Jeff Leah: Yanga itafungwa 3-0 na Marumo na nina uhakika haitofuzu Fainal wala kuchukua kombe

Watu hamuishi maneno, ila Rivers ilikuwa hivyo hivyo. Watu walisema ina rekodi nzuri nyumbani akapigwa. Naona sasa tumehamia kwa Marumo. Ubora wa Yanga usibezwe.
 
Mkuu unachosahau ni kuwa game approach haiangalii tu mpinzani, inakuwa planned kulingana na uhitaji wa matokeo na sio mpinzani.

Game ya 2 leg na Marumo hakuna approach yeyote itakayoweza kufikiriwa kuwa Marumo atapaki basi na kusubiri kupiga counter attack.

Kwasababu ni game inayohitaji Marumo aahinde goli zaidi ya mbili ili apate nafasi ya kusonga mbele na hiyo ndio main approach ya game.

Kutomuheshimu mpinzani hujui ina maana gani really?

Au umeuliza kwa masihara tu

Kutomuheshimu mpinzani na kusema kumdharau mpinzani au kum-underestimate ni neno moja.
 
Huyu Jamaa anaweza kuwa ndiye Jemedar said
 
Watu hamuishi maneno, ila Rivers ilikuwa hivyo hivyo. Watu walisema ina rekodi nzuri nyumbani akapigwa. Naona sasa tumehamia kwa Marumo. Ubora wa Yanga usibezwe.
Watu walisema na ilifaa tuwaheshimu maoni yao.

Vile vile kuna watu waliwahi kusema na matokeo yakaja vile vile kama walivyosema, hatuwezi tukachukua hiyo kama fimbo ya kuanza kuwatusi.

BTW mimi niliwakataa Rivers United mapema siku ile ile ilipotolewa draw.
 
Hayo ni maoni yake ...mpira hauchezwi mdomoni!....

Mwambieni hivyo huyo leah...ndio maana jina la babaake ni la kike!....aache kuwa na mawazo ya kike kike! Kwenye vitu serious....
 
Yanga haijawani kufungwa goli nyingi hivyo tokea league ianze
 
Nataka kuona hiyo intensity ya Marumo unayoisemea kwa kuangalia mechi yao dhidi ya Pyramids, bondeni.

Kwa taarifa ni kuwa Marumo alipiga Shots on target 4 na kupata kona mbili tu. Pyramids alipiga 3 na kona 8. Possession aliachwa mbali na Pyramids.

Alipocheza na Yanga alipiga on target 4, kona 4 na possesion 52.

Kwa kuangalia mechi ipi walikuwa na intensity kubwa zaidi ya nyingine?
 

Labda ndio sababu GSM na yeye kawa serious kaamua na yeye atue bondeni
 
Yeah ofcoz we ni hater na unaumizwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya Yanga.
Upende Usipende Yanga inaenda fainaliView attachment 2623098

Mi sio hater niga, nasema ukweli nadhani ndio kinacholeta shida...

Fatilia takwimu za wakati huo sio tu unabisha, ili uone jinsi gani utavyojiona mbwiga....
 
Nakuuliza wewe ni kwa namna gani Marumo waliacha kuwaheshimu Yanga? Dadavua hoja yako kwa kuonyesha matukio katika mechi husika iliyochezwa pale kwa Mkapa.

Nimekuuliza, kuna mchezaji hakuchezeshwa kwa sababu zisizo na msingi? Maana hapa ndipo nitakuelewa kuwa waliwadharau kwa kudhani wale wa kikosi cha pili wanaweza kuleta matokeo.

Na kwa akili yako, unadhani Yanga watakuja na approach ya aina hiyo hiyo waliyocheza hapa?

Hebu acha maneno yako. Huenda wewe ndiye Leah 🤣🤣🤣. Angalia na maneno ya kuongea. Sema Yanga itafungwa, tutakubali. Lakini si kutuletea mpaka matokeo yaani 3 bila.

Hayo ni mahaba. Hakuna data zozote zinazosupport hoja yako na huyo Leah wako.
 
Intensity bila nidhamu, angalia kipindi Pyramids wakiwa golini kwa Marumo na pindi Yanga wakiwa golini kwa Marumo, observe reaction yake hapo utanipa jibu

Halafu

Intensity ilikuwa juu kulingana na Quality ya Pyramids iliwabidi wacheze counter attacks na kutegemea set pieces na sio kupishana.
 
Cha msingi kisinda,key Steven wasianze kwenye huo mchezo mudathir aanze first half,musonda ama mzize mmoja wao aanze
 
Eti ndio Leah mwenyew[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata alipocheza na Yanga walicheza kwa counter attacks. Mpira waliumiliki zaidi wakiwa kwenye eneo lao, si katika zone ya Yanga.

Ukweli ni kuwa Marumo walicheza kwa uwezo wao wote kutafuta ushindi. Na walionyesha kiu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…