Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Haya mambo hayatokei bahati mbaya na pengine mnadhani yanasababishwa na masababu makuuubwa kama vile; baba kutumbua mali na michepuko au kumpiga/kumfoka mke wake kipindi akiwa na nguvu la hasha! Sababu ya haya pengine ni ndogo ndogo sana zinazokuja kumpa β€œuthamani” mama wakati wa uzee dhidi ya baba.

Nimesema sababu ya haya ni ndogo ndogo sana kwakuwa si kila baba aliwahi kumtreat vibaya mkewe kipindi wakiwa na nguvu na si kila baba alikuwa anatumia mali zake nje balada ya kwenye familia, wababa wengine huishi na wake zao vizuri tu na bado uzeeni hupokea treatment isiyofair kutoka kwa watoto. Kinachowafelisha wababa wengi ni kutokuwa na uwezo wa kutengeneza bond na watoto wao isiyovunjwa/vunjika kwa urahisi na bond hiyo yapaswa aitengeneze mwenyewe baba na si kusubiri kupigiwa chapuo na mama. Kwenye hili linatufavour wanawake sababu ya vitu vidogo vidogo tunavyofanya kila siku kwa watoto wetu, mfano: wakiwa wadogo kuwapikia, kuwalisha, kuwabembeleza, kulala nao, kucheza nao muda mwingi, kuwaogesha, kuwapeleka hosptal, kuwapeleka shopping etc, na wakiwa wakubwa kuwa nao karibu na kuact kama daraja kati yao na baba yao, mfano: mtoto ana shida anamueleza mama, mama anaichukua anaipeleka kwa baba inatafutiwa suluhisho, then suluhisho hilo analibeba mama kulipeleka kwa mtoto as if amelitatua peke yake wakati kiukweli wamelitatua kushirikia na baba, au baba amelitatua nyuma ya pazia, mbele ya pazia amemrudisha mama kupeleka feedback, hapo mama anajizolea credits zote kwa mtoto.

Lazima tufahamu hivyo vitu vidogo vidogo wanavyovifanya wamama (care taking) automatically huwafutia hatia kwa watoto wao na kusababisha kupokea huruma ya moja kwa moja kutoka kwa watoto zao kuliko wababa, sijasema wanaume muanze kuwapikia, kuwalisha sijui kucheza na watoto huu ni uamuzi wa mtu binafsi kufanya au kutokufanya lakuzingatia wacheni kujitia ubusy uliopitiliza kwa madai ya kuwatafutia ada sijui kuwajengea nyumba jifunzeni kubalance mambo sababu inaonesha nature haiwapi favor katika hili. Nafahamu kubalance mambo ni ngumu sana, lakini lazima mkubali kuwa kuwa mwanaume unayejielewa inahitaji XXL efforts, na msidhani kuwa mama bora ni rahisi kiivyo mtu yakupasa ujitoe ufahamu kweli kweli, kila mtu ana ugumu wake.

Ukitaka kuamini ninayosema, chunguza mtoto aliyelelewa na single father uone kama kuna siku za maisha yake atamchagua mtu mwingine yeyote dhidi ya babayake.
 
Hakuna laana duniani hiyo imani iue

Unachopaswa kujua zile ni fedha za baba yako si za mama yako wala zako
Inawezekana baba yako alimuoa mama yako akiwa na kazi hivyo matunda ya kazi yake yamekulea na kumtunza mama yako

Mafao yake ni yake acha aamue cha kufanya kazi yenu ni kumsaidia ushauri wa namna ya kuzitumia ila ushauri wenu si amri

Msaidie baba yako kama tendo jema kwa kila mtu pia tambua kumtunza ni kudhihirisha heshima kwake ambayo ni amri ya Mungu
Heshima>>>>>>integrity

Mama hasiwe borakuliko baba yako

Unajua mateso ya baba yako?
Unajua kwa nn ameoa kibinti?
Uliwahi kuwa kati au ulichukua upande ulipofikiri maisha ya wazazi wako?

Unajua litakalokupata wewe?

Life only one who lives in can define it!

Waheshimu wazazi wako upate rehema na neema duniani

Ukishindwa ni jukumu la Mungu si wazazi na Mungu hatoi hukumu leo isipokuwa lessons na hukumu ni mwisho
 
Ramark,
Mkuu sisi wote ni wanaume ila unatetea upuuzi, kama mafao yake ni yake hata akiyatumia kuhonga, kwa nini awe mlalamishi kwa watoto ambao hakuwathamini kipindi akiwa na mali?
 
