Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi

Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi

Soma history kipindi UN anagawanya hyo Palestine na kuform Israel 1948

Wapalestine walkuwa wengi na wakapewa eneo dogo kuliko jews ambao walikuwa wachache

Na tangia hapo majews walikuwa wanaexpand mpka sasa inaonekana kma Palestine hamn nchi

Ndomn nikakwambia weka udini pembeni
Jewish states ilianza kama vijijij ndani ya miji mkubwa, baada ya frequently war ya kuvamiwa na waarabu Jews walianza kuji- organizes na kuunda Vikundi vidogo vidogo vya ulinzi..
Hilo eneo kubwa unalolisema wamelipata kupitia vita, ukianzisha vita ukipigwa mali zako ni halali kwa mshindi, hii kanuni hata Mtume Muhammad(S. A, W) ndo alikuwa anaitumia
 
Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

REUTERS: Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

Jerusalem imekuwa ikigonga vichwa vya habari kufuatia ghasia ambazo zimekuwa zikiripotiwa mjini humo kati ya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israeli ambazo zimewaacha mamia wakijeruhiwa mbali na mshambulizi ya kulipa kisasi kutoka pande zote mbili yakiripotiwa.

Ghasia hizo ziliongezeka siku ya Jumatatu usiku baada wanamgambo wa Kipalestina kurusha roketi kutoka ukanda wa Gaza hadi Jerusalem.

Kundi la wanamgambo la Hamas limetishia kuwashambulia maafisa wa polisi wa Israel baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa katika eneo takatifu la Waislamu mjini Jerusalem siku ya Jumatatu.

Likijibu, Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za wanamgambo katika ukanda wa Gaza.

Maafisa wa afya wa Palestina katika eneo la Gaza wanasema kwamba watu 22 wakiwemo watoto waliuawa katika shambulio hilo.
Jeshi la Israel limesema kwamba takriban wanachama 15 wa kundi la Hamas linalotawala Gaza ni miongoni mwa waliokufa.

Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

REUTERS: Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

Siku ya Jumanne, Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent, liliripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 700 walijeruhiwa katika ghasia hizo na maafisa wa usalama wa Israel mjini Jerusalem na eneo la West Bank.

Hizi hapa sababu tatu zilizopelekea kuzuka kwa mzozo huo.

1. Siku ya kusherehekea Jerusalem​

Jerusalem imeshuhudia ghasia ambazo hazajiwahi kutokea tangu wikendi ya 2017, zikisababishwa na jaribio la muda mrefu la Wayahudi kujaribu kunyakua nyumba za familia za Kipalestina katika eneo lililonyakuliwa na Israeli la mashariki mwa Jerusalem.
Ghasia hizo za Jumatatu zilizuka nje ya msikiti wa Al Aqsa , katika mji wa zamani wa Jerusalem.

Wapalestina waliwarushia mawe maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kutoka Israel ambao nao walijibu kwa kuwarushia risasi bandia za mipira na vitoa machozi .

Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent lilisema siku ya Jumatatu kwamba zaidi ya watu 300 walijeruhiwa.

Vikosi vya polisi vya Israel vilisema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi ilijeruhiwa pia.

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Msikiti wa Al Aqsa upo katika eneo takatifu linalojulikana na Waislamu kama Haram al Sharif, na Hekalu la Mlimani kwa Wayahudi.
Vikosi vya polisi wa Israel vilisema kwamba maelfu ya Wapalestina waliweka vizuizi katika eneo hilo wakitarajia kutokea kwa ghasia wakati wa maandamano ya Kiyahudi siku ya Jumatatu ili kuadhimisha siku ya Jerusalem.

Maandamano hayo yanaadhimisha hatua ya Israel kunyakuwa eneo la mashariki la Jerusalem 1967 , wakati wa vita vya siku sita ambapo ilifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wote.

Mji huo wa zamani upo mashariki mwa Jerusalem , ikiwa ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani ikiwemo:

Msikiti wa Al-Aqsa, Hekalu la mlimani, Ukuta wa magharibi wa dini ya Wayahudi na kanisa la Wakristo la mtakatifu Sepulcher.

Na eneo hilo linatambulika kuwa mji mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na ni mji wa tatu mtakatifu katika Uislamu.

Hatma ya eneo la Jerusalem mashariki ndio kiini cha ghasia kati ya Israeli na Wapalestina na kila upande unapigania haki yake.

Israel inasema kwamba eneo lote la mji huo ni mji wake mkuu , ijapokuwa hilo halitambuliwi na jamii ya kimataifa , na Wapalestina wanadai kwamba eneo hilo ndio mji mkuu wa taifa la Kipalestina litakaloundwa katika siku zijazo.

