.Jenerali wa IRGC Mohammad Zolghadr, aliyechukua nafasi ya Larijani, kuna uwezekano mkubwa aliangamizwa jana usiku baada ya maficho yake kusambaratishwa!!
- Tunachokijua
- Kumekuwa na baadhi ya Taarifa zinazoeleza kuwa Jenerali Mohammad Zolghadr alisheshika nafasi ya Ali Larijani kama katibu mkuu wa Baraza la ulinzi wa Taifa (SNSC), ameuliwa baada ya makazi yake kushambuliwa.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa taarifa hiyo inayodai kuwa Zolghadr aliyeteuliwa na kuanza majukumu yake kama Katibu mkuu wa baraza hilo Machi 24, 2025 ameuawa si ya kweli ya kweli.
Hakuna chanzo chcochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa ya kufariki kwa kiongozi huyo. Ufuatiliaji kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu, umebaini kuwa vyanzo vya kuaminika taarifa pekee iliyochapishwa kuhsus kiongozi huyo ni kuhusu kuachaguliwa kwake.