Mkuu sisi wote ni wanaume ila unatetea upuuzi, kama mafao yake ni yake hata akiyatumia kuhonga, kwa nini awe mlalamishi kwa watoto ambao hakuwathamini kipindi akiwa na mali?
Mlalamishi!!!? Nawakati anakukumbusha takwa la kimungu la kumheshimu
Kuheshimu inamaana kubwa ndiyo maana nilitumia 'integrity' kuonyesha uwote katika kuheshimu yaani kuanzia mawazo hadi mwili na wewe shauri basi
Ukiamua nawe timiza wajibu wako wa kumsaidia kwani nani aliwaambia wazazi wanalipiziwa kisasa?
Ukitengeneza kisasi kati ya wewe na wazazi wako wakati wanao wanashuhudia unafundisha nini? Na kanisani au msikitini unaenda!!
Na si kwamba nawe umeacha kuhonga!! Au kutumia 80% ya mshahara au fao lolote peke yako!
Vijana wa kiume tunasumbuliwa na tamaa ya kisasi kuliko mabinti ambao wao wanajua baba anapaswa apate hela ya gongo.kidogo au tumbaku lkn wewe unataka hata ukimpa hela lazima anunue sukari nawakati sukari mwili wake ni chache

Eleweni mantiki ya kuishi na familia

Ukiwa mkubwa tambua huwezi badili kwa haraka tabia mbaya ya mzazi wako, take time tena kwa wema

But your first priority must be your legitimate familiy before wazazi
 
Basi na ikifika jioni pambana na michepuko sio kuleta mizigo nyumba kubwa komaa huko huko, ndiyo maana wengi hula mpaka mabanzi kwa wake zao[emoji3][emoji3][emoji3], kama ni faraja kinacho warudisha huwa nini!
 
Oyaaa ngapi uko
 
Chief, kwanza kabisa mzee alipita tu kwa mama, alikua na mke wake wa ndoa, mama hakujua.

pili, nilijitahidi sana kurudisha majeshi kwa mzee. nikampanga aje bar flani tuongee jambo moja zito sana, baada ya bia kutuchangamsha akaanza kulia shida zake nikamwambia mzee hela yako ipo usjali tunywe bia, baada ya mda kidogo nikamwambia mzee tuagize chakula tule, akadai hio hela ya chakula iongezee kwenye hela uliyonipromise kunipa, kiukweli moyoni nilimshangaa sana huyu mzee. ni kwamba yupo kimaslahi sana hata kula chakula cha pamoja na mimi anaona kama natumia hela zangu vibaya ni kheri nimpe yeye akale na mwanamke wake mwingine.

akaanzisha tabia kila wiki ananiomba hela. nikaona kwamba mimi nimemfata kiupendo tujenge chemistry na ukaribu, yeye ananiona kama kitega uchumi kipya kimeleta kwenye maisha yake.

alipoharibu kabisa ni baada ya kuomba hela jumamosi ya kuamkia Pasaka nikamwambia sina, ndo akatuma mmeseji mreeefu wa kulaani watoto wake ambao hawamtunzi.

kiukweli tangu siku hio nilimwona hana maana. ni mtu ambae hataki kuelewa wewe mfuko wako upoje, yeye anataka shida zake zitimizwe kabla ya za kwako.

sina mazoea nae tena.
 
Honour and sense of duty
Basi na ikifika jioni pambana na michepuko sio kuleta mizigo nyumba kubwa komaa huko huko, ndiyo maana wengi hula mpaka mabanzi kwa wake zao[emoji3][emoji3][emoji3], kama ni faraja kinacho warudisha huwa nini!
 
Mwambie ukweli huo hapo juu ukisum up uzi huu

Laana haina mizizi dunia ache ajiliwaze na laana

Mwambie pesa yangu si yako be cold pliz
Mwambie nakusaidia na si lazima upate kila unapotaka na ajue kabla ya yeye kuna familia, wewe, mama yako, na wadogo zako

Kuomba hela kila mara kwa ajili ya matumizi ni upuuz now kama unaweza mpangie bajeti ya kila mwezi kiasi fulani kama huwezi mwekee miez miwili, mkatie bima ya afya kama ofisi inakuruhusu au ya mwaka reneuwable kisha muache

Usimuhukumu kwa matumiz yake kwani jukumu lako ni kutoa si kusimamia matumizi( mke wake huyo hakuhusu na wala hasidisturb uamuzi wako kwa baba yako)

Dunia hii na wazazi hawa wenye mitindo yao si lazima wabadirike unachopaswa ni kukubali ndiye baba, muaminishe mke na watoto, mama, ndugu zako na rafiki then maisha yatakuwa rahisi yaani kubali uhalisia uhalisia kisha ishi katika Honour, justice and sense of duty
 
Technical answer
 
Baba inabidi ujiandae na haya yote kwa kuwekeza katika ujana wako. Hata uzeeni watoto wakijitenga huwezi kufa njaa, vitega uchumi vyako vinakulea.
Kumbuka ma Baba hutumia mpaka senti yao ya mwisho hata ikibidi kukopa watoto wao wapate elimu,mahitaji na malezi Bora kwa mstakabali wa maisha yao lakini wakishalishwa sumu na mama zao ndio matokeo yake sasa hapo ni muda gani atajiwekea hakiba?
 
