Kila Mbongo
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 308
- 435
Upo sahihi kabisa!cdm wagombea
mbowe -2005
dr slaa 2010
lowasa - 2015
lisu -2020
Naweza kurekebishwa km nimekosea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo sahihi kabisa!cdm wagombea
mbowe -2005
dr slaa 2010
lowasa - 2015
lisu -2020
Naweza kurekebishwa km nimekosea
[emoji736][emoji736][emoji736]cdm wagombea
mbowe -2005
dr slaa 2010
lowasa - 2015
lisu -2020
Naweza kurekebishwa km nimekosea
Aisee tafuta 2005 mgombea Urais Chadema alikuwa nani? Na alipata kura 500,000mbowe hakuwahi kugombea urais.
kumbe na wewe ni kila,za
Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Kitu hujui nyamaza!Afunguke zaidi yaliyokuwa yanapangwa na Team Jiwe .
Mna maneno nyie, ha hahahaha haaaa!Huo ni wajibu wao
Hata Sisi walimu tunasimama kidete kuwafundisha wanafunzi
Hatupaswi kusifiwa kwa kufundisha ila tunapaswa kusifiwa kama tukiendesha magari au tukibeba bunduki na kupigania vita
Really!!?
akili yako haijaona tofauti Magufuli akiwa hai na akiwa amekufa?
unaelewa maana ya power vacum?
Upo nchi gani wewe ,,, ni katiba ya nchi gani walikuwa wanalinda? Maana ya bongo inavunjwa waziwaziSalute to General Mabeyo.
Wakati Majeshi ya Nchi nyingi za Kiafrika huwa yako mstari wa mbele kuvunja Katiba za Nchi zao JWTZ imeonyesha mfano.
Mbona hajaongelea ile kesi ya mchongo ya ugaidi ya kina Mbowe?View attachment 2270035
====
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anayemaliza muda wake Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ametaja kifo cha Rais wa awamu ya tano John Magufuli, na matukio yaliyofuata baada ya tukio hilo, kama moja kati ya changamoto kubwa alizokabiliana nazo kwani Jeshi lilipaswa kusimama kidete kuilinda Katiba ya nchi.
Mabeyo, aliyeanza kutumikia wadhifa huo mnamo Februari 6, 2017, baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli, akichukua nafasi ya Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange, alieleza hayo wakati wa mahojiano maalum na kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV hapo Juni 22, 2022.
“Nadhani [Watanzania] ni mashuhuda [kwamba] kwa mara ya kwanza, [Tanzania] tukampoteza Rais aliyekuwa madarakani,” Mabeyo, 65, alisema wakati wa mahojiano hayo.
“[Hiki] kilikuwa ni kipindi kigumu kidogo. Lakini tulisimama kidete, kwa utulivu mzuri, kama jeshi, tukitimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba, kuilinda nchi yetu [na] kuilinda Katiba.
“Na hilo likapita salama. Tukampokea Rais mpya, ambaye tunaendelea naye mama Samia Suluhu Hassan, na naamini kwamba tunaendelea vizuri. Nchi iko salama mpaka sasa. Wananchi wako watulivu, wanaendelea kufuata miongozo kama inavyotolewa na Serikali,” aliongeza Mabeyo.
Rais Magufuli alifariki mnamo Machi 17, 2021, kutokana na matatizo ya moyo, tukio lilioandika historia mpya kwa taifa la Tanzania ya Rais kufariki akiwa madarakani. Habari za kifo cha Rais huyo aliyekonga nyoyo za watu wengi na kuwakera wengine zilitangazwa usiku wa Machi 18, 2021, na aliyekuwa Makamu wake wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Samia aliapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita mnamo Machi 19, 2021, huku Jeshi la Ulinzi (JWTZ), ambalo kazi yake kuu ni kulinda Katiba na mipaka ya nchi, likipongezwa kwa kiasi kikubwa kusimamia uhamisho huo wa madaraka kwa utulivu mkubwa.
Matishio ya ugaidi
Mabeyo, ambaye aliagwa rasmi bungeni hapo Juni 14, 2022, huku Spika wa Bunge Tulia Ackson akimshukuru kwa “utumishi wako uliotukuka” kwa Tanzania, alitaja matishio ya ugaidi ambayo Tanzania imekuwa ikikabiliana nayo kwa miaka ya hivi karibuni kama moja ya “milima” aliyopaswa kuipanda wakati wa uongozi wake.
Matukio haya ni pamoja na yale ya Amboni, mkoani Tanga; Kibiti, mkoa wa Pwani; ugaidi huko mkoani Mwanza; na huko Mtwara kwenye mpaka na Msumbiji ambako magaidi wamekuwa wakifanya maisha ya jamii za karibu na mpaka huo kuwa magumu kwa kutokuwa na uhakika wa usalama wao.
