WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
Hao sasa ndio Mashujaa wa Afrika walioipambania nchi kikweli kweli siyo jitu linatoka Chato na kuvaa kombati eti shujaa wa Afrika ,ni aibu kumwita mtu shujaa wakati alikuwa tapeli wa kufilisi matajiri,RIP SHUJAA KIWELU.Kama wameifaidi ni kwa kazi kubwa na heshima nyingi waliyoiletea nchi.
Tunaona watu wakifaidi bila kufanya lolote la maana.
Kwanini anazikwa Dar na wakati kwao ni Moshi?Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021
Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.
Pia soma
- Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu
Shujaa aliharibu kila kituTangu shujaa asepe naona hata taarifa zinatolewa na jeshi zinakua zimekamilika/ziko kisomi.
Tunaona mabadiliko kila sehemu.
Du umepiga nyundo balaaHao sasa ndio Mashujaa wa Afrika walioipambania nchi kikweli kweli siyo jitu linatoka Chato na kuvaa kombati eti shujaa wa Afrika ,ni aibu kumwita mtu shujaa wakati alikuwa tapeli wa kufilisi matajiri,RIP SHUJAA KIWELU.
Shujaa wa Mataga group of comedy.shujaa gani ujinga wa kujaana utukufu wsiokuwa nao. Alwaya dictators are like that, angalia Idd Amin kama kichaa
View attachment 1792666
View attachment 1792659
View attachment 1792661
Wachaga wengi Siku hizi wanaziikwa kwenye maeneo yao Dar wanaitika wito Wa Waziri Wa Ardhi Lukuvi anasema ardhi Moshi kumejaa makaburi tu hata kufanya maendeleo kunakuwa kugumu kila sehemu makaburi tu na hawataki yahamishweHuyu mzee kwanini wanamzika Dar? kwa nini asipelekwe kwao Moshi? Maana serikali inaweza kugharimia.
Anyway, maybe ni wish yake azikwe Dar. But I find it strange.
Nafsi yake ipumzike alipoandaliwa na mola wake.
Hakuna mtu anataka kuishi milele ila Tunataka vizazi tunavyoacha vipate Amani ambayo Magufuli aliwanyima watu
Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Hahah hii nakumbuka sana, George alikataa kabisa kumpigia saluti Luteni kanali ambaye aliamini waliingia jeshini kisiasa wao na kina makamba na wengine akina mkuchika, Lowasa etc. Jamaa aliongezewa muda akakataa katakata😃😃😃 mwaga mastori mzeeKuna nyingine ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ( Poti wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ) Jenerali George Waitara ila kwa leo naomba nisitiririke wala kuserereka nayo Kwanza.
Hizo ni Story za kwenye Chai sasa,Hahah hii nakumbuka sana, George alikataa kabisa kumpigia saluti Luteni kanali ambaye aliamini waliingia jeshini kisiasa wao na kina makamba na wengine akina mkuchika, Lowasa etc. Jamaa aliongezewa muda akakataa katakata[emoji2][emoji2][emoji2] mwaga mastori mzee
Hivi Waitara yupo wapi? Alibadilisha sana jeshi kutoka jeshi la kizembe la kimazoea very mechanical to jeshi la kisasa ndio aliona Kuna upungufu mkubwa wa viongozi jeshini maana waliobaki ni wale wazee kazi yao kusimulia walivyopigana Vita vya visiwa vya Anjuani na KAR. Wao hata kustaafu walikuwa wanaona sio haki maana wanahisi jeshi ni lao na hawakuwa wameinvest kitu maana wengi walikuwa na vyeo Ila shule hakuna.Kuna nyingine ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ( Poti wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ) Jenerali George Waitara ila kwa leo naomba nisitiririke wala kuserereka nayo Kwanza.
Waitara ndio baba wa Tanapa kuzuia ujangili. Askari wa kweli hawataki vipaza sauti ili wasikike. Huwa wanayofanya yanawaelezea wao ni kina naniHivi Waitara yupo wapi? Alibadilisha sana jeshi kutoka jeshi la kizembe la kimazoea very mechanical to jeshi la kisasa ndio aliona Kuna upungufu mkubwa wa viongozi jeshini maana waliobaki ni wale wazee kazi yao kusimulia walivyopigana Vita vya visiwa vya Anjuani na KAR. Wao hata kustaafu walikuwa wanaona sio haki maana wanahisi jeshi ni lao na hawakuwa wameinvest kitu maana wengi walikuwa na vyeo Ila shule hakuna.
Waitara alihakikisha anaanzisha Ile special program ya transit pale kunduchi unavuliwa uraia miezi 3 then monduli kulamba nyota zako fasta. Vijana unakuta kaingia lieutenant au captain Ila miaka kumi na mbili unasikia kalamba ukanali aisee wakati zamani ilikuwa ni ndoto ya maisha only few can survive to that rank.
Waitara alipiga stop kufuga kambini. Aliwaambia iwekwe maeneo maalum sio kila sehemu unakuta mabanda yamejaa mabaya na kuku.