Kumbuka ma Baba hutumia mpaka senti yao ya mwisho hata ikibidi kukopa watoto wao wapate elimu,mahitaji na malezi Bora kwa mstakabali wa maisha yao lakini wakishalishwa sumu na mama zao ndio matokeo yake sasa hapo ni muda gani atajiwekea hakiba?
  • kuna kile kipindi cha kuanzia miaka 0 hadi 7 ya mtoto, kabla hajaanza primary unaweza kujijenga.
  • pia kuna kipindi cha primary na sekondary mtoto akisoma public school ada ni bure unaweza ukajimudu kujijenga.
  • pia kuna kipindi kile cha chuo mtoto akipata BOOM unaweza kujijenga.
  • pia kuna SACCOS na mabenki unaweza kukopa ukajijenga.
baba anaesema hela zake zote zinaishia kusomesha ni mvivu wa kufikiri.
 
Aisee wanaume tunapitia ktk majukumu mazito sana ktk kutafuta ridhiki mfano mie kazi nikuyo kuwa nayo before ilinibdi niwe naendesha gari.

Ktika pilika hizo ndani ya miaka mi 4.....
1.Nimepinduka na gari mara moja
2.Gari gari imekata tyroid hand mara moja nikaingia porini hii steering inakuwa out of control gari inakupeleka inakotaka
3.Nikabadlishiwa gari kilichofuata nikishaingia nayo porini out of control mara 2 unakuata mguu unachoma tyre ya mbele inachomoka...... so inakupeleka direction yake...
4.Nyingine usk nimesinzia baada ya kazi nzito.....kuendesha gari nikasikia ngu...ngoma igonga karavata inayoyoma mtaloni.....!
So kazi,zetu ili kupata kipato cha kukidhi familia kama kula,kusomesha na kuwa na maisha mazuri.

Wanaume tunachotaka kwenu kina mama ni mapenzi,na amani hatupendi kelele na ukosefu wa amani na maneno mengi hapo ndio tunaenda nje kujiliwaza na pombe na sigara na vimada.

So tunakuwa na misongo ya kazi,ndoa,na kendesha familia,kuingia ktk vimada ila nako yunakutana vimeo mwisho wa siku nako kunaleta shida na kuongeza invoice...

Kifupi maisha ya mwanaume ni taabu tupu na hapo ndio unagundua Baba zwtu wamepitia ktk shida japo tunajifanya hakuna kama mama.
Wababa mnanielewe changamoto tulizonazo,
Tunashindwa kula kazini ili mradi unachopata wale watoto na mama kazi ngumu mlo mmoja wenzio mke na watoto wanapiga lakaa 3......

Mwisho wa siku uzeeni baada ya kustaafu mwili ndio unajibu mapigo,mke anakuona you are nothing,watoto wanaona mama ndio kila kitu so unabaki mpweke tu.

wamama wanajitunza,wanavaa,wanjipodoa,wanakula vizuri,kazi zao sio hatarishi,wanakuwa krb sana na watoto wao maana muda mwingi wako nao we uko mzigoni upendo wao na watoto ni mkubwa mnoooo...

Tujitahidi kuwekeza ili akiba itufaaa maisha ya uzeeni,tuanzishe vibiashara vitusaidie uzee,tule vzr na tujitunze...tuishi maisha yenye furaha.....! amani na upendo,maisha ni sasa mbeleni taabu tuache visununu...!

Tusisahau kuishi na wenzetu/ke kwa akili...imeandikwa
 
Apo
Apo kwenye kichwa Cha familia tu ni kifo tosha
 
Mimi Sina utafiti wowote ila natazama mazingira tu
Chukulia kijana anafanya kazi ya bodaboda zaidi ya miaka kumi alafu mkewe yupo tu nyumbani na makopo yake ya mkaa,jamaa anaendesha basi dar to bukoba alafu wife wake ana mradi wa saloon...mwanaume wa kipemba ni mvuvi usiku kucha yupo baharini huku mkewe anajipara na kula vzr...usisahau Kuna makamanda wapo migodini huko lazima tufe mapema
 
[emoji30][emoji30][emoji30] imenigusa san tena mnoooh,
 
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™ Umenikosha mkuu na wanaume tuzingatie point yako ya mwisho tujiwekezee wake zetu tukishafika miaka 60 ndio wanatumaliza kiulaini Sana wakishirikiana na wayoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…