“Kwa kweli, kipindi hicho kilikuwa kigumu sana lakini tunashukuru ushirikiano na wananchi, ushirikiano na vyombo vingine vya usalama, tumeweza kuhimili,” alibainisha Mabeyo kwenye mahojiano hayo.
“Lakini ni bahati mbaya kwamba majirani zetu [Msumbuji] wanakabiliwa sasa na tishio hilo [la ugaidi] kwa kiasi kikubwa. Na sisi kama sehemu ya ukanda wetu huu wa [Nchi za Kusini mwa Afrika] tumekubaliana kwamba tuwasaidie wenzetu,” aliongeza Mabeyo.
Migogoro ya ardhi
Kwenye mahojiano hayo pia, Mabeyo alikiri uwepo wa migogoro ya ardhi baina ya jeshi na wananchi, akisema mingi ya migogoro hiyo inatokana na Serikali kushindwa kulipa fidia kwa wakati lakini pia uvamizi wa maeneo ya jeshi na wananchi.
Migogoro ya ardhi kati ya jeshi na wananchi ni tatizo kubwa ambalo mara kadhaa Serikali imeahidi kutafuta namna bora za kukabiliana nalo.
Hivi karibuni, kwa mfano, Waziri wa Ulinzi Dk Stergomena Tax alikiambia kituo cha habari cha Dar24 kwamba Serikali iliandaa mpango wa miaka mitatu – 2020/2021 mpaka 2022/2023 –kwa ajili ya kutatua migogoro hiyo.
“Kwa sasa wataalam wapo sehemu mbalimbali za nchi ambazo zimeainishwa na kuna baadhi migogogoro imeshatatuliwa na kuna sehemu bado inaendelea kutafutiwa ufumbuzi,” Dk Tax amenukuliwa akisema.
Kwenye mahojiano yake na ITV, Mabeyo alisema jeshi linafanya kila linalowezekana kuhakiksha migogoro iliyopo sasa inatatuliwa na kwamba hakuna migogoro mipya inazalishwa.
Alipoulizwa anatamani kuona jeshi la aina gani muda huu ambao anaenda kustaafu, Mabeyo alisema kwamba anatamani Jeshi la Tanzania liwe la kisasa zaidi, huku likijitegemea na kutoa mchango zaidi katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
“Kwa nini wenzetu wanatengeneza zana wanatuletea kutuuzia sisi?” anauliza Mabeyo. “Kwa nini na sisi tusitengeneze zana za kututosheleza sisi wenyewe? [Wenzetu] wana hoteli, wana nyumba nzuri ambazo watu wanakuja wanakaa wanaongeza uchumi wa nchi. Na sisi jeshi letu liwe hivyo.”
Lukelo Francis ni mwandishi wa The Chanzo kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Anapatikana kupitia lukelo@thechanzo.com.
Katiba yenyewe imempa nguvu nyingi raisi..Magufuli alikuwa akisigina Katiba, sasa kwanini hawakusimama kidete kuilinda katiba wakati huo?
Nani kaandika hio caption kwa hio picha ..au takwimu za twawezaHe talks too much mpaka atatoa na siri za jinsi Jiwe alivyofariki. Anamaliza muda wake basi aondoke tu kwa amani....Utumishi uliotukuka!
View attachment 2270187
Kumbe yule jamaa alihoji hivo?? Daa mwamba hajaonekanaga hata shati...jiwe alikuwa nazo za mchongo na watu walipohoji hilo walipotezwa
RIP Ben Saa8
Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Kama hiyo jamaa ndo kamaliza form 6 sa hivi unahisi anaweza kumbuka aliekuwa mgombea 2005?? Si alikuwa bado mdogoAisee tafuta 2005 mgombea Urais Chadema alikuwa nani? Na alipata kura 500,000
Maza ana Masters kasomea Marekani.. Maza yule ni levels ingine sio kama wewe usiejielewaAlichofanya alizuia maccm yaliyotaka kumpindua Samia kisa Hana degree kama Sheria inavotaka wakati Mzee magu amedanji. Lakini ccm kila siku wanavunja Sheria yeye ameufyata. Asituchuze
" sisi kama jeshi tutakulinda" siku ya mazishi Chato.Mama nina jambo sitalisema hapa bali nitakuja ofisini kwako... Gen Mabeyo
Uongo Mbowe mbona aliruhusiwa kugombea uraisi wakati ni form six division zeroAlichofanya alizuia maccm yaliyotaka kumpindua Samia kisa Hana degree kama Sheria inavotaka wakati Mzee magu amedanji. Lakini ccm kila siku wanavunja Sheria yeye ameufyata. Asituchuze
Wala hajiandai kwa siasa. Amachosema nikweli na katika viapo vyao wanaapa kuilinda katiba ya nchi.Mjeshi anapostaafu na kujiandaa kuwa mwanasiasa hapo baadae lazima atafute kiki za namna hii…usitafute sifa kwa kutimiza wajibu wako…