Jeshi la Afrika Kusini pamoja na FARDC limefanikiwa kuwadhibiti M23 kuelekea GOMA

Alvin_255

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
246
Reaction score
503
🇨🇩#RDC: Jeshi la Afrika Kusini linatangaza kwamba limefaulu, pamoja na FARDC na washirika, kusimamisha maendeleo ya muungano wa M23/RDF kuelekea Goma:

"Vikosi vya maadui vya M23 vilikuwa vimezindua shambulio kubwa kwa askari wetu ili kumtia Goma, lakini hawakuweza kuendeleza shukrani kwa upinzani wa kishujaa wa wapiganaji wetu mashujaa."

Vikosi vyetu havikusimamisha maendeleo ya M23 tu, lakini pia viliweza kuwarudisha. nia ya M23, pamoja na mambo mengine, ilikuwa kuudhibiti mji wa Goma, lakini walipata upinzani mkali kutoka kwa kikosi cha Afrika Kusini kilichowazuia kufika Goma. "

COMMUNICATED ⤵️

 
M 23 wanamiliki mikoa mingapi huko DRC? Mbona kila siku wanaibuka na kutulizwa. Kuna mtu mmoja aliwahi kuandika humu kwamba ni vitoto vidogo na vina dhibitika hata na FFU wetu, sijui kwanini nchi hiyo yenye msaada wa kijeshi kutoka nchi kadhaa bado wanashindwa kuwamaliza M23.
 
Hao M23 wanachofanya ni kutibua hali ya hewa na kutulia/pasikalike kama huko kwingine wameteka kote, inaonekana hata hiyo Goma kama wangedhamiria nayo wangeichukua TU
vijana wamerudi chimbo zao baada ya kujidhihirisha kuwa wapo!

Kuna clip niliona M23 wanarudi kutoka vitani raia wanawashangilia kwa kazi safi 😁
 
M 23 ni jeshi kabisa linajitosheleza(japo kinaripotiwa kama kikundi cha kigaidi).Watoto nadhani ni sehemu pia katika jeshi lao(Sehemu kubwa ni watu wazima).M23 nadhani michezo yao mingi wanafanyia Goma,Kivu,Bukavu,na kinshasa kama sijakosea
 
vitoto vidogo na vina dhibitika hata na FFU
Kakudanganya vibaya sana ngoja nikufumbue macho m23 ni jeshi kamili lenye wataalamu wote wa kivita , wana intelijensia kali sana, wana vifaa vya kisasa mno, wana askari wenye mafunzo bora kabisa, wana mifumo ya kisasa ya uongozaji vita( drones) ,

Wana wataalam mbali mbali wa medani mpaka snipers, commando, na elites wengine usiwachukulie poa hata kidogo na
Sio kwamba ni vitoto ni mashabab haswa tu na wana nidhamu ya kijeshi sio waasi koko wale
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…