Hivi kwanini sehemu kubwa sana ya jamii zetu wanaume(baba)ndio huwahi sana kufa?
nishakutana na watu wengi sana ambao baba zao wamefariki ila mama zao bado wazima,ni kwa asilimia ndogo sana kuona mama ametangulia mbele za haki na baba akawa hai,huwa kuna kitu tunapewa wanaume au ndio asili ya jinsia yetu kuwahi kufa?
JAMBO HILO LIMEFANYIWA UTAFITI WA KISANYANSI!
Nitafupisha kabisa!
Mwanaume kwa maumbile ya asili ameumbwa na Sumu zinazoanza kufanya kazi pale anapo balehe.
Testosterone - tezi hii ndiyo inayomfanya Mwanaume kuwa jinsi alivyo:-
Fujo kuanzia kula,kuendesha vyombo vya moto,mahusiano na kazi ngumu ngumu na mambo yanayofanana na hayo!
Tezi hii inapoendelea kutoa misusumo huleteleza maisha ya Mwanaume kuwa maisha ya Vurugu na kutojali mambo muhimu ( RECKLESS BEHAVIOURS) ya afya na tahadhari zingine hasa katika rika toka miaka(14 - 40).Kitaalam kipindi hi huitwa testosterone storm.
Mbaya zaidi!!!! Tenzi hii kwa urefu wa maisha ya Mwanaume huendelea kuzalisha mafuta ya sumu(Cholesterol) au rehemu ndio maana wauza mafuta ya kula wanajitahidi sana kuweka lebo ya "Haina Rehemu" Wakijua fika mafuta hayo ni sumu na ndio chanzo cha matatizo ya Moyo na Damu.
Hivyo mwanaume huanza kuugua mapema sana na bila kujua shida kubwa ameumbwa nayo!
Kinyume chake Mwanamke ameumbwa na dawa inayomtibu magonjwa yake kwa haraka bila hata dawa hasa pale anapofikia kukoma kupata ada ya Mwezi
(menopause).
Hivyo tunavyozidi kuzeeka Mwanaume anakuwa na afya mbovu;wakati wakina bibi huwa wanaanza kunawili tena na kupata uzima kila siku(ostrogen) inakuwa na kazi ya kuzalisha dawa kutibu Wanawake.
Asante.
Chanzo: Harvard University gazette - 1998 - Why women live longer than Men.