Jenerali Mabeyo: Tulimpoteza Rais Magufuli, tulisimama kidete kama Jeshi kulinda Katiba

Uongo Mbowe mbona aliruhusiwa kugombea uraisi wakati ni form six division zero

Hakuna sheria inayosema Raisi lazima awe na digrii
Hebu toa kwanza comment kuhusu Kauli ua CDF achana na Mbowe
 
Wapo chini yake. Hata CIA ni kitengo cha Jeshi la Marekani
Kaka umezingua. CIA sio kitengo cha jeshi. Ni taasisi ya usalama inayojitegemea nje ya jeshi
Ila wanafanya kaz kwa ukaribu na jeshi

Cia ikiwa under ODNI(office of director of national intelligence).
Wakati majeshi yao yako under DOD department of defence.
 
Kwamba kabla magufuli hajakalia kiti mtangulizi wake aligoma kutoka ofisini? Mpaka ngome wakaenda kumtoa?
 
Mjeshi anapostaafu na kujiandaa kuwa mwanasiasa hapo baadae lazima atafute kiki za namna hii…usitafute sifa kwa kutimiza wajibu wako…
Tatizo kubwa hamuelewi changamoto kubwa iliyokuwepo baada ya kifo cha Magufuli.
Hamjui kuwa kuna watu ambao wapo mpaka sasa, walijitayarisha kuuteka urais.
Nyie mnaona jeshi lipo lipo tu, hamjui kuwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilisha tekwa na kuwa compromised.

Mama Samia siku ya kuapishwa alipelekwa Ikulu na Jenerali wa jeshi.
Hongera jeshi letu, lilifanya kazi nzuri.
 
Mabeyo atakula kuku nadhani muda mwingi uliobakia wa maisha yake. Bila yeye Samia asingekuwa rais muda huu.

Lile kundi lenye roho za mbwa mwitu halikutaka kumwacha hai baada ya kifo cha JPM, ni Mabeyo aliyempambania mpaka akaweza kumrithi JPM nafasi yake.

Kwa kifupi Mabeyo na IGP walicheza zaidi ya Pele.
 
Aiseeh...kumbe watu walipanga kujitwalia uraisi kinyume na katiba?
 
Hapo kasema yeye akiwakilisha JWTZ inamaana DIGIS na IGP wao walisimamia upande gani?? najaribu kuwaza tu.
Nchi hua ina jeshi moja tu. hapa bongo ni JWTZ, hizi nyingine hua ni taasisi, Ila bongo utasikia jeshi la polisi, sijui magereza, mara uhamiaji, mara jeshi usu. Yani kazi kuchanganya watu tu. Siasa mbaya Sana.
 
Story za vijiweni na kusadikika
 
Alichofanya alizuia maccm yaliyotaka kumpindua Samia kisa Hana degree kama Sheria inavotaka wakati Mzee magu amedanji. Lakini ccm kila siku wanavunja Sheria yeye ameufyata. Asituchuze
Hakuna sheria inayotaka rais kuwa na degree.
 
Natumaini siku moja tupate mtu hata kwa siri aandike kitabu kuhusu zile siku 15 za Magu kutoonekana mpaka kutangazwa amefariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…