniona vile,Hahahahaaaa!michepuko+stress+vyakula =rip.
 
Ahsante kwa mada nzuri kabisa nionavyo mimi.
1.Mwanaume anaemcha MUNGU huchelewa kufa ikilinganishwa na mwanamke asie mcha MUNGU Kwa uzoefu wangu wa niliowaona.note,hapa nazungumzia wale waliozeeka halafu mmoja akatangulia.(hapa inahusisha na Kutubu,kusamehe na Upendo)

2.Waheshimu baba na Mama upate miaka mingi na heri Duniani,Wanawake hawa ambao sasa ndo wazee walikuwa wanawajali sana wazazi wao ndo maana wameongezewa Umri wa Kuishi Duniani.

3.Mengine ni ya ziada ya kibinadamu zaidi...
 
KikulachoChako

Ni kweli mkuu comment zako huwa ndefu na zenye mambo ya msingi nikikuta comment ndefu iliyoshehen ndani humo hata bila kuangalia jina najua ni mkuu KikulachoChako
 
Last edited by a moderator:
Ngumu kumeza! ila ndio ukweli wanaume wanatangulia kufa, haijalishi umri wala nini hapa. Niliwahi kuhudhuria mazishi ya jamaa fulani, mchungaji alihubiri sana mwishowe alisema,

Jamani wanaume Mungu ameamua kufupisha maisha yetu, kwani wanaume wengi, (sio wote) huwaumiza wake zao na kusababisha wanawake kulia kila siku kumuomba Mungu awaondolee chanzo cha huzuni kwenye maisha yao!

Na chanzo cha huzuni hizo ni wanaume, kwa hiyo Mungu ameamua kufupisha maisha yetu ili wanawake wawe na amani! Na ukifuatilia kwa undani wanawake wengi waliofiwa na waume zao baada ya muda hunawiri na kupendeza kuliko walipokuwa wakiishi na waume zao. Mimi nilichukua mahubiri hayo nakuyaishi!
 
majukumu mengi mwili unachoka mapema... alafu nahisigi hata kupizz kunapunguza siku za kuishi .. si kila mwanamke anapizz wakati wa ngono ila mwanaume hadi mara tano ndiyo maana wanakufa

Duh idadi ya mabao ikiwa sababu wengi 40yrs wataisikia tu!

Anyway wanaume tunatumika Sana! Wanawake,kazi,pombe,sigara ukijumlisha na stress ya maisha na vile vile tunakuwa wakubwa kiumri kuliko wake zetu ni wazi mara nyingi tutatangulia!
 
Hoja yako ina mashiko kiasi fulani.Nadhani kunasababu nyingi sana zinazochangia mwanaume kutangulia kufa kabla ya mwanamke.

1. Mara nyingi mwanaume anaoa mwanamke mwenye umri mdogo kuliko wake hii ni sababu kubwa kuliko nyingine zote.Utakuta mwanaume kaoa mwanamke mdogo kamzidi umri wa miaka 10 - 20 sasa hapa unatarajia nani ataanza kufa kama si mwanaume.

2. Mwanaume anakuwa na majukumu mengi kuliko mwanamke hii inasababisha mwanaume kuanza kupata maradhi yanayotokana na mahanagaiko ya maisha kama HBP,Kisukari.......... ambayo yanachangia asilimia kubwa mwanaume kuwahi mbele ya haki kuliko mwanaume.

3. Wanawake wengi wanachangia sana vifo vya wanaume hasa hali za kimaisha vinapoyumba.

4. Wanaume wengi wanachangia vifo vyao wenyewe kwa kujirundikia majukumu ya kutunza nyumba zaidi ya moja.Ni kama vile dume la Simba porini linakuwa na streess kibao kulinda himaya yake ya majike isiingiliwe na madume mengine (territory).Tazama mwanaume mwenye wake wengi anavyopata shida kuhudumia familia zaidi ya moja utamwonea huruma.
 
Wanaume wanakufa mapema sababu ya hasira,mwanamke akiwa na hasira au akionewa atalia machozi hivyo sumu zote zitatoka kwa njia hiyo.

Ila mwanaume akiwa na hasira au mkewe akimuudhi atakaa kimya,ataumia moyoni atakiombwa msamaha atakubali lakini hawezi kusahau,hivyo kusababisha maumivu ya moyo na kupelekea kupata magonjwa sugu na vifo vya ghafla.

Poleni wanaume
 
1. Angalia umri wanandoa wanavyooana. Je mume na mke ni yupi anakuwa na umri mkubwa. Kumbuka kuwa kijana anaweza kufa lakini mzee ni lazima kufa kwa sababu kifo ndio mwisho wa maisha na uzee ndio umri wa mwisho
2. Wanawake kubaki wajane, ni wanaume ndio hasa huamua kuoa. Hivyo mwanaume akifiwa na mke ni rahisi kuamua kuoa mke mwingine ili asibaki mjane , mwanamke akifiwa atasubiri kama atatokea mume mwingine wa kumuoa

Pia scientifically life expectancy ya mwanamke inaizidi ya mwanaume, hivyo hata wakifunga ndoa na umri sawa Me atakuwa wa kwanza kuondoka!
 
Duh idadi ya mabao ikiwa sababu wengi 40yrs wataisikia tu!

Anyway wanaume tunatumika Sana! Wanawake,kazi,pombe,sigara ukijumlisha na stress ya maisha na vile vile tunakuwa wakubwa kiumri kuliko wake zetu ni wazi mara nyingi tutatangulia!

duh poleni sana
 
Katika bustani ya Eden kifo alitamkiwa mwanaume; mwanamke na viumbe wengine kufa ni matokeo
 



(Kwanini wajane ni wengi kuliko wagane??)


Mtalaamu saikolojia na mahusiano Dk. Chris Mauki anatoa sababu zifuatazo:

1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha ' life expectancy':

Kama unafahamu hili jambo linaloitwa 'life expectancy'; utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.

2. Ugumu katika kufunguka:
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa sana tu

3. Ugumu katika kusamehe:

Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

4. Tabia hatarishi:

Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

5. Ugumu katika kujali afya:

Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

6. Msongo wa mawazo:

Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo 'stress' ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Maisha sio mabaya kiasi hicho, maisha ni mazuri. Chagua kuishi

Chriss Mauki
 
Hili swala sina utafiti wa kutosha ila nadhani ni mipango tu ya Mungu,na kwa utafiti usio rasmi imebainika kuwa tokea kwenye kuzaliwa watoto wa kiume chini ya miaka 5 wengi hufa kwa maradhi kulinganisha na wale wa kike hivyo kupelekea hata idadi ya wanawake kuwa wengi kuliko wanaume.

Sasa inpokuja kwa wale wa kwenye ndoa kufa mapema na kuacha wake zao hili naona itakuwa ni kwenye lilelile swala la ku mantain ratio na bado nadhani kuwa resistance ya wanaume kuvumilia mikiki ya ndoa ni mdogo licha ya kuonekana kuwa wako masculine in nature.
 
Back
Top Bottom