Wakati wa maandamano hayo ya kuadhimisha siku ya Jerusalem, mamia ya vijana wa Israel walipeperusha bendera na kuelekea katika maeneo hayo ya Waislamu , wakiimba nyimbo za kizalendo.

Wapalestina wengi wanachukulia hatua hiyo kama uchokozi.

Polisi wa Israel walitembelea eneo hilo kuamua kuwapiga marufuku Wayahudi wakati wa maadhimisho ya siku ya Jerusalem.

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitetea ulinzi uliowekwa.

"Hii ni vita kati ya wavumilivu na wasio na uvumilivu, kati ya wasiofuata sheria na wanaofuata sharia," alisema.

"Wale wanaotaka kuchukua haki zetu mara kwa mara hutulazimisha kusimama kidete, kama maafisa wa polisi wa Israeli wanavyofanya."

Kwa upande wake rais wa Palestina Mahmoud Abbas alishutumu vitendo vya Israel.

"Shambulio la kinyama la vikosi vya Israel dhidi ya waumini waliokuwa katika msikiti mtakatifu wa Al Aqsa na maeneo yake ni changamoto mpya kwa jamii ya kimataifa," alisema msemaji wake Nabil Abu Rudeineh.

2. Uwezekano wa kuzifurusha familia za Wapalestina

Wimbi jipya la ghasia linatokana na juhudi za siku nyingi za Wayahudi kuzifurusha familia kadhaa za Kipalestina kutoika katika makazi yao karibu na wilaya ya Sheikh Jarrah mashariki mwa jerusalem.

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017
.​

Umauzi wa mahakama mwaka huu uliounga mkono kufurushwa kwao ulizua shutuma kutoka kwa Wapalestina.

Mahakama ya kilele nchini Israel ilikuwa inatarajiwa kusikiliza kesi siku ya Jumatatu lakini kikao hicho kikaahirishwa kutokana na ghasia hizo.

3. Hali ya hofu wakati wa Ramadhan

Wimbi hili la ghasia linajiri katika siku za mwisho za mwezi mtukuafu wa Ramadhan.

Kizuizi cha Ramallah

Hofu ilitanda tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhan katikati ya mwezi Aprili , huku kukiwa na msururu wa matukio ambayo yamesababisha ghasia.

Wakati Ramadhan ilipoanza , ghasia za usiku zilizuka kati ya polisi na Wapalestina wakipinga vizuizi vilivyoweka nje ya lango kuu la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem ambalo lilikuwa limewazuia kukongamana eneo hilo usiku kucha.

Lakini ghasia hazikutokea Jerusalem pekee kwani sehemu nyengine pia zilirekodiwa katika mji wa Haifa , Kaskazni mwa Israel na mji wa karibu wa Ramallah katika eneo la West Bank.

Wapatanishi wa mashariki ya kati , wakiwemo Marekani, muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa wameonyesha kukerwa na ghasia hizo na kutoa wito kwa pande husika kuvumiliana.

CHANZO: BBC Swahili
Yaan habari hata haileweki kabsa,nmetoka job nmechoka,Nimesoma na hii habari imeniongezea uchovu zaidi
 
Warudi kwenye vitabu vya dini ndivyo vinavyosema kweli, huyo Israel anadekezwa sana na Marekani anafanya unyama anavyotaka pasipo kukemewa na haichukuliwi hatua yoyoye.
Hayo ndio maagano na SHETANI

Kwa SHETANI utapata kila kitu lakini ni lazima mufanye makubaliano,na siku zote SHETANI hana mkataba mwepesi na upendezao mbele ya wanadamu na MUNGU muumba

We hujiulizi kwanini ndoa za jinsia moja zinapigiwa na zinafungwa makanisani sehemu za ibada ambapo maovu yanakemewa?,ndio wale walishafanya mikataba na SHETANI na SHETANI anawapa kila kitu nguvu,uchumi na kila kitu lakini SHETANI mambo yake yanakwenda na yuko very smart

Na siku Palestinians watakapopigana kwaajili ya ALLAH kwa ajili haki ndio siku ya ushindi kwao ndivo ilivoandikwa
 
Kwa mda mrefu kumekuwepo na mzozo kati ya wa-Palestina wa- Israel. Wa-Palestina wanadai hapo wa- Israel walipo ni kwao kwa asili.

Swali langu, je madai haya ni sahihi na halali kiasi gani?

