Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

'Bila Kunyukwa'😀 ishakuwa Imani tena. Nahisi tunahitaji huduma ya ushauri nasihi
 
Mambo ya daddy ,mammy ,junior ni hatari. kwa lyfe style za kibongo unless uwe na Mtonyo wa kwenda.
Hawa watoto wanaolelewa hivi ndio mwisho wazazi wakipata ajali ghafla wakafa huishia kutaabika sana na dunia
 
Na hayo yote yazingatie 👇
 

Attachments

  • IMG-20241020-WA0006.jpg
    94.3 KB · Views: 1
Nashukuru mzee wangu kwa kunipa kipondo kilali pale nilipotoka nje ya mstari. Bila hivyo leo hii ningekuwa pusha au teja.
Ulitusumbua sana kijana mshukuru mungu mzee Ndomba alikupeleka kikamanda.
 
Zipi zitaje kwa manufaa ya wengi
 
Amini nakuambia...mzee aliekuchapa katika njia ya kukuelekeza uishi kwenye miiko na ukaja fanikiwa lazima utarudisha fadhila kwa kumtunz vzur...labda kama huyo mtt hajitambui..vivyo hivyo kwa mwalimu aliekuwa mnoko lkn alikuwa na nia njema kwako
 
Ukizungumzia kina mama hapo nakubaliana na wewe kabisa. Wengi ni wakatili hasa wale waliozalishwa bila kuolewa na kisha kuachwa wahangaike na watoto huwa wana uchungu sana wa kuachwa hasira wanamalizia kwa mtoto.
 
Hakika, umesema vyema waziri.
 
Naona wameanzisha sijui programs zao za child protection..ila ukiziangalia kwa jicho la tatu ni kutaja kutuaribia tu hiki kizazi....wanapitia sijui mashuleni na kuwaambia watt kuwa hairuhuisiwi kuadhibiwa kwa namna yyte ile ..huko huko wanapitisha na ajenda zao za ushoga....serikali inatakiwa uwe makinii sanaa na Hawa wanajileta kama NGO's
 
Nunua vitu vya jumla weka ndani acha kumtuma mtoto vitu rejaja dukani mara sukari robo, mara kiberiti kimoja, mara chumvi pakiti moja n.k
Mkuu hapa ndo unakosea...uchumi haulingani kwa wote...na haya ndo yanaleta makuzi tofaut ktk jamii
 
Mkuu hivyi unadhani ulivyo wewe namimi tunalingana kiuchumi?

Hujui Kuna familia Kila siku hununua mafuta 300 na sabuni ya kufulia na kuogea ndo hiyo hiyo? Kwa comment Yako inaonyesha wazi hujui hata uchumi wa watanzania walio wengi
Uko sahihi...pia hata hiyo kumtuma mtoto inamjengea hali ya kuish maziringira yyte ya kudekezwa na kupiga kazi pia
 
Jibu ni ndio. Ila tunajua ajenda iliyoko nyuma ya pazia mnataka tuishi kama ulaya Kwa sababu akili Zenu pamoja na kusoma kwenu hakujawahi wasaidia kabisa. Kila kitu lazima mabwana Zenu wa waambie Cha kufanya kuacha akiri yenu tu itatue vitu vidogo kama Hivi hamuwezi.

Hivi mlisomea utahira? Tuacheni sisi tulee Watoto wetu tunavyoona inafaa. Sio kutupangia
 
'Bila Kunyukwa'😀 ishakuwa Imani tena. Nahisi tunahitaji huduma ya ushauri nasihi
Tufanye Hivi muheshimiwa ninyi waleeni Watoto wenu kama Yai vile mbona inafaa nasisi tuwalee vile tunaona inafaa. Elimu Zenu Bado hajawahi kutusadia wa Africa Kila kitu mnafanya Kwa ku copy then mna paste. Akili Zenu zimedumaa na kukaririshwa na WA magharibi eti Kila wanachofanya wao ni sahihi tu.
 
Nashangaa sana sijui ni lini tutaanza kujiamlia na sisi mawazo yetu. Kama na kuleta napo tufundishwe Nini maana ya kuwa mzazi sasa.
 
Mimi nishapigwa tayari na wazazi wangu,ni zamu yao sasa
Kupiga mtu yeyote yule(hasa asie na uwezo wa kukurudishia) ni hatua ya juu kabisa ya uonevu.

Jiulize, wewe ukikosea, ni nani huwa anakupiga?
 
Mlete kwenye huduma ya marekebisho ya tabia
Hiyo clinic ni Kubwa kiasi gani?
Kama Kuna muongozo wa malezi Kwa watoto TZ yote (kama vile Hakuna kuguswa na fimbo Kwa kosa lolote lile). Hiyo clinic itatosha kujaza watoto watukutu TZ yote?
 
Ndo matoto yenu ya siku hizi changamoto kidogo anaanza kulia mara aseme ana depression, mitoto inakua milaini laini hadi unakua baba mzembe mzembe,

Malezi ni Tamaduni ukianza kuiga malezi ya watu wengine unapoteza utamaduni wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…