Je, Waziri Masauni apumzike? Akipumzika ndio Mwisho wa haya?

Masauni na hao wengine kosa lao liko wapi? wewe hufahamu sheria iliyopitishwa kuruhusu watu wa usalama wa taifa kufanya vitendo vya aina hii na wanalindwa na sheria? acheni kudivert attention kwa yule anapaswa kuwajibika kuaddress hii hali..Rais mwenyewe ndiye awajibike!
 
Sijajua.. utaratibu ukoje..

Hivi mpaka JESHI LA WANANCHI linaingia kazini kutetea Wananchi huwa kuna factors zipi zinapelekea JWTZ kuwa activated kwa maslahi ya Umma hasa ktk eneo la Usalama?

Nilikuwa nawaza tu kama upande wa pili hakueleweki basi wazee waingie kazini kufanya Ulinzi wa Raia na mali zao.
 
Tangu nchi hii iumbwe, wahalifu wapo, na wataendelea kuwepo, inawezekana hata sasa hivi kuna mtu anaiba simu hapo Tandale. Kwa hiyo hizo individual cases ndio zifanye waziri aondoke?
Tangu lini individual alitumia gari zenye namba za serikali?

Tangu link individual anaweza kumpeleka mtuhumiwa karakana ya polisi Ostabei?

Tangu lini individual anaweza kumiriki pingu na SMG?

............,.................... Wewe?
 
nawaombea wahusika na washiriki uchaguzi wa ndani wa chadema,

Mwenyezi Mungu awaepushe na kila hila na njama za muovu yeyote anae kusudia na kulenga kuhatarisha afya na kukatisha uhai wa wengine kwa maslahi binafsi ya uongozi na siasa...

Mungu awalinde, awanusuru na kuwapiganie katika hilo Aimen..

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mkuu britanicca , kwanza ubarikiwe sana kwa uwepo wako na nyuzi zako.

Mwanzo jf ilikuwa just a social media ya user generated forum, mtu ulikuwa una post chochote na kinapanda. Sasa jf sio a social media only, jf sasa ni social media na mainstream digital media, iko more responsible na contents. Ukileta kitu too hot kinachoweza kuunguza, kinaondolewa kwanza, kinachunguzwa ikithibitika ni kweli, kinapandishwa. On be the first to know, could JF be ni funga kazi zaidi ya mainstream media zote? Shuhudia hapa

Nakushauri ukileta zile sensitive za kule mahali, zipooze kwa kuondoa majina ya watu, maana sasa jf pia ni 'sehemu' juzi kati kwenye kongamano la maendeleo sekta ya habari, Mama aliitaja jf na alimuita Max "Mwanangu Max", Rais Samia aitaja JamiiForums, asema utoaji wa Habari umehamia mtandaoni kama ilivyo JamiiForums

Tone ya Rais Samia kumuita Max mwanangu was a loving tone, hivyo kitendo cha kutajwa kwa jina na kwa upendo na Mkuu wa nchi ni heshima kibwa!, Rais Samia ameiheshimisha sana jf, hivyo lazima Max arudishe heshima hiyo kwa kutumia kanuni ya reciprocate, ukiaminiwa jiaminishe, ukipendwa pendeka na ukibebwa bebeka!!.
Nimenote siku hizi kwenye ziara zote za Rais Samia nje ya nchi, reporter wa jf yupo

P
 
Kudisclose maeneo, maafisa na mission ni makosa ya kijinai.

Namini unafahamu vyema sana.

Hivyo wanajiepusha na mkono wa sheria wao na wewe pia.
 
Tutaongelea wapi sada kama jf ndio imekuwa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…