Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Jiulize kwa nn mama kaenda kwa watoto?

Ni uchizi mkeo kwenda watoto nawe ukaridhia na hakuna mwanamke mwenye akili atakyemuacha mume akaishi kwa watoto kwani ajiulize mama yake aliishi kwake au mama mkwe wake

Umaskini wa wazazi ndiyo chanzo kwani kwake hali milo mitano perday ila kwa mwanaye unategemea nini

Mimi najua cos nayaexperince now
 
Ramark,
Hilo ni suala la kiimani, Kama ni mtu wa Imani ni jukumu lako kumsaidia mzee wako kwa maana alikusaidia wewe ukiwa Mdogo.
Lakini wapo wanaume wengi tu wamezitumia Mali zao kuwainua watoto wao hata kwa kujinyima ili wapate elimu.
Mwanamke yeyeto hawezi kaa na mtu asiyemtatulia shida zake iwe ni pesa au mapenzi.
 
Wala sio wote umaskini unawafanya waende kwa watoto wao.
Wengine ni visa tuu na vitimbwi kwenda kusumbua wakwe zao. Wengine wanajidai hawataki kukaa mbali na watoto wao. Hasa Wamama wa watoto wa kiume.
 
Aisee kwa haya masuala ya mahusiano kuna mambo mengi sana. Usichukulie kirahisi hivo

Hili haswa linategemea na jinsi baba ulivyotengeneza mahusiano yako na familia yako, kuna familia huku mtaani baba ni suruali tu ama jina, visanga wanavyofanya kwa familia zao haviongeleki.

Umeona ya Mara juzi baba kabaka watoto wake watatu na mmoja kampa mimba, Just Imagine
 
Na wababa wahivyo ni wasumbufu hakuna mfano, na wengi wanalalamikia watoto wao,
ukirudi nyuma waliwaterekeza watoto sasa ili wasitengwe wanakuja na hilo lakutengwa

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Sawa, lakini nenda Ulaya na Marekani wazee wapo kwa kuwa hawategemei watoto isipokuwa chao sio timiza wajibu kwa familia but don't expects return bro
 
cha msingi ni kuinvest tu. jenga nyumba au nunua hata mbili. uzeeni unakua unakusanya kodi tu.
Yes hii usaidia kutokuwa Sana tegemezi na kuja walaumu watoto ambao nao hawana sababu ya Hali ya uchumi plus kuelemewa majukumu.
Japo wapangaji wanasumbua but huwezi kufa njaa.Pia siasa za kiafrica hazitabiriki waweza fanywa masikini ufe mapema anytime.

Pana mtu kimara alikuwa na nyumba zake za ghorofa plus mafrem hakujua njaa kabisa, Mr bulldozers akanyoka nazo mazima leo analala kwenye uwanja kazungusha manailoni kujisitiri umri umekwenda Hana pa kwenda ni mzee nguvu Hana tegemeo limeliwa na bulldozers utaacha vipi kufa haraka. Funzo sababu Siasa za afrika hazitabiriki usirundike vitega uchumi vyako sehemu moja utawahi kwenda mbinguni yakitokea mabadiliko mfano mafuriko, Moto, kimbunga. Wekeza Sasa nunua hata pori litakufaa uzeeni
 
Ukweli ni kwamba mara nyingi mabinti ndio huwatunza baba zao na watoto wa kiume huwatunza mama zao.

Ila wanaume kwa kupenda kuonekana vidume tunaliliaga kuzaa watoto wa kiume kuliko wa kike. tuombe Mungu sana tuzae na mabinti, wale ndio nguvu yetu kipindi cha uzee.
 
Sawa, lkn nenda ulaya na marekani wazee wapo kwa kuwa hawategemei watoto isipokuwa chao so timiza wajibu kwa familia but dont expects return bro
Utamaduni wao wale ni mfumo waliouandaa,pia wengine awakai na wazee wao sababu ya mazingira uwafanya mda mwingi kutokuwepo nyumbani na wazee uhitaji huduma za karibu na faraja Sana.Thus uwaweka kwenye vituo ili waweze farijiana wao kwa wao.
 
Ndio maana sisi wanaume tunaaswa sana kujenga bond imara kwa watoto wetu.

Mama zetu waliwazidi kete baba zetu, sababu wababa wetu walikuwa busy sana na kazi,kiasi cha kutohangaika na watoto kabisaa,mtu anashinda kazini akirudi misele, kwa washkaji vijiweni.akirudi ni usiku mkali anakoromea mama na watoto wanapigwa hovyo.

But siku hizi mjitahidi jaman, nenda katumikie beberu, ila ukirudi hakikisha hata mnashindana kucheza game la nyoka kwenye simu na mtoto, mnabadilishana story mbili tatu mnacheka na masomo nk.

Halafu hakuna upuuzi mwingine wababa mnafanya kama kufokea, kupiga mama au kumtamkia maneno ya dharau mbele ya wanaye. Hiyo ni mbaya sana. Watoto wanakuwa na rangi nyeusi kuhusu baba yao, na hata wakifanikiwa kutoka, wanamuwaza mama yao kwamba anateseka tu huko aliko, maana wanakufahama baba yao[emoji181]
 
Wala sio wote umaskini unawafanya waende kwa watoto wao.
Wengine ni visa tuu na vitimbwi kwenda kusumbua wakwe zao. Wengine wanajidai hawataki kukaa mbali na watoto wao. Hasa Wamama wa watoto wa kiume.

Bila shaka umemaanisha.

Vitimbi vya kwenda kuwasumbua WAKWE ZAO.
 
Hapana tusiogope kuwekeza kwenye nyumba, na kwa nyongeza ni vizuri ukawa unajishughulisha na mifugo kama kuku wa nyama au mayai, ng'ombe pamoja na mbuzi. Kitendo cha kuhangaika kuwalea mifugo kitakukeep bize sana hutapatwa na maradhi ya uzeeni mapema kwa sababu mwili unashughulika.
 
Unajua kwanini, coz mwanaume ana familia mbili mke na watoto wanakusubiria kipato nacho kidogo, watoto wa kike wengi ni rahisi kulisha watoto viporo na kutuma kwa wazazi wao. Kiasili wanawake wengi awakosi akiba au miundombinu, wewe Mia 5 utaacha change wao hata hamsini ni lzm wadai. Ujibanabana Hadi wanapata za kuwatumia wazazi
 
Mzazi aliyetuchukua majukumu yake kwa ukamilifu sizani kama watoto wanaweza mtenga mzazi, kina baba wengi hutumbua mali zao na michepuko nakushindwa majukumu kutimiza majukumu yake,wengi hupokea matunda ya ulezi wake mbovu, ushauri tunzeni familia yenu kwa ukamilifu mtavuna mema ya watoto na mke

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Yes kukaa tu ni lazima uzeeke mapema, but Bora kuku au mbuzi, ng'ombe na uzee wapi na wapi ukipigwa teke au pembe si utawahi kurudisha no
 
Kupambana sio kupata wengi tu wamepambana Sana ujanani Hadi uzeeni Hadi wamekata tamaa na awajapata.
Mimi nikiona mzee yeyeto anateseka najiona ni sawa na Mimi natamani nimsaidie sema tu bado sijapata.Wazee awahitaaji zaidi ya kula na kunywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…