Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi


Ili ujibiwe swali lako, uliza hivi, hivi kabla wa Israel hawajahama katika nchi yao, wa Palestina walikuwa wakiishi wapi? Unaposema Waisrael, unaanzia kipindi gani? Maana hapa kuna mwenye nchi na mhamiaji. Ni nani mhamiaji/mvamizi kati ya Israelites na Palestinians? Angalia sana Historia ya hawa watu ndipo utajua nani ni nani.
 
Mfilisti hana chake pale. Ardhi ile yote ni ya watoto wa Yakobo, wakuu wa Baba Abraham
 
Ndio maana vita ilikuwa kali ,ni ngumu kwa wenyeji wenye akili timamu kukubali madai ya mtu alietoka mbali akidai eti nchi hii nimepewa na Mungu kwa hiyo ni yangu, wakati nyinyi ndio mmeijenga ile nchi , ni ngumu sanaaaa
Mwenda kwao si mtoro. Wewe kama unajimilikisha viwanja na mashamba ya watu kwa kuwa huwaoni oni, usije ukang'ang'ania unahaki watakaporejea. Bdo wako wengine wazawa hasa wa maeneo hayo wanarejea hivi karibuni. Wapalestina, warudi walikokuwa wakiishi kabla ya wenye nchi hawajaondoka.
La sivyo wakubaliane na mwenye nzengo. badala ya kuvamia plot za wenzao na kung'ang'ania.
 
  1. Kwani ile ardhi imeandikwa itarithiwa na Wayahudi au Wana wa Israel?
  2. Maana siyo kila myahudi ni mbegu ya Yakobo, wengine historically walibadili dini tu na kufuata uyahudi na hivyo vizazi vyao kufuata uyahudi mpaka leo
  3. Je sisi siyo watoto wa Ibrahimu?, Biblia inasema Wakiristo ni watoto wa Ibrahim
  4. Kama sisi ni watoto wa Ibrahim je agano lake halituhusu?, Je urithi wa Ibrahim siyo urithi wetu?
  5. Kama sisi ni wana wa Ibrahimu then kwa nini wale Wakiristo wa Kipalestina waishio katika hiyo nchi wasiwe na haki ya kuishi kwenye nchi ya baba yao Ibrahimu?
 
Shida ni kuwa parestina wanamjua Jakob( yakubu) , wanamjua isaka(isihaka), wanamjua ibrahimu na wanasema ni baba wa Iman na ndio maana wanachinja katika eid il Hadji kutoa sadaka ya damu Kama Ibrahim, wanamjua yesu (Isa),....shida ya mashabiki wa Israel mmempa Israel point kuwa mungu ni wake pekeake , na wengine wafe tu, ibrahimu wa peke yao, Jacob wa peke yao yaan kila kitu....hii Vita ni ya watu flan flan sio israel na parestina....af mjue kuwa Israel hakuna mkristo Wala msamalia, Ila parestina inao
 
Huu ni upuuzi Mungu siyo mbaguzi kiasi hicho na aipendelee israel hadi wew kudai eti ni taifa teule la Mungu.

Inamaana mataifa mengine hayakupewa kipaumbele na Mungu?

Tuache kutukuza waisrael kwa misingi ya imani na dini za kulishwa/kupandikizwa.

waisrael wanatofauti gani na Wangoni kwani wote ni wahamiaji na wanavipaji vyao.

Hii habari ya yesu ,yesu,yesu, ni utumwa kwa Waafrika wamewasahau hata Wazee wao kisa tu dini za kuja.
 
Israel sio kwao pale , Sema alianza uvamizi mapema kabla hao waitwao sasa wapalestina, Kwahiyo wote wale ni wavamizi wakae waelewane
 
Israel sio kwao pale , Sema alianza uvamizi mapema kabla hao waitwao sasa wapalestina, Kwahiyo wote wale ni wavamizi wakae waelewane
Unaongelea mwaka gani huo? Hao Israel walipovamia palikuwa pa nani? Kama palestina anakuja kuvamia wakati tayari kuna watu, nani mchokozi? Pengine Mh. Lukuvi angeweza kumaliza huu mgogoro.
 
Umeandika mengi sana ila ukiweza nenda kabebe mtoto mpalestina na mtoto muisraeli utuambie tofauti yao kisha ufikiri kama mtoto muisraeli ni mfano wa MUNGU ni kwann mtoto mpalestina unamuhusisha na shetani.
 
Unaongelea mwaka gani huo? Hao Israel walipovamia palikuwa pa nani? Kama palestina anakuja kuvamia wakati tayari kuna watu, nani mchokozi? Pengine Mh. Lukuvi angeweza kumaliza huu mgogoro.
Israel mbona alikuta watu wengi hapo au unafikiri alikuta mapori? alikaa hiyo nchi kimabavu kwa kuwaua wenyeji wa nchi, hivyo huyo ni mvamizi tu kama hao waitwao sasa wapalestina , haijalishi ulivamia mwaka gani, jambo la msingi ni kwamba ulivamia na kuua wenye nchi
 
Kamwulize Lukuvi, naye angetatua mgogoro huu kwa mitazamo ya vurugu kama yako? Kama kuna watu walikutwa wakaondolewa, na kwa kuwa siyo hao wapalestina, basi hao watu walikubaliana. Israel amekataa uvamizi wa wafilist. Analinda mipaka yake. Hao watoto wa Goliath, waambieni hapo wamekwama, waende wakaavmie kwingine kama irani hivi, jordan au syria kama wana ubavu.
 