I really would appreciate more about the general na amepotea yupo kimya sana haonekani kama bwana Davis
Historia ya nchi yetu huwa haiandikwi kabisa. Italeta shida sana mbele ya safari. wanywa kahawa wataanzisha mada zao zisizo na kweli na kuaminisha watuHujui hata historia ya nchi yako, Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa mpaka kufa baada ya kumuua aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Kreluu mwaka 1972.
Marehemu Jenerali Kiwelu atakumbukwa kwa kuongoza operesheni kali ya vikosi vya jeshi LA wananchi na kuyafurusha majeshi ya uvamizi ya nduli IDD Amin kwenye Ardhi ya Tanzania mwaka 1978.
RIP shujaa wa ukweli.
Mwinyi Kweli anatakiwa a Edit hicho kitabbu chake
Kabla kwenda kumkabili Raisi hakuwa peke yake walienda kwenye landrover na viongozi wengine wa juu JESHINI ila kiongozi akiwa yeye KIWELU na walienda sababu ya hasira waliyokuwa nayo
Walimwita waziri wa Fedha wakati huo Profesa Kighoma Malima awaeleze sababu ya mishahara kuchelewa na maslahi duni Jeshini ,wakati huo ukusanyaji kodi ulikuwa chini mifisadi ilikuwa kibao serikali ilkuwa hela haina!!
Profesa Malima ,Profesa wa uchumi akaanza kusema ngoja niwaeleweshe kichumi tatizo liko wapi tatizo kodi ndogo!!! Kiwelu akasimama akasema wewe karani wa wizara ya fedha kamwambie bosi wako atuachie nchi atupe masaa hata matatu tu tutakusanya kodi .UMESIKIA WEWE KIKARANI CHA WIZARA YA FEDHA
Profesa Malima akakimbia anahema akamwambia Mwinyi wanataka kupindua nchi.Hawajakaa muda KIWELU AKAINGIA IKULU NA TEAM YAKE WANA MIHASIRA KIBAO WAKAONGEA wakamaliza
Walipotoka mishahara ikapanda na maslahi kuboreshwa na kila askari mwenye kuanzia nyota wakakopeshwa magari ya kutembelea pick up kwa bei nafuu na wakaanzishiwa maduka yao ya kununua vitu ambayo ni duty free hayana kodi .Magufuli ndiye alikuja kuyafunga baada ya kuona yanatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi vitu vinaenda kwenye hayo maduka halafu vinashushwa maduka binafsi
Baada ya sakata lile Mwinyi alimuondoa uwaziri wa Fedha Profesa Kigoma Malima na kumuweka Jakaya KIkwete mwanajeshi mwenzao kuwa waziri wa fedha!!! mambo yakatulia
Okay okayWaitara ndio baba wa Tanapa kuzuia ujangili. Askari wa kweli hawataki vipaza sauti ili wasikike. Huwa wanayofanya yanawaelezea wao ni kina nani
Mwinyi Kweli anatakiwa a Edit hicho kitabbu chake
Kabla kwenda kumkabili Raisi hakuwa peke yake walienda kwenye landrover na viongozi wengine wa juu JESHINI ila kiongozi akiwa yeye KIWELU na walienda sababu ya hasira waliyokuwa nayo
Walimwita waziri wa Fedha wakati huo Profesa Kighoma Malima awaeleze sababu ya mishahara kuchelewa na maslahi duni Jeshini ,wakati huo ukusanyaji kodi ulikuwa chini mifisadi ilikuwa kibao serikali ilkuwa hela haina!!
Profesa Malima ,Profesa wa uchumi akaanza kusema ngoja niwaeleweshe kichumi tatizo liko wapi tatizo kodi ndogo!!! Kiwelu akasimama akasema wewe karani wa wizara ya fedha kamwambie bosi wako atuachie nchi atupe masaa hata matatu tu tutakusanya kodi .UMESIKIA WEWE KIKARANI CHA WIZARA YA FEDHA
Profesa Malima akakimbia anahema akamwambia Mwinyi wanataka kupindua nchi.Hawajakaa muda KIWELU AKAINGIA IKULU NA TEAM YAKE WANA MIHASIRA KIBAO WAKAONGEA wakamaliza
Walipotoka mishahara ikapanda na maslahi kuboreshwa na kila askari mwenye kuanzia nyota wakakopeshwa magari ya kutembelea pick up kwa bei nafuu na wakaanzishiwa maduka yao ya kununua vitu ambayo ni duty free hayana kodi .Magufuli ndiye alikuja kuyafunga baada ya kuona yanatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi vitu vinaenda kwenye hayo maduka halafu vinashushwa maduka binafsi
Baada ya sakata lile Mwinyi alimuondoa uwaziri wa Fedha Profesa Kigoma Malima na kumuweka Jakaya KIkwete mwanajeshi mwenzao kuwa waziri wa fedha!!! mambo yakatulia
Aliondolewa front line wakati wa vita ya Kagera sababu ya utukutu wake huo huo. Alikataa kumwambia Marehemu Sokoine, akiwa waziri wa ulinzi, mipango na namna ya kuvuka na kujenga Daraja lililovunjwa la Kagera. Yeye ndio aliongoza campaign ya kumtoa Nduli Amini ndani ya Tanzania. Kikosi cha kwanza kuvuka ili kujenga daraja la kagera kilikuwa cha makomandoo kadhaa wakiongozwa na "Kabunda", chini yake General Kiwelu. RIP Mwanajeshi.Huenda kidogo sasa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akapumua ( na nashangaa katika Kitabu chake hajazungumzia Mkwara aliopigwa na Marehemu ) wakati alipokuwa Rais wa Tanzania 1985 hadi 1995 kwani Marehemu alikuwa ni Shupavu, Makini, Asiyeogopa kama Haki na Sheria vyote viko upande wake na mwenye Kujiamini kama ilivyo Sifa Mama ya Mwanamedani ( Mwanajeshi ) yoyote yule duniani.
