Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa - Dubai lapambwa kwa picha za Bendera ya Tanzania

Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa - Dubai lapambwa kwa picha za Bendera ya Tanzania

Nilikua naangalia Station moja ya nje muda huu [emoji1256] UAE na Tanzania wana mpango wa makusudi kuwaondoa wamasai ngorongoro ili kubinafsisha hiyo hifadhi. Tuendelee kuomba hali siyo nzuri huko mbeleni.
Ni hilo ndiyo lengo kuu, ndiyo maana akina Maulid na genge lake walipewa pesa ndefu kwenda kuwatoa wamasai Ngorogoro ibaki wazi
 
Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa pale Dubai muda huu limenakshiwa kwa Bendera ya Tanzania mwanzo mpaka mwisho lote. Dunia nzima sasa inatazama maajabu haya kwenye Jengo hilo refu zaidi Duniani huku Utalii wa Taifa letu ukizidi kutangazwa. Yote hii ni matunda ya ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan Dubai na heshima inayopewa Taifa letu baada ya ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio makubwa sana ya Kiuchumi na Uwekezaji.

Hiyo ni pamoja na mafanikio mengine makubwa ya ziara hiyo ambayo ni Kusainiwa kwa Hati 36 za Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Trilioni 17.1 ambayo itatoa ajira 204,575 kwa Watanzania. Ziara ya Rais Samia Dubai imetulipa kwelikweli. Kazi Iendelee.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com

View attachment 2134475

View attachment 2134476

View attachment 2134477
Mbona ni Kama Bendera ya Congo DR sasa
 
Habari njema. Bila ccm isingeweza kutokea hicho. Hapo umasikini kwa kheri Tanzania
 
Kwani lazima kila kitu upinge/ulalamike?
Unajua maana ya kupinga au kulalamika?.Sidhani kama alichotoa huyo bwana ni kupinga au kulalamika.katoa tu mawazo yake mbadala.tujifunze tuheshimu mawazo mbadala kama ambavyo wewe ambaye hutoi mawazo mbadala unaheshimika.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri kila mtu anashangaa tunavyoshangilia tukio hili kama vile ni very exceptional [emoji2]. Hii nchi sijui wapi tuliingia chaka aisee [emoji55]

Hapo imetumika pesa! Sijui tunashangilia nini [emoji55]
 
Jamaa itakua wamepewa ngorongoro na mkoa mzima wa Arusha ili kufanya hivyo.
 
Jamani chunguzeni. Kama huu ni ukweli basi nchi hii imejaa wapuuzi wenye mamlaka kupita wakati mwingine wowote. Jee kama tukio hilo lilifanyika kwa nusu siku ni kiasi gani nchi imelipa? Na faida gani imepata kwa rangi ya bendera kuonekana hapo? Ujinga mtupu.
Kiasi hicho kikitumika vizuri kinaweza kufanya mambo mangapi ya maana?
Bado mavuvuzela ya mbogamboga yanashangilia!
Well, you must surely be wondering how much it costs to display an ad on the Burj Khalifa - the world's tallest building ever constructed. We will tell you that, to display a three-minute message, once between the time slots of 8 PM - 10 PM, one has to pay over Rs. 50 lakhs on weekdays, and the price increases by Rs. 20 lakhs on the weekends. Further, for two plays of a three-minute message/clip, it costs over Rs. 1 crore and Rs. 2 crores for playing your clips five times a night between 7 PM till midnight. A Dubai- based company manages all these projects and affairs and is known as, Mullen Lowe MENA. The content to go live must be submitted to the company at least a month before as it has to be reviewed by EMAAR, the owners of Burj Khalifa, before putting it out on the big screen.
 
Jamaa itakua wamepewa ngorongoro na mkoa mzima wa Arusha ili kufanya hivyo.
Hapo kuna mastaa wanawekwa siku za birthday zao sasa si aibu hii taifa zima kushangilia namna hii? Tumelogwa? Unfortunately ni pesa yako tu unarushwa pale! Tunarejea kwa kasi kwenye unnecessary issues [emoji58]
 
Nilikua naangalia Station moja ya nje muda huu [emoji1256] UAE na Tanzania wana mpango wa makusudi kuwaondoa wamasai ngorongoro ili kubinafsisha hiyo hifadhi. Tuendelee kuomba hali siyo nzuri huko mbeleni.
Safi sana!..

Si mnapumua nyie?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa itakua wamepewa ngorongoro na mkoa mzima wa Arusha ili kufanya hivyo.
Sasa hivi mgogoro huo unajadiliwa Aljazera katika Stream.
Marudio ya mjadala huo ni saa 5.30 na jioni saa 11.30. Ni vema tufatilie ulimwengu unatuzungumziaje katika suala hili la Ngorongoro
 
Back
Top Bottom