Ngumu kumeza! ila ndio ukweli wanaume wanatangulia kufa, haijalishi umri wala nini hapa. Niliwahi kuhudhuria mazishi ya jamaa fulani, mchungaji alihubiri sana mwishowe alisema,
Jamani wanaume Mungu ameamua kufupisha maisha yetu, kwani wanaume wengi, (sio wote) huwaumiza wake zao na kusababisha wanawake kulia kila siku kumuomba Mungu awaondolee chanzo cha huzuni kwenye maisha yao!
Na chanzo cha huzuni hizo ni wanaume, kwa hiyo Mungu ameamua kufupisha maisha yetu ili wanawake wawe na amani! Na ukifuatilia kwa undani wanawake wengi waliofiwa na waume zao baada ya muda hunawiri na kupendeza kuliko walipokuwa wakiishi na waume zao. Mimi nilichukua mahubiri hayo nakuyaishi!