Yaani watu WALIUAWA wewe unasema wamekubaliana? wale waliuawa na kudhulumiwa maeneo yao na wayahudi kwa hiyo yule pale sio kwake na wala hana hiyo haki ya kumnyooshea kidole mvamizi mwengine mnaomwita palestina, yaani kunya anye kuku ila akinya Bata kaharisha, ahahaha mavi ni mavi tuuu
 
Asiye sikia la Mkuu.......
Ndio kinacho wakumba wa Palestina
" Do not give them a land"
'If you give them an INCH they'll
take a YARD!"
"If you give them a YARD they'll take a MILE"
"If you give them a MILE they'll take the WHOLE LAND"
 
Hadithi za kusadikika.
 
Ukitaka kuishi na kubarikiwa, jiungamanishe na Israel. Ukitaka kufa kifo cha milele na kuishi maisha ya laana, jaribu kumshambulia na kulitakia mabaya taifa hilo na watu wake. Huko ni kugusa mboni ya jicho la Mungu...!!


Mbona kuna mashoga wengi huko Israeli ??!
 

Kipindi taifa hilo linaundwa nchi ya Palestine ilikuwa chini ya Utawala wa kikoloni wa Muingereza na ni hao waingereza waliopeleka mkataba (Balfour treaty) huko UNO wa kuanzishwa kwa taifa la Israeli (mwaka 1948).

Kitu Kilichotakiwa kufanywa na Uingereza kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Israeli ni; kugawa nchi ya palestina ili kupata nchi mbili, nchi ya Israeli na nchi ya Wapalestina iliyokuwa huru yaani nchi ya Wapalestina huru ilitakiwa iwe Sovereign ikiwa na mji wake mkuu, kwakuwa Waingereza hawakutaka Nchi ya Wapalestina iwepo walichofanya ni kuunda taifa/nchi ya Israeli pekee na kuwaacha Wapalestina bila nchi kamili sovereign state/autocratic ili Waisraeli waimeze Palestine yote kitendo ambacho Israeli imekuwa ikifanya tangu mwaka huo wa 1948 hadi leo kwa kuwafukuza Wapalestina kutoka katika maeneo yao ya asilia na kujenga makazi ya Walowezi wa kiisraeli.

Kifupi ni kwamba, Waingereza na Waisraeli hawataki taifa la Wapalestina liwepo hapo Palestina kwani Waisraeli wanasema Wapalestina kwao ni Syria na lazima warudi huko na Wapalestina wanadai kuwa Waisraeli walipendelewa na UNO kuja kuiba ardhi yao kwa kuanzishwa taifa.la Israeli hapo Palestine huku wao wasipewe uhuru sambamba na kuanzishwa kwa Israeli hivyo basi Wapalestina wanadai Israeli hana haki ya kuwepo hapo, kimsingi mgogoro huo ndivyo ulivyo.

Maagizo ya UNO ni "two state solution"---- yaani Suluhu ziundwe nchi mbili yaani nchi ya Israeli na nchi ya Wapalestina, Swali ni hili; KWANINI NCHI YA WAPALESTINA HAIKUANZISHWA WAKATI NCHI YA ISRAELI ILIPOANZISHWA??? AU KWANINI WAINGEREZA HAWAKUWAPA UHURU WAPALESTINA WAKATI ISRAELI ILIPOANZISHWA? ?---- kuna dhuluma.na njama zilifanywa na Mataifa makubwa ya Uingereza.na Marekani kupitia UNO ili kuwadhulumu Wapalestina ardhi na hatimaye nchi yao yote.

Ndiyo maana mgogoro huo haumaliziki toka 1948.
 


Waisraeli walitapakaa katika sehemu kubwa ya Bara arabu, Afghanistani (pashtun), Bara hindi (India, Pakistani, Bangladesh, na Kashmir), Ulaya Russia, Ukraine, Germany, France, Uk, Turkey nk, Africa; Ethiopia, SA, Egypt , Latin America; Argentina, Brazil, Canada, the US nk.

Hao waisraeli wa ulaya ndio Ashkenzai na ndio hao wanaotetea itikadi ya Zionism na ndio hao waliokuwa wakorofi sana, Waisreali wengine wako poa, kipindi Yesu "anapaa" (ukweli ni kwamba alihama yeye na mama yake pamoja na Mariam Magdalena na akaelekea Kashmiri kwenda kuwafundisha Injili Waisraeli wa huko na akafia huko, Angalia Rozabal Shrine).

Yesu alipoondoka aliacha Palestina Makabila 2 ya Wana waisraeli Yudea na Benjamin makabila mengine yalikuwa yametawanyika katika sehemu kadhaa za dunia na hadi hivi karibuni miaka ya 1940 bado Waisraeli waliendela kutawanyika duniani, hayo makabila 10 yallliyotawanyika yalikuwa utumwani chini ya mfalme Nebuchadnezzar wa Babylon ambaye alipowaacha huru hawakurudi Palestine bali wakatawanyika sehemu mbalimbali duniani.

Yale makabila mawili yaliyobaki palestina yalimezwa na Makabila ya Wasamaria, Samartans/Wafilisti, Wapalestina na utambulisho wao kwa takriban miaka 2000 ukawa umefutika kabisa ndipo mwaka 1948 UNO kwa hila wakaamua kuwapendelea Waisraeli na kuanzisha tena milki yao hapo Israel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…