Jeff Leah: Yanga itafungwa 3-0 na Marumo na nina uhakika haitofuzu Fainal wala kuchukua kombe

Jeff Leah: Yanga itafungwa 3-0 na Marumo na nina uhakika haitofuzu Fainal wala kuchukua kombe

Nakuuliza wewe ni kwa namna gani Marumo waliacha kuwaheshimu Yanga? Dadavua hoja yako kwa kuonyesha matukio katika mechi husika iliyochezwa pale kwa Mkapa.

Nimekuuliza, kuna mchezaji hakuchezeshwa kwa sababu zisizo na msingi? Maana hapa ndipo nitakuelewa kuwa waliwadharau kwa kudhani wale wa kikosi cha pili wanaweza kuleta matokeo.

Na kwa akili yako, unadhani Yanga watakuja na approach ya aina hiyo hiyo waliyocheza hapa?

Hebu acha maneno yako. Huenda wewe ndiye Leah 🤣🤣🤣. Angalia na maneno ya kuongea. Sema Yanga itafungwa, tutakubali. Lakini si kutuletea mpaka matokeo yaani 3 bila.

Hayo ni mahaba. Hakuna data zozote zinazosupport hoja yako na huyo Leah wako.
Mbona nimeeleza labda kama tu hunizingatii.

Huko juu nimeeleza namna Yanga wanapokuwa kwenye zone ya Marumo walikuwa wanauchezea mpira bila kuhofia hatari yeyote inayoweza kusababishwa na wapinzani wao.

Nani kakuambia mchezaji tegemeo kutochezeshwa ndio indication ya kuonesha wapinzani wame underestimate match?

Pale ambapo hau approach kila game with the same mindset and same level of preparation.

Nimekuuliza mechi ya Marumo na Pyramids uliwaona Marumo walivyokuwa wana react pindi Pyramids wapo kwenye eneo lao?

Did they react the same when playing here?
 
Geof Leah tatizo lake ni ushoga, ndiyo sababu ya kuondoka hata pale Mawingu...
Majizzo anatumia nguv na pesa nyingi kupush Vituo vyake tatzo lake anaokota Presenters wenye akili ndogo sana...
All in all, wanatumia vituo vyake kupata followers Instagram, maana kwasasa ukiiponda Yanga au Simba unaongeza followers...
 
Hata alipocheza na Yanga walicheza kwa counter attacks. Mpira waliumiliki zaidi wakiwa kwenye eneo lao, si katika zone ya Yanga.

Ukweli ni kuwa Marumo walicheza kwa uwezo wao wote kutafuta ushindi. Na walionyesha kiu sana.
Hapo ndio napo kupinga.

Counter attacks za tempo kulingana na matukio mafupi huwezi ukafananisha na counter attacks kama whole plan ya mchezo.

Na ndio maana ukiangalia umiliki wa mpira ulikuwa kwa Marumo.
 
Mnapenda ku catch feelings kwenye vitu vidogo.

Mchambuzi anaongea kupitia takwimu na sio kuridhisha upande eti kwasababu ni timu ya nyumbani au namna gani.

Hakuajiriwa kwa kazi hiyo na isingependeza boss wake kuona kila siku unajadili mlengo mmoja tu wa kimaoni.

Huyo Geaf Leah ni mshabiki mkubwa wa Mayele tena sana na anamuelezea kwa namna ya kiukubwa sana pengine tofauti na wachambuzi wengine wote ambao mimi nimewasikiliza chambuzi zao.

Hapo umem attack kupitia tittle tu ya uzi lakini naimani hujasikiliza sababu za msingi kwanini yeye ameona hivyo.

Huwa nashangazwa sana sometimes unakuta matokeo yamekuja kinyume na wachambuzi walivyobashiri basi kila mtu anaanza kuwarudia kuwatukana.

Hiyo sio fair na ukitaka kuona jaribu kufatilia tu hata hapo studioni wanakuwa wachambuzi wenyewe kwa wenyewe wanatofautiana maono.

Lakini angalia namna wanavyo argue kisomi kukosoa maoni ya mchambuzi mwezake kwa kutoa sababu za mashiko kuonesha namna gani mwezake hayupo sahihi.

Huwezi kukuta wanatukanana kwa hiki kiwango ambacho sisi mashabiki tumekuwa tukiwafanyia.
Sahihi kabisa mkuu.
Ai lavu yanga.
 
Bafikile bafikile bakyala ba Nzovwe..

Hana lolote. asitutishe na form 4 yake ya kenya
 
Bafikile bafikile bakyala ba Nzovwe..

Hana lolote. asitutishe na form 4 yake ya kenya
Ukuti nzovwe? Jo mwana jwa mbeya?

Ukumanya ku Nzowe

Nimetumia kumbukumbu zangu zooote kuunganisha hayo maneno
 
Mchambuzi nguli mwenye kujua vizuri kiingereza Goeff Leah kutoka sports headquarters Efm amesema ana uhakika Marumo atashinda tena goli kuanzia 3-0 na Yanga hatofuzu na hivyo ndoto za ubingwa zitaishia hapo.

Mimi kama mjumbe siuwawi, njooni mtoe ya moyoni, mtiririke na kuserereka
Akakojoe alale huyo
 
Mkuu,

Unataka tudadavue uhalali wa hoja ya huyo Mchambuzi? Ungepaswa kutiririka ni kwa namna gani yeye anaona Yanga akifungwa 3 bila huko kwa Madiba.