Je, wakati wa- Israel wanawekwa hapo wao walikuwa wameenda kutalii wapi?
 
Lipumba hela aliyopewa kuihujumu CUF imeisha hivi sasa analialia tu wamwongezee,na aliyemuingiza chaka hivi sasa yuko motoni
nilimshangaa eti anawatetea waperestina, kwani walikuwa wapikipindi waislael wanachukua ardhi wanayodai ni yao...
 
Yeyote atakaye kujua ugomvi wa hawa watu, lazima achimbe historia kutoka kwa Ibrahimu (Abraham) na kizazi chake chote kilichofuata mpaka kwa Yakobo na Essau...

Ni maswala ya ugomvi wa urithi. Na ugomvi huo hakuna awezaye kuuamua isipokuwa ni Mungu mwenyewe kwa wakati wake aliopanga mwenyewe...

Na kizuri kingine ni kuwa Taifa la Israeli na ardhi yake ndilo lenye haki zote 100% na eneo hilo wanalolitaka Wapalestina...

Mkono na nguvu ya ulinzi wa Mungu Yehova iko juu ya taifa lake teule. Chokochoko wanazofanyiwa wana wa Israel na taifa lao ni za kawaida kwa shetani kwa sababu ni kawaida yake kumpinga Mungu Yehova. Kamwe hawezi kuacha kumchokoza na kumchokonoa Mungu Yehova mpaka wakati wake utakapofika wa kufungwa milele...

Pamoja na yote haya, ukweli ni huu, hakuna wa kuweza kuwapiga hao akawaua wote na kisha kuwanyang'anya ardhi yao na kuishi hapo. Hayupo...!!

Israel limekuwa ni taifa ambalo mara zote limekuwa linawindwa sana ili ikiwezekana lifutwe kabisa duniani na kukiteketeza kizazi chote, lakini hakuna aliyewahi kufanikiwa na hakuna wa kufanikiwa leo, kesho na hata milele...

Mara nyingi ambacho hufanikiwa huwa ni kuwandoa kwa muda ktk ardhi yao na kukaa utumwani ktk nchi za watu wengine wakiteswa na kutumikishwa sana kama watumwa kama vile walivyochukuliwa utumwani Misri na kuishi huko kwa miaka 430, Babeli (Iraki ya leo) nk nk

Majaribio mengi pia yamefanyika kwa lengo la kukifuta kizazi cha Wayahudi (Waisrael) lakini nalo halijawaji kuwezekana pia na halitawezekana...

Kumbukeni nyakati zile za WWI & II. Shetani alijegeuza sura na kuwa binadamu wakiongozwa na Adolf Hitler akiwa na agenda kuu kukifuta kizazi cha wayahudi popote walipo duniani. HAKUWEZA...!!

Unaweza kuwaua wote, lakini ukibakisha wawili au watatu watazaana tena kwa wingi na kwa kasi ya ajabu sana na kuwa na nguvu isiyo ya kawaida tena na tena...

Hao (Israel/Waisrael) waacheni hivyo hivyo. Hilo ni taifa teule la Mungu na ndiko alikotokea Yesu Kristo .... Yeye (Yesu Kristo) ni wa ukoo huo pia...

Ukitaka kuishi na kubarikiwa, jiungamanishe na Israel. Ukitaka kufa kifo cha milele na kuishi maisha ya laana, jaribu kumshambulia na kulitakia mabaya taifa hilo na watu wake. Huko ni kugusa mboni ya jicho la Mungu...!!
 
Kwa mda mrefu kumekuwepo na mzozo kati ya wa-Palestina wa- Israel. Wa-Palestina wanadai hapo wa- Israel walipo ni kwao kwa asili.

Swali langu, je madai haya ni sahihi na halali kiasi gani?

Je, wakati wa- Israel wanawekwa hapo wao walikuwa wameenda kutalii wapi?
Huruma yao ndio iliyowaponza.
 
Arabs hao walihamia tu na waliwakuta wayahudi na Wasamalia na Makabira mengine ya Waisrael wakiishi hapo Tawala vamizi za Kiislam ndio zilijaza arabs hapo from Arabian Peninsula... and from 1948 hadi 1968 Gaza ilikuwa under Egyptian rules After war Israel akatake over Gaza and Sinai hadi pale walipoingia mkataba wa Amani na Israel. So Gazan ni Egyptian japo Egypt alikataa kuwapa passport watu wa jimbo la Gaza japo niAsili moja na wao..

