Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

ni life style tu.. kukaa na mambo mengi moyoni... hatupendi kutua mizigo kwa kuomba ushauri au msaada..hii hudhoofisha sana afya.
pia ulaji mbovu, wanaume wengi huwa tunakula harakaharaka hii hufanya tukose virutubisho vingi kwani msosi haumeng'enywi vizuri.
kukosa furaha/kununa,wengi hudhani ukauzu ni sifa kumbe wanajimaliza, kutabasamu,kucheka ni afya.
Lakini pia Mungu akiona upumzike hakuna namna nyingine hapo.
 
For Your Information
 

Attachments

  • 1440001860288.jpg
    1440001860288.jpg
    28.5 KB · Views: 147
Walaaah

Sojasoma kabisa ulichokiandika....

Hebu nisimulie ulichoandika basi??


Mkuu likes hazitoshi. Kama una kagelofrendi kalikuwa kanakuzengua na umeshakapiga chini, nitupie namba zake PM. Mi ndo mtaalam wa kuzoa vitu used. Kitaalam mi naitwa Tingatinga (siyo magufuli). Nina uzoefu na hii kazi kama Mugabe alivyo na uzoefu na uraisi. Sitakuangusha.

Ee Mungu mpofushe wife wangu BADILI TABIA asisome huu uzushi wa CCM kwenye hii post. Nsije kosa kura za Friends of Lowassa na chakula cha usiku wa manane wakati bundi wamelalana.
 
Ndo nshakasirika hivyo tayari....:wink2::A S confused:

Ila kumbuka maudhi,hasira,chuki,gubu ni moja ya sababu zinazo waondoa duniani haraka

Mi hapa nitalia machozi baada ya hapo nitajisikia mwepesiiii

Vipi bado una hasira? sitaki uondoke mapema
 
Mume miaka 30 Mke miaka 24 watakufa pamoja kweli?
 
Wanaume tunahaki ya kufa mapema kuliko wanawakea,hebu fikiri mtu mmoja analisha watu watano hadi nane (familia) alafu wote wanafikiri kwa kutumia kichwa chake kwenye maisha ya kila siku hadi maendeleo yao....sababu nyingine wanaume ndo watafutaji wakuu,huko hukumbana na uwezekano ajali kuliko yule anaebaki home
 



(Kwanini wajane ni wengi kuliko wagane??)

Mtalaamu saikolojia na mahusiano Dk. Chris Mauki anatoa sababu zifuatazo:

1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy” – Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.

2. Ugumu katika kufunguka – Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa sana tu

3. Ugumu katika kusamehe – Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

4. Tabia hatarishi – Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

5. Ugumu katika kujali afya – Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

6. Msongo wa mawazo – Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Maisha sio mabaya kiasi hicho, maisha ni mazuri. Chagua kuishi

Chriss Mauki

Ongeza hii: wanaume wengi ndiyo watafutaji kwenye familia,wanakuwa busy sana kiasi kwamba muda wa kupumzika unakuwa mfupi....pia ndiyo "decision makers" kwenye "family level "ugumu wa maisha huwafanya kuwa na" stress"
 
Back
Top Bottom