Jeshi la Afrika Kusini pamoja na FARDC limefanikiwa kuwadhibiti M23 kuelekea GOMA

Vita ni biashara na uchumi kwa mataifa mengine. Lakini hao M23 kwanini hawadhibitiki, au huo ndio uwanja wa majaribio ya silaha zao?
DRC itakuwa kama Israel na palestina, Sioni ni namna gani watapata suluhu ya kudumu.
Ukijua kwanini M23 wanapigana solution itakuwa rahisi sana, kwa ufupi ni ukabila wa wacongo na kukataa kuwatambua M23 kama raia na kutaka kuwamaliza wote, hata mimi nisingekubali na zingepigwa mpaka mshindi apatikane
 
🇨🇩#RDC: Jeshi la Afrika Kusini linatangaza kwamba limefaulu, pamoja na FARDC na washirika, kusimamisha maendeleo ya muungano wa M23/RDF kuelekea Goma:

"Vikosi vya maadui vya M23 vilikuwa vimezindua shambulio kubwa kwa askari wetu ili kumtia Goma, lakini hawakuweza kuendeleza shukrani kwa upinzani wa kishujaa wa wapiganaji wetu mashujaa."

Vikosi vyetu havikusimamisha maendeleo ya M23 tu, lakini pia viliweza kuwarudisha. nia ya M23, pamoja na mambo mengine, ilikuwa kuudhibiti mji wa Goma, lakini walipata upinzani mkali kutoka kwa kikosi cha Afrika Kusini kilichowazuia kufika Goma. "

COMMUNICATED ⤵️

View attachment 3214162
Goma ishachukuliwa kitambo na M23, ww unaandika porojo tu hapa
 
Mbona JWTZ wasitoe media statement kama hii?

Miakq mitano ijayo jamaa wa SANDF watajibebea maujiko kwamba bila wao..kingenuka
 
Ukijua kwanini M23 wanapigana solution itakuwa rahisi sana, kwa ufupi ni ukabila wa wacongo na kukataa kuwatambua M23 kama raia na kutaka kuwamaliza wote, hata mimi nisingekubali na zingepigwa mpaka mshindi apatikane
Madai ya M23 yote unayajua?
 
Tutsi community wana haki ya kujilinda
Madai yao ni ya kipuuzi tu!

Kiasili wao si wakazi waasili Congo, ni wakimbizi ambao waliyokimbia mapigano nchini mwao.

Congo ina makabila mengi tu! Kwa nini Tutsi wao pekee ndiyo walazimishe wawepo kwenye serikali?

Yaani mkimbizi aliyekimbia vita huko Rwanda sijui Burundi aje Tanzania halafu baadaye adai utambulisho wake kama raia halali wa Tanzania na awepo kwenye nyadhifa za juu za serikali serikalini?

Huo ni upuuzi!
Kwa kuwa serikali ya Congo ni dhaifu. Hawa dawa yao wagongwe na watolewe kwenye hiyo nchi warudishwe nchini kwao Rwanda.
 
Uko sahihi kabisa ila POw's ya Bamutu unailewa lakini?🤣🤣🤣🤣

Ukisikia mauza uza basi ndo hayo hakuna cha Pows hapo jiongeze kidogo tu utaelewa
Nasikia fardc wanatembeza kichapo huko goma,wameenda na kichwa cha chigoro ntawirigado, general wa rpf huko m23
 
Mbona JWTZ wasitoe media statement kama hii?

Miakq mitano ijayo jamaa wa SANDF watajibebea maujiko kwamba bila wao..kingenuka
JWTZ wapo sake, nyuma ya goma kuelekea kinshasa,kila mtu na chimbo lake na jukumu lake,japo nasikia wana kambi pia goma
 
Nasikia fardc wanatembeza kichapo huko goma,wameenda na kichwa cha chigoro ntawirigado, general wa rpf huko m23
Sio zile special unit za kutoka Kinshasaa na Lubumbashi kweli? Mana wale kweli wazee wa kazi kuliko hawa
1000347091.jpg

🤣🤣
 
Wanataka kutambuliwa kama raia wa Congo, haki na usalama wao, hizo za kusema wanataka kujitenga ni uhuni tuu ili kuwamaliza
Kuna jengine umesahau!

Wanataka wawepo jeshini tena kwenye nyadhifa za juu!

Na wanataka wawepo kwenye serikali nyadhifa za juu!

Congo kuna makabila mengi, kwa nini kabila hili moja ndilo linataka lipewe umuhimu wa namna hiyo?
 
Mkuu kwani ktk hayo makabila inayosema yapo mengi congo hayapo kwenye serikali? Je hayapo jeshini?
Sasa kama watusi wakitambuliwa kuwa ni moja ya kabila ndani ya congo kwanini unadhani hawana haki ya kuwa jeshini wala serikalini?
Hii shida inaanzia hapa ' Ubaguzi'
 
Umeelewa nilichokiandika?

Suala si kuwepo jeshini, suala ni kuwa kwenye nafasi za juu jeshini.

Halikadhalika wanataka vivyo hivyo mpaka kwenye madaraka ya kiserikali.

Na ili kuweka rekodi sawa kila wanapopigwa M23 hukimbilia Rwanda au Uganda ila mara nyingi ni Rwanda.

Swali la muhimu: Ikiwa wamo madarakani utiifu wao utakuwa kwa nani?

Na pasipo kujificha PK inafahamika kuwa inawasaidia na mfano mzuri Kikwete aliliweka wazi hili! Kikwete Ni rais mstaafu na bila shaka ana taarifa sahihi zaidi kuliko mimi na wewe.

Ikiwa hii ndiyo hali; mamlaka wanayoyahitaji wakipatiwa utiifu wao utakuwa kwa nani? Utakuwa kwa dola ya Congo au kwa yule bwana (PK) waliyekuwa wakimtumikia?
 
Unaonekana huelewi, uko biased sana na analysis yako..go educate yourself
 
Back
Top Bottom