Westbank na Jerusalem zilikuwa zinatawaliwa na Jordan na Asilimia 70 ya Raia wa Jordan wanasema ni Arabs from Palestina land ambao ni Asili yao niAl masri ambayo ni from Egypt pia... so kuna zaidi ya raia m6 had 7 walikimbia kichapo cha vita na Israel maana Waisrael waliokimbia Ulaya walipokuwa wanarejea Arabs wakaanzisha vita... so uhasama ukaanza Vita wakashinda Israel ila kusingekuwa na vita amani ingetawala hadi leo hii.

So huu upuuzi anaoufanya Iran na kushawishi direct wapalestina kupigana vita na Israel ulishafanywa sana na Arabs Country na mara zote arabs walifail... na wanaendelea tu kufail na kuloose more...

Hiyo land zamani iliitwa Caanan na Mji huru aliohamia Ibrahim Mzee wa Imani babu wa Mataifa Mengi. Mwanae Isaka aliishi akamzaa Esau na Yacob na kisha Watoto watoto wa Yacob aliyeuzwa Misri na kaka zake akawa mtu Mkubwa Katika serikali ya Pharao Misri akawachukua ndugu zake Wote wakahamia Misri wakazaana sana ukaja utawala mpya Yusuph akawa akasahaulika wakawa Watumwa hadi Mungu wao akaamua kuwaokoa kwa Kumtumia Mussa as Mesenja wake so wakatakiwa kurejea Caanan ambapo Mji ulishahamiwa na jamii nyingine za watu haswa Philistines ambao sio hawa Palestines kwa vinasaba wala maumbo wala rangi zao so Miaka ikaenda Israel ikajisimamia ikawa na Tawala nyingi ikajenga miji yake na kuipa majina ambayo hadi leo yapo, Gaza, Samaria,Jerusalem,Nazareth n.k Waroman walizingua kwa kuwanyima haki ya Uraia Wayahudi japo kabira zingine kama Samaria waliendelea kuishi hapo hapo hadi leo hii kumbuka Israel ni Watoto 12 wa Jacob ambao kila jina la Mtoto linarepresent one of the tribe of 12 tribes of Israel na kila tribe lilikuwa na kazi zao utawala walikuwa ni Jews Dini waliwa Dan koo ya Mussa, na nyingineza kama Samaria,Manashe, n.k jina hilo la Palestin land likuja baadae sana na Roman likiwa na Maana yake Ardhi ya Wafilisti. but sio Arabs hawa wa Leo ni Tofauti kabisa..

Watu wanaoisha Katika Mji huo enzi za Watawala wa Kale waliitwa Palestine but if Israel akirejea Utawala wake ardhi inarudia old name yake Caana Na Taifa ni Israel..

Arabs hawana chao pale... na Mistake zao kukataa offer zote za UN na za Israel yenyewe hadi leo hii hawataki... Na Israel ameshasema wazi Arabs watabakia na wao wanakubali na Arabs pia watambue akilini mwao kuwa Israel ipo na itaendelea kuwepo hivyo wakitaka amani na kuishi side by side bila ugomvi Israel inabariki ila wakitaka vita basi sawa wakianzisha watapigana tu mbwai mbwai tu.
 
umeongea ukweli wa mungu mtupu Taifa lolote likiichukia israel utakuta lina uchumi mbaya, haliwiki ktk mashindano ya Olyimpic, halichezi world cup na hata hapa africa utakuta ligi ya kuingia world cup inawapa ugumu. tazama mataifa yaliolinda na kujenga urafiki na wajukuu wa Rebeca yaani israel, Ulaya magharibi , kenya, Marekani na misri yalivyo nona kiuchumi na Riadha /soka. Tazama mataifa yaliochukia Israel yasivyojua kutumia pesa, Saudi Arabia, Libya, Sudan kaskazini,somalia na Mali. mungua katika mwanzo hakuongopa kuhusu laana ya mchukia Israel!
 
1948 baada ya mwingereza kuondoka palestina, kipande cha gaza kilichukuliwa na Misri na west bank kilichukuliwa na Jordan. Misri na Jordan walikali ardhi hizo kwa miaka 19 wakilima na kupanua himaya yao. Maajabu hawakuthubutu kuwapa wapalestina ardhi hizo wakijua fika hakuna mpalestina mwenye haki ya kumil;iki ardhi ile. Baada ya kushindwa vita vya six day war 1967 gaza ilitekwa na israel na vile vile west bank ikachukuliwa na wanajeshi wa israel. hapo ndipo kukazaliwa PLO na nchi zote za kiarabu wakanza kudai uhuru wa palestina na Gaza na west bank eti ya mpalestina ! sasas mbona misri na Jordan hawakuwapa ardhi ya Gaza na west bank wapalestina wakati mwingereza anaondoka palestina mwaka 1948?
 
