I think Kama unaweza kutumia milioni 157 kujitangaza then ukapata watalii kutoka Dubai naamini sio tatizo since huwezi kupata hela kama hauna hela.
Ukiacha mambo ya mkataba wa Loliondo, waarabu wanaokuja kula maisha mngekuwa mnaona Ile convoy yao Wala isingekuwa hii million 157 ni ishu kabisa.
Mswahili usipotangaza yanakuwa maneno mkasema mbona Kagame anatangaza visit Rwanda kule Arsenal, Mara Kenya wanatangaza kwenye CNN, hivi unajua Tangazo moja CNN inalipiwa bei gani???
Kwa namna hii ya thinking tuna safari ndefu sana, nadhani wamefanya kazi nzuri mno wakati mwingine tusiwaze kwa kuangalia myopically.
Kama Kuna 10% hiyo anayejua aje aseme otherwise wacheni kazi ifanyike wandugu tutamtumia Mrisho Mpoto au Wanne Star mpaka lini? Kwanza alipwe milioni sita Yani nanii anamjua??? Unapoweka tangazo watu wanauliza hii bendera ya wapi? Then anapogoogle anakutana na Mt. Kilimanjaro, Serengeti etc hata agents wa watalii wanaona.
Let's be positive. Wakati mwingine ukiwa kiongozi halafu unafanya mema watu wanaibuka namna hii ndio unajikuta unasema wacha nipige hela zangu nimalize muda nikastaafu kwa raha.
Let's show appreciation kwa kufikiria positively, imagine Will Smith, Angelina Jolie wanapokuja wanalala Grumeti kule Serengeti wanaacha bei gani? Chumba kulala dola 2000 per night hapo hajataka kiwe customised ambapo huwa mpaka 12,000 dollars per night.
Sasa lazima tujiulize mtu mwenye hela zake aliyezoea kwenda Hawaii, Malibu, Malta, Santorini nk anaanzaje kujua mlima Kilimanjaro, Serengeti nk wakati agents wake wanachojua ni Alps mountains, Niagara falls nk? Lazima tukubali tutumie pesa ndio pesa itakuja, the fact tuna hivi vivutio haimaanishi kwingine hakuna, yaani Malaysia wanajitangaza CNN, Croatia, Switzerland yenyewe, Netherlands, sisi ni nani tusitangaze ili wajue? Tukiacha wataenda Kluger National park au Nairobi National Park or Masai Mara nako Kuna Simba, chui etc then tutaanza kulalamika.
On my side, Dubai is the best spot kwa kutangaza kwa sasa Tena tunapaswa kufungua information centre pale ambayo TIC na ministry ya utalii kwa maana ya Tanapa na foreign affairs wawepo pale Kama tourist information centre maana matajiri wa dunia na watu wengi sana wapo pale kustarehe so wanapata muda wa kuangalia na kuuliza hii ni wapi? Then atajiuliza Kuna nini huko mbona wameweza kutangaza?? I believe ni wazo zuri sana na la kupongezwa forget about gharama ya Tangazo 157 million think about Return On Investment.
Najua nitashambuliwa Ila tuwe positive sometimes.