Je, Waziri Masauni apumzike? Akipumzika ndio Mwisho wa haya?

Kutajwa na Rais ndo kutafanya uyafumbie macho maovu eti kujiheshimisha


Acha uchawa mkuu
 
Serikali ni mimi, wewe, yule na huyu hapa, mimi naamini kwamba tatizo ni jamii, jamii kushindwa kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazo kuja, changamoto nyingi zinasababishwa na binadamu kwa makusudi ama kwa kutokujua
Kwa hiyo sisi wote hata tulioko huku TANGANYIKA Katavi, ni Mawaziri wa Mambo ya Ndani??
 
Kutajwa na Rais ndo kutafanya uyafumbie macho maovu eti kujiheshimisha


Acha uchawa mkuu
Ndiyo utaratibu, swali fikirishi je humu hukutani na hoja zenye tungo tata binadamu tuna uelewa tofauti utashangaa mtu ashupalia kitu ambacho hakijui ama hana utaalamu nacho hadi unabakk kushangaa
 

Muwe na shukrani. Serikali inapoamua kuwapoza kama kugharamia mazishi au matibabu shukuruni. Kuna mtu anaweza akakukanyaga asikupe hata pole. So mnatakiwa kuwapongeza Serikali kwa kuwaonea huruma kidogo. Chukueni pesa.
 
Wameruhusiwa na nani kuuwa?. Anaye ruhusu ni mtu kuuwa siyo Sheria. Kwani Sheria imejitunga. Kuna wapuuzi walioishiwa maalifa wanaona kujilinda na wizi na dhulma zao ni kuuwa wengine. Mkuu kwa akili yako unaona kuuwa ni kulinda?. Nakwambia ukweli Mungu bado ameamua kushika amani ya hii nchi ndiyo maana hata hao wauwaji wanapata nafasi ya kuuawa na kuona wao ni walinzi na wanastahili kuuwa na wanaona wanalinda. Siku Mungu akiamua kubadilisha akili ya watanzania hata hao wauwaji wenu hawatakua na nafasi hata ya kumnyooshea mtu kindole Chao. Mtu anashushwa kwenye Basi na anaenda kuuwawa na bado watu wanaona sawa?. MUNGU TUREHEMU.
 
Ninapinga alichoandika britanicca waziri awajibike wakati waliofanya uhalifu huu wanafahamika..hata Rais anafahamu mambo haya, kusema Masauni awajibike na kumuacha mteuzi wake wakati anafahamu wanaofanya matukio haya si sawa.
 
Kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume Muhammad (SAW), kuna aina saba za watu ambao watapata kivuli cha Arshi ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, wakati ambapo hakutakuwa na kivuli kingine isipokuwa cha Mwenyezi Mungu. Hawa watu saba ni:Imamu (kiongozi) mwadilifu –

1. Kiongozi ambaye hutawala kwa haki na uadilifu.

2. Mwanamume ambaye moyo wake umefungamana na msikiti – Yaani, anapenda sana ibada na mara kwa mara huswali msikitini.

3. Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu – Walikutana kwa ajili ya Mungu na wakaachana kwa ajili ya Mungu.

4. Mwanamume aliyekataa maasi – Mwanaume aliyekataliwa na mwanamke mwenye hadhi na uzuri kwa ajili ya kufanya dhambi, lakini akamwambia, "Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu."Mtu anayetoa sadaka kwa siri –

4. Aliyejitolea kwa siri kiasi kwamba mkono wake wa kushoto haujui kilichotolewa na mkono wake wa kulia.

5. Mtu ambaye anapomfikiria Mungu faragha, machozi humtoka kutokana na unyenyekevu wake kwa Mungu.

6.Kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu – Aliyeishi maisha ya uadilifu na kumtumikia Mungu tangu ujana wake.

Hadithi hii inapatikana katika Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim.
 
Hawa wazanzibari watatu wa mama, Abdul, waziri na kamishna wa mafunzo ndio vinara wa ukatili kwa watanganyika. Uzanzibari imeshamiri kuanzia ikulu ndio maana hatujasikia uhalifu huu ulifanyika huko visiwani
 
Iwe Sheria basi likiondoka kituoni na kukaguliwa hakuna kusimamishwa na yoyote hadi linafika linakoelekea!
 
Hizo ni primitive mythology tu, pole
 
Kuachia madaraka au kujiuzulu ni kitu ambacho hakimo kwenye akili yake!
 
Tangu nchi hii iumbwe, wahalifu wapo, na wataendelea kuwepo, inawezekana hata sasa hivi kuna mtu anaiba simu hapo Tandale. Kwa hiyo hizo individual cases ndio zifanye waziri aondoke?
Comrade ,hai kina masauni wasipo hukua hatua wataanza kupotea wao kama enzi zileeee za vifo vya ghafula vya kina kijazi!!

Halafu utakuja kutuandikia nini!!?
 
Ninapinga alichoandika britanicca waziri awajibike wakati waliofanya uhalifu huu wanafahamika..hata Rais anafahamu mambo haya, kusema Masauni awajibike na kumuacha mteuzi wake wakati anafahamu wanaofanya matukio haya si sawa.
Hupo sahihi. Maana wakati mwingine ruhusa anatoa mwingine alafu awajibike mwingine. Wafanyaji matukio wanafahamika
 
Labda aliwekwa kimkakati Hadi uchaguzi wa s. Mitaa upite kwa kufanikisha ushindi kwanza halafu ndio mwingine ateuliwe!!

Wamefanikiwa Kwa kiasi chake!

NB
Nitaendelea kuonyesha resilience hao jamaa wasinipate hata kidogo na Wala sitopost Ili wapate sababu zao za execution!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…