Ni kwamba Kipindi hicho cha Awamu ya Pili ( ya Rais Mwinyi ) Mishahara kwa Wanajeshi ilikuwa inachelewa sana Kulipwa hadi kupelekea Wanajeshi kuanza ' Kujisevia ' Bidhaa Madukani kwa Ubabe na wengine hata Kujiingiza katika Uratibu wa Uhalifu ili tu waweze Kujikimu.
Hali ilipozidi kuwa mbaya ( na hapa naiongelea 1985 hadi 1995 ) Marehemu huyu Afande Kiwelu alienda moja kwa moja kuonana na Rais Mwinyi ambapo alimweleza kuwa anampa Masaa machache tu awe ameshawalipa Mishahara yao Wanajeshi vinginevyo ' wanamtimbia ' mazima mazima pale Ikulu hali iliyomfanya Rais Mwinyi ' aufyate ' na Kuwatafutia Mishahara yao alikokujua na kuwapa mara moja ambapo Heshima ya Marehemu ndani ya Jeshi ( JWTZ ) iliongezeka maradufu na kuwa Mmoja wa Makamanda waliopendwa zaidi na Wanajeshi Kipindi chake cha Utendaji.
Na ni Juhudi hizi hizi za Marehemu Afande Kiwelu ndiyo zilisababisha tokea Siku hiyo Awamu zote za Marais mpaka sasa ( leo ) watacheza na Mishahara ya Kada zingine zote kwa Kuwacheleweshea ila siyo kwa Wanajeshi ( JWTZ ) na nahisi Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alihakikisha kila Rais anayechukuwa nchi basi anapewa Angalizo hilo ndiyo maana tokea Awamu yake hadi sasa sijasikia Upuuzi huo ukijitokeza tena.
Mwambieni Rais Mstaafu Mzee Mwinyi akifanyie ' editing ' Kitabu chake alichokizindua hivi karibuni na aliweke hili Tukio kwani lina Umuhimu sana kwa Watu kujua na wale ambao Kipindi hicho mlikuwa bado katika Zipu za Baba zenu na wale walioko pia Zipuni kwa sasa ili wakizaliwa wakutane nayo.
Kwani ni Jambo ( Tukio ) ambalo lilitokea ( lilimtokea ) Mzee wa Watu achilia mbali na lile la ' Kuwambwa ' Kwake Makofi akiwahutubia Waislamu alipowagusia Kutumia Condoms pale Wakitiana ( Wakitinduana ) ili Kujiepusha na Maambukizi ya UKIMWI ambao miaka hiyo ulikuwa umepamba sana Moto na ' Unawafyeka ' mno Watanzania.
Aliondoa watu kibabe ili kuruhusu mgodi wa kahama ujengwe. Ni kwanini aliondolewa frontline akapewa General Musuguli enzi zile za vita ya Kagera?..alipandishwa cheo toka Brigadier kuwa Major General wakati wa vita vya Kagera.
..baada ya vita vya Kagera aliteuliwa na Rais Nyerere kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga, akahamishiwa Rukwa, na baadae Tabora.
..alipandishwa kuwa Lieutenant General na kuteuliwa na Raisi Mwinyi kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jwtz.
..Raisi Mkapa alimpandisha cheo kuwa General na kumteua kuwa Balozi wa Tanzania Ufaransa.
..Baadae uteuzi wa kwenda ubalozini ukabadilishwa na General Kiwelu akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Malima alikuwa mtata sana. Haaaahaaaa
Aliondolewa front line wakati wa vita ya Kagera sababu ya utukutu wake huo huo. Alikataa kumwambia Marehemu Sokoine, akiwa waziri wa ulinzi, mipango na namna ya kuvuka na kujenga Daraja lililovunjwa la Kagera. Yeye ndio aliongoza campaign ya kumtoa Nduli Amini ndani ya Tanzania. Kikosi cha kwanza kuvuka ili kujenga daraja la kagera kilikuwa cha makomandoo kadhaa wakiongozwa na "Kabunda", chini yake General Kiwelu. RIP Mwanajeshi.