TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
إنا لله و إنا إليه راجعون
 
Kufuta kwake uchaguzi alisababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha yao hasa kisiwani Pemba, historia itaendelea kumwandika hivyo na familia yake wataishi na tag hiyo, why he went so low katika maamuzi yake ili kuilinda ccm,na make things .more craze eti naye alichukua form ya kuomba Urais thr ccm!
Hao waliopoteza maisha kama ni watoto wadogo kweli ni tatizo.
Ama kama watu wazima ni mihemuko Yao ya kisiasa na ushabiki usiokuwa na maana.
Any way kwenye ushabiki hata kwenye mpira watu wanakufaga!! Mimi siwezi kupoteza maisha kwaajili ya kumshabikia Zito,Mbowe au Lipumba huo ni ulimbukeni. Hawa wanasiasa Huwa wanatafuta riziki zao kwenye siasa lakini hapohapo wanawafanya walalahoi ndio ngazi na madaraja ya kuwafikisha kwenye shine zao! SIWAPENDI WANASIASA.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
Alichelewa Sana, ikiwezekana afe tena.
 
Wasalaam,

Acha Mungu aitwe Mungu yule fedhuli mpindua meza matokeo ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha nae Sir God Kampindua, huyo ndio Mungu sasa hamna Cha kibwengo, tumbili ama ngedere atabaki salama.

Sir God ni Mwamba Kampindua mpindua meza, ndio basi tena Jecha Salim Jecha atafunikwa na Dongo la futi 6 Leo.

Leo ni siku ya furaha Kwa wenye majonzi tulioumiziwa ndugu zetu na huyu fedhuli na dubwana Jecha.

Shukrani Sir God 🙏🙏🙏

Wabillah Tawfiq

Wadiz
Unaandika upumbavu halafu unasema eti "wabillaahil tawfiyq.??!!"
Unataja jina la Allaah baada ya kuandika maneno ya jeuri na uadui kwa muislamu mwenzio aliyekufa au wewe ni kafiri?!
Wewe muislamu kweli kuendeleza maneno ya visasi na marehemu.
Kama wewe siyo mtoto una uhakika hujawahifanya dhambi hapa duniani ? Sisi sote ni watenda dhambi, na sisi sote tunahitaji msamaha wa mola wetu.
Sera ya uislamu kwa waislamu wenzetu waliotangulia ni kusema:
ربنا اغفر لنا ولإخواننا الذين سبقونا بالإيمان ولا تجعل في قلوبنا غلا للذين آمنوا ربنا إنك رووف رحيم.
 
Mzee Jecha akiwa na mamlaka ya kusimamia na kutangaza maamuzi ya Wananchi juu ya ni watu gani washike mamlaka ya nchi, alishindwa kuifanya kazi hiyo na akatumia nafasi yake vibaya kwa kufanya vile ilivyompendeza yeye.

Kama haitoshi, Mzee Jecha katika uchaguzi uliopita katika hali ya kuwakejeli wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, alichukuwa fomu na kuomba kugombea Urais wa Zanzibar kwa mwavuli wa CCM. Hii ilikuwa ni kejeli isiyo kifani kwa Katiba na misingi ya utawala bora.

Nguvu na Kiburi vina mwisho, tuutengeneze mwisho mwema.
Madaraka hulevya, Ila Mungu akiweka usawa kwenye kifo, hata uwe nani, lakini hatujifunzi, Kuna dhuluma nyingine ilifanywa 2020 ya kupita bila kupingwa na kutengeneza bunge la Chama KIMOJA, lakini hatujifunzi.
 
Malipo ni hapa hapa akamsalimie Maalimu Seif atamkuta amemwandalia sehemu ya kujutia.
Mimi nadhani nyinyi ni katika wale wanaoamini kwamba WABAYA HAWAFI kwahiyo kwakuwa mnaamini nyinyi hamna dhambi mnadhani mtaishi milele hamtakufa!. Ingekuwa watu wanakufa kwa kulipwa mabaya waliyoyafanya nadhani kwa mtazamo wenu kuwa Jecha alikuwa mtu mbaya basi kwanini asingekufa yeye kwanza maalim seif akabakia?!
 
Yeye alipokuwa anadhulum alidhani ataishi milele, usituingize kwenye dhambi zake.
 
Back
Top Bottom