Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na 99% Lina wabunge wa CCM.Sema hili Bunge drama zinazidi sasa.
Swadakta, alipambana sana na OLUMBA kutoka Chiolu.Wago alitokea Aliakoro.Correct!,jamaa alikuwa noma sana ,mapigano ya koo kugombea bwawa la samaki
Kwa wale tunaopenda drama, hizi ni kama za Akina comrade Kipepe VS Pimbi, prof Ndumila vs Lodi Lofa, yaani Zina mwanzo mwisho haujulikani.CCM bhana !! sarakasi tupu !
Meno yanaumanaMbwa kala mbwa!
Wanakomalia "hadhi ya Bunge" badala ya maslahi ya wananchiHaya ndiyo mambo Wabunge wetu wanayeweza.
Kero za wananchi kama tozo na changamoto nyingine hata huwa hawajali kivile.
Shame on them!
Kama upinzani hawapo ,nani abughudhiwe?Magufuli alisema wanaccm wasibugudhiwe.
Kwa mara ya kwanza leo umeongea!GAIDI Hamza Msomali kafunika maigizo yote ya bunge la kijani
Nchi nzima kwa sasa hakuna mtanzania anayefuatilia kinachoendela bungeni. Hii ni kwasabb hadhi ya vikao vya bunge chini ya Ndugai imeshuka kiasi cha kufanana na vikao vya send-off.
Watu wengi wazito waliwahi kulisuta bunge hili. Mfano:-
"Bunge ni dhaifu".........Prof. Assad
"Bunge ni kibogoyo" ..@pascal Mayalla.
Sasa ili kulifanya hili bunge walau liongelewe Ndugai ameanzisha maigizo na akina Gwajima na Jerry Slaa. Wnachokifanya Jerry Slaa na Gwajima ni maigizo tu. Kwenda na vitabu vingi visivyotumika wala visivyoendana na muktadha wa suala lenyewe.
Gwajima anakataa kiti na microphone siku ya kwanza na siku inayofuata anagoma kukaa na kukubali mic. Ni maigizo at work.
Halafu ujinga huo kupewa headlines na media ili bunge lifuatiliwe.
Leo tunaambiwa Jery Slaa amegoma kufika mbele ya kamati hivyo akamatwe. Lkn wenye akili tushajua hii ni episode tu ktk hiyo movie.
Bunge limechuja na limekosa mvuto.