Kwa mda mrefu kumekuwepo na mzozo kati ya wa-Palestina wa- Israel. Wa-Palestina wanadai hapo wa- Israel walipo ni kwao kwa asili.

Swali langu, je madai haya ni sahihi na halali kiasi gani?

Je, wakati wa- Israel wanawekwa hapo wao walikuwa wameenda kutalii wapi?
Wote wale ni wavamizi tu hakuna mwenye nchi
 
Arabs hao walihamia tu na waliwakuta wayahudi na Wasamalia na Makabira mengine ya Waisrael wakiishi hapo Tawala vamizi za Kiislam ndio zilijaza arabs hapo from Arabian Peninsula... and from 1948 hadi 1968 Gaza ilikuwa under Egyptian rules After war Israel akatake over Gaza and Sinai hadi pale walipoingia mkataba wa Amani na Israel. So Gazan ni Egyptian japo Egypt alikataa kuwapa passport watu wa jimbo la Gaza japo niAsili moja na wao..

Westbank na Jerusalem zilikuwa zinatawaliwa na Jordan na Asilimia 70 ya Raia wa Jordan wanasema ni Arabs from Palestina land ambao ni Asili yao niAl masri ambayo ni from Egypt pia... so kuna zaidi ya raia m6 had 7 walikimbia kichapo cha vita na Israel maana Waisrael waliokimbia Ulaya walipokuwa wanarejea Arabs wakaanzisha vita... so uhasama ukaanza Vita wakashinda Israel ila kusingekuwa na vita amani ingetawala hadi leo hii.

So huu upuuzi anaoufanya Iran na kushawishi direct wapalestina kupigana vita na Israel ulishafanywa sana na Arabs Country na mara zote arabs walifail... na wanaendelea tu kufail na kuloose more...

Hiyo land zamani iliitwa Caanan na Mji huru aliohamia Ibrahim Mzee wa Imani babu wa Mataifa Mengi. Mwanae Isaka aliishi akamzaa Esau na Yacob na kisha Watoto watoto wa Yacob aliyeuzwa Misri na kaka zake akawa mtu Mkubwa Katika serikali ya Pharao Misri akawachukua ndugu zake Wote wakahamia Misri wakazaana sana ukaja utawala mpya Yusuph akawa akasahaulika wakawa Watumwa hadi Mungu wao akaamua kuwaokoa kwa Kumtumia Mussa as Mesenja wake so wakatakiwa kurejea Caanan ambapo Mji ulishahamiwa na jamii nyingine za watu haswa Philistines ambao sio hawa Palestines kwa vinasaba wala maumbo wala rangi zao so Miaka ikaenda Israel ikajisimamia ikawa na Tawala nyingi ikajenga miji yake na kuipa majina ambayo hadi leo yapo, Gaza, Samaria,Jerusalem,Nazareth n.k Waroman walizingua kwa kuwanyima haki ya Uraia Wayahudi japo kabira zingine kama Samaria waliendelea kuishi hapo hapo hadi leo hii kumbuka Israel ni Watoto 12 wa Jacob ambao kila jina la Mtoto linarepresent one of the tribe of 12 tribes of Israel na kila tribe lilikuwa na kazi zao utawala walikuwa ni Jews Dini waliwa Dan koo ya Mussa, na nyingineza kama Samaria,Manashe, n.k jina hilo la Palestin land likuja baadae sana na Roman likiwa na Maana yake Ardhi ya Wafilisti. but sio Arabs hawa wa Leo ni Tofauti kabisa..

Watu wanaoisha Katika Mji huo enzi za Watawala wa Kale waliitwa Palestine but if Israel akirejea Utawala wake ardhi inarudia old name yake Caana Na Taifa ni Israel..

Arabs hawana chao pale... na Mistake zao kukataa offer zote za UN na za Israel yenyewe hadi leo hii hawataki... Na Israel ameshasema wazi Arabs watabakia na wao wanakubali na Arabs pia watambue akilini mwao kuwa Israel ipo na itaendelea kuwepo hivyo wakitaka amani na kuishi side by side bila ugomvi Israel inabariki ila wakitaka vita basi sawa wakianzisha watapigana tu mbwai mbwai tu.
Waarabu na wale wa israel wote ni wavamizi, maana Israel babu yao alitoka Mesopotamia na waarabu wametoka Arabuni, tofauti ni kwamba kila mmoja alijipenyeza kwa wakati wake
 
Back
Top Bottom