ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
Leo kuna sehemu fulani nilikuwa nimekaa zangu nakunywa soda. Karibu yangu kulikuwa na baba mmoja wa makamo kidogo, alikuwa meza ya pembeni anakunywa pombe na tayari alikuwa amelewa chakalii.
Ghafla nikamsikia anamwambia muhudumu: Usinione hivi, mimi nina mke na watoto watano. Nina gari nimepack hapo nje. Akaendelea kujisifia sana kuhusu maisha yake na misimamo yake, akisema yeye hayumbishwi na mtu.
Nikaanza kujiuliza moyoni: kwa nini mtu ajisifie kiasi hicho kwa mtu asiyemjua? Nikahisi kuna kitu hakiko sawa.
Baada ya muda mfupi akaingia mama mmoja mwenye kitambi, akamfuata pale mezani kwa hasira
We mpumbavu, mbona hupokei simu zangu? Simama twende!
Yule mwanaume aliyekuwa anajisifia muda mfupi uliopita akanywea kabisa Mama akachukua simu yake akaanza kuikagua pale pale huku amesimama, kisha akamuamrisha anyanyuke waondoke.
Kwa nje yule mwanaume anaonekana smart sana, ukikutana naye kwa umri wake unaweza kumpa heshima kubwa. Lakini nilichokiona pale kilinishangaza kumbe anaburuzwa sana ndani ya ndoa.
Hapo ndipo nikagundua kitu: labda baadhi ya wanaume wanaonekana wakali au wanaongea sana nje kwa sababu ndani ya nyumba hawana sauti.
Poleni wanaume wote mnaoteseka kwenye ndoa zenu. Inawezekana wengine wanakuja kulalamika mitandaoni kwa sababu kwenye maisha halisi hawapati nafasi ya kujieleza
kama kuna mwanaume humu JF anapitia huu moto nampa pole ya dhati ya moyo wangu🤝