Mimi naanza kwa kukuletea matokeo ya Marumo Gallants awapo katika ardhi ya nyumbani kwa mechi zote 6 kisha matokeo ya Yanga akiwa ardhi ya ugenini, kisha tupime logic ya Mchambuzi wako.

Mpaka sasa Marumo Gallants kacheza mechi 6 nyumbani;
1.Mtoano
Vs ASSM ELGECO PLUS 1-0
Vs AL AHLI TRIPOLI 3-0

2.Makundi
Vs AL ALKHADAR 4-1
Vs USM ALGER 2-0
Vs SAINT ELOI LUPOPO 3-2

3. Robo Fainali
Vs Pyramids 1-0

Katika hizo mechi sita, ambazo kashinda magoli zaidi ya 3 (kwa scenario ya mchambuzi) ni mechi 3 sawa na 50%. Na katika hizo ambayo katoka na clean sheet ni ni moja tu dhidi ya Al Ahli Tripoli. Nasemea clean sheet kwa sababu hii ni knock out. Mwenzako kupata goli moja tu ni milestone. Akishinda 3-1, Yanga anapita.

Hivyo, katika mechi zake 6, iliyozaa uhakika ya kutoboa kwa goli 3-0 ambayo kasema Leah ni moja ambayo ni sawa na 17%.

Turudi kwa Wenzetu Utopolo kwa Matokeo ya Ugenini. Mind you, tunapaswa kuvitupilia mbali factors zingine na turudi kupima uhalali wa hoja za Leah kwa matokeo ya uwanjani kwa timu zote mbili.

Yanga mpaka sasa katika kombe la Shirikisho kacheza mechi tano;
1. Knock out
Vs Club Africain 0-1

2.Group Stage
Vs Monastir 2-0
Vs AS Bamako 1-1
Vs Tp Mazembe 0-1

3.Robo fainali
Vs Rivers United 0-2

Katika mechi tano, Yanga kashinda mechi 3 ambayo ni sawa na 60% na kutoka droo moja na kushindwa moja. Hivyo, Yanga anaonekana kuwa na rekodi nzuri ugenini. Na katika mechi zote sita, hakuna mechi ambayo kafungwa zaidi ya goli mbili. Hivyo, hiyo 3 ya Leah hakuna. Katika mechi tano, Yanga kafunga katika mechi nne, sawa na asilimia 80.

Sasa hoja yake ya kusema Yanga atafungwa goli 3-0 anaipata wapi? Uwezekano wa kushinda 3 anao, ila si bila. Matokeo sawa yana namna yake, lakini kwa data tu, mchambuzi huwezi kukurupuka na kusema atafungwa kiasi kadhaa cha magoli.

Uwezekano wa Marumo Gallants kushinda upo kama ilivyo nature ya mpira. Lakini si kwa kiwango cha kuaminishwa na Leah.

Twende mdogo mdogo.
Uchambuzi murua kabisa. Una nafasi yako pale Jangwani siku tukimfurusha haji manara
 
Mkuu,

Hapa tunachozungumzia ni nini? Mimi ninachokikataa ni hoja ya Yanga kufungwa 3 mtungi. Ulisema tunapaswa kutazama takwimu na hizo nilizokuwekea ni takwimu za timu zote. Moja ikiwa nyumbani na nyingine ugenini.

Kisha, hatupaswi kuangalia ni nani mwenye quality kwa wapinzani waliopita bali kwa timu zote mbili.

Ukitaka kusema hivyo, unakosea sana. Maana yake ungetuaminisha kwa mfano mechi ya Man United Vs Sevilla. Man U alitoka kukutana na timu yenye ubora na kumchabanga Barca. Baadae akakutana na Sevilla, akaogeshwa za kutosha.

Hakuna cha Pyramids wala Nini, hapa ni Marumo vs Yanga.
Hawezi kukuelewa maana tayari anaonekana ni mbabe wa Ruvu shooting anaetafuta faraja kwa Marumo. Anataka kupanua wigo wa uchambuzi wakati topic inatu limit kwa Yanga na Marumo
 
Hii mbona ipo wazi kabisa...
Bahlabane ba Ntwa!!!!
shaya amaxoxo uMarumo washaya izinja ngokulinganayo..
Matunda ya kuangalia Isidingo kwa zaidi ya miaka 20 tunaanza kuyaona. Msalimie Zukisa kama una wasiliana nae
 
Mchambuzi nguli mwenye kujua vizuri kiingereza Goeff Leah kutoka sports headquarters Efm amesema ana uhakika Marumo atashinda tena goli kuanzia 3-0 na Yanga hatofuzu na hivyo ndoto za ubingwa zitaishia hapo.

Mimi kama mjumbe siuwawi, njooni mtoe ya moyoni, mtiririke na kuserereka
Bado yataitwa maoni na maoni hayawezi kubadilisha rangi bluu kuwa nyekundu matokeo yatategemeana na game plan za walimu wote wawili
 
Mimi ni Simba, ila huyo jamaa huwa ni mnoko na elements za kichoko.

Huwa anapenda sana kuzipondea timu zetu zikicheza huko nje. Yaani huwa anapenda sana kupata kiki kwa kuona timu zetu za Kibongo hazina lolote.

Kila la kheri Yanga. Naumia, ila nawatakia mtoboe muende fainali.
Well said ni kweli huyu jamaa anajiona yeye ni Bora kuliko wachambuzi wengine anapenda Sana kukosoa wachezaji wetu ktk ligi ya kibongo anapenda Sana kuwasifia akina Shalulile na wachezaji wengine nje ya ligi yetu hata kama wachezaji hao wana viwango vya kawaida
 
Back
Top Bottom