Wanaume tuandae mapema maisha yetu ya uzeeni.
Ujue hakuna wakujakumtegemea financial sio wanao wala ndugu. Wala mke usimtegemee uzeeni.
Andaa mapema ukiwa kijana.
Punguzeni kuoa uzeeni na kuzaa uzeeni.
Maandalizi ya maisha ya uzeeni ni kwa wote,wanawake na wanaume na halina mahusiano ya utegemezi kwa yeyote kati yao,ila wakiwa pamoja,ndio maana ya kusaidiana na umaana wa kuwa pamoja.
Maisha kuoteza umaana au ladha,haimaanishi uzee.hayo huweza kutookea sababu ya changamoto kadhaa,hata kwa vijana.Ndio sababu wapo wazee wanaona maisha yana ladha nzuri sana hadi miisho kabisa ya maisha yao.
Mtoto unamleta duniani ili kutimiza amri ya Mungu ya kuijaza nchi (nadhani dini mbili zakubaliana na hili).Ila uzeeni,hata uwe na mabilioni pamoja na mali,msaada ya nguvu ya mtoto utahitajika,labda kama ulizaa majuha ama hukuzaa kabisa ama watoto ni washenzi kiasi ya kusahau kuna wazee waliowaleta hapa duniani.Na ni hapo hata ndugu watahusika (hasa kama nawe uliwajibika katika huuenzi undugu na hata urafiki kwa misaada n.k wakati una nguvu ujanani mwako).
Watoto wanazaliwa mda wowote ambao Mungu anamjalia mtu.Kwa usahihi,vema wakizaa mapema zaidi wakati mtu akiwa na nguvu NA UWEZO WA KULEA.Ila,si kila mtu Mungu humjalia uwezo huo mapema.Ktk dini,Ibrahimu alijaliwa mtoto uzeeni,na ndio akaleta uzao ulioenea sana leo huko waliko.
Kuzaa mapema bila maandalizi ndio kuleta viumbe duniani,wanateseka na kuishia kuja kuwa machokoraaa si ajabu na hata kuja kuwaona wazazi ama mzazi ni chanzo cha madhila yao.Huzai tu sababu una mbegu-sawa na huli tuu chakula sababu kipo.Hivyo,usahihi ni kujitahidi kuandaa mapema na kuzaa mapema,MUNGU akipenda na hali ikiruhusu kimalezi.
kila kitu chema chahitaji maandalizi makubwa na umakini sana,HASA KWANZA kuchagua mwenza (kabla hata ya huko kuzaa).Kuoa tu mapema (sijui unamaanisha ni mapema kiasi gani-nachukulia ukibalehe tu na kuwa na kashughuli LABDA).Kukurupuka na kukimbilia kuoa tu ndiko huku kuzalisha kuoa 'stress' ambazo zitapelekea labda hata malezi mabovu ya hao uliozaa 'mapema',maisha mafupi sababu ya tensions kwa muoaji na hata kuja kuharibu ndoa na watoto kuishi maisha ambayo hayakutazamiwa.
Haipaswi mtu kumpangia mda mtu mwingine kwani,binadamu hawafanani kamwe.Hili litamfaa huyu na lisimfae sana mwingine japo ni zuri.Akiga na kufuata mkumbo sababu tu nia ni njema ndio kuishia mahangaiko,majuto n.k.Kila mwenye akili ndogo tu ajua ni muhimu kutumia juhudi,maarifa na pamoja kudra za Mungu,kujiandaa mapema,kuoa mapema na kuzaa mapema ili kulea mapema wakati nguvu (na hata labda akili) zipo.Ila,si kila binadamu hupata hiyo baraka.Tupatapo hayo mapema,yabidi kushukuru Mungu na si kudhani 'kila mtu apaswa ayapate mda huo wa mapema na kila mtu anayapata ila ni kuzembea tu'.Ila,kwa mzembea kusudi kufanya hayo mapema,hilo ni tatizo lake mwenyewe na hasa ukizingatia risks za kuzaa uzeeni pia, hasa kibaiolojia,licha ya risks zingine.
Kuoa mapema na kuzaa mapema si sifa ama ujanja sana,na ndio chanzo cha kuvunjia ndoa kadhaa.Ila,kila mtu yapendeza akifanya hayo mapema HASA,kama alijiandaa mapema,na AKAFANIKIWA KUCHAGUA MTU SAHIHI 'mapema' na hatimae,kukubaliana WOTE WAWILI wazae mda upi na idadi gani ya watoto watakaowamudu.Kwani,sio ukishaoa tu ndio uzalishe ili watoto waje tu kiholela bila makubaliano na mipangilio ya wawili.Maoni yangu tu.Kila la heri