Yeyote atakaye kujua ugomvi wa hawa watu, lazima achimbe historia kutoka kwa Ibrahimu (Abraham) na kizazi chake chote kilichofuata mpaka kwa Yakobo na Essau...
Ni maswala ya ugomvi wa urithi. Na ugomvi huo hakuna awezaye kuuamua isipokuwa ni Mungu mwenyewe kwa wakati wake aliopanga mwenyewe...
Na kizuri kingine ni kuwa Taifa la Israeli na ardhi yake ndilo lenye haki zote 100% na eneo hilo wanalolitaka Wapalestina...
Mkono na nguvu ya ulinzi wa Mungu Yehova iko juu ya taifa lake teule. Chokochoko wanazofanyiwa wana wa Israel na taifa lao ni za kawaida kwa shetani kwa sababu ni kawaida yake kumpinga Mungu Yehova. Kamwe hawezi kuacha kumchokoza na kumchokonoa Mungu Yehova mpaka wakati wake utakapofika wa kufungwa milele...
Pamoja na yote haya, ukweli ni huu, hakuna wa kuweza kuwapiga hao akawaua wote na kisha kuwanyang'anya ardhi yao na kuishi hapo. Hayupo...!!
Israel limekuwa ni taifa ambalo mara zote limekuwa linawindwa sana ili ikiwezekana lifutwe kabisa duniani na kukiteketeza kizazi chote, lakini hakuna aliyewahi kufanikiwa na hakuna wa kufanikiwa leo, kesho na hata milele...
Mara nyingi ambacho hufanikiwa huwa ni kuwandoa kwa muda ktk ardhi yao na kukaa utumwani ktk nchi za watu wengine wakiteswa na kutumikishwa sana kama watumwa kama vile walivyochukuliwa utumwani Misri na kuishi huko kwa miaka 430, Babeli (Iraki ya leo) nk nk
Majaribio mengi pia yamefanyika kwa lengo la kukifuta kizazi cha Wayahudi (Waisrael) lakini nalo halijawaji kuwezekana pia na halitawezekana...
Kumbukeni nyakati zile za WWI & II. Shetani alijegeuza sura na kuwa binadamu wakiongozwa na Adolf Hitler akiwa na agenda kuu kukifuta kizazi cha wayahudi popote walipo duniani. HAKUWEZA...!!
Unaweza kuwaua wote, lakini ukibakisha wawili au watatu watazaana tena kwa wingi na kwa kasi ya ajabu sana na kuwa na nguvu isiyo ya kawaida tena na tena...
Hao (Israel/Waisrael) waacheni hivyo hivyo. Hilo ni taifa teule la Mungu na ndiko alikotokea Yesu Kristo .... Yeye (Yesu Kristo) ni wa ukoo huo pia...
Ukitaka kuishi na kubarikiwa, jiungamanishe na Israel. Ukitaka kufa kifo cha milele na kuishi maisha ya laana, jaribu kumshambulia na kulitakia mabaya taifa hilo na watu wake. Huko ni kugusa mboni ya jicho la Mungu...!!