Jeshi la Guinea-Bissau lachukua madaraka baada ya Uchaguzi wenye utata

Jeshi la Guinea-Bissau lachukua madaraka baada ya Uchaguzi wenye utata


View: https://www.youtube.com/live/wxK-HnLPxTA?si=9Wstp_UkmnL2fThE
Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló amepinduliwa.

Rais Umaro ameripotiwa kukamatwa na maafisa wa kijeshi baada ya milio ya risasi kusikika katika mji mkuu, Bissau kwa siku 3 mfululizo.

Shirika la habari la BBC limeripoti kwamba Rais huyo ametiwa mbaroni na maafisa wa kijeshi na kwa sasa yupo chini ya ulinzi.

Brigedia Jenerali Denis N’Canha, mkuu wa Brigedi ya kijeshi mjini Bisau amehutubia kupitia televisheni ya taifa na kutangaza kuwa jeshi limechukua madaraka.

Jenerali N’Canha amesema askari wote wa kikosi cha ulinzi cha Rais wamekamatwa pamoja na mawaziri kadhaa.

Kabla ya Jeshi kutangaza mapinduzi hayo, Rais Sissoco alipiga simu kwenye kituo cha televisheni cha France 24 kilichopo Ufaransa kwa sauti ya kutetemeka na kusema: “Nimewekwa chini ya ulinzi, nimeondolewa madarakani” kabla ya simu hiyo kukatwa ghafla.

Guinea-Bissau ilikuwa ikisubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili, ambapo mgombea mkuu wa upinzani Fernando Dias alienguliwa katika orodha ya wagombea ili kumfanya Rais Umaro ashinde kirahisi.

Jenerali N’Canha ametangaza kufutilia mbali matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyoonyesha kumpa ushindi Rais Umaro kwa zaidi ya 90% na amesema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu mkubwa. Jenerali N’Canha ametangaza kufunga mipaka ya nchi, huku akiwataka wananchi wabaki watulivu. Pia ameeleza kuwa Jeshi litaongoza nchi hiyo kwa muda mfupi ili kurejesha hali ya utulivu kabla ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Rais Umaro alikuwa Rais wa kwanza Afrika kumpongeza Rais Samia baada ya matokeo ya uchaguzi wa Tanzania kutangazwa. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter (X) Rais Umaro alipost picha akiwa na Rais Samia na kuandika maneno yafuatayo: “Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Samia Suluhu kwa kuchaguliwa tena. Ushindi huu ni ushahidi wa imani ambayo wananchi wa Tanzania wamempa na ni kielelezo cha dhamira yake thabiti ya kuendeleza na kustawisha Tanzania.”

Nini maoni yako??
 
Haizimi hoja za vifo vya raia wasio na hatia. Haizimi hoja za EU
Haizimi hoja ya ICC mpaka kigagila asahau kupaka hina mwaka huu
kwan tunazima hoja ama tunaongelea ukwel
 
Ni hatari sana Watawala wowote wanapochezea mchakato huru wa uchaguzi ikiwemo kuwakata wapinzani wao kisiasa na kuwatia ndani kwa makosa ya uongo, ili wao wapate ubwerere wa kupijitisha washindi pasipo kushindanishwa

Mbinu alizotumia Omaru Sissoko ili ajitangaze mshindi wa kiti cha Urais ni kama alizotumia Samia na genge lake la wahuni yaani kuengua wapinzani wake

Sasa mwenzake wamefyatua na kumng'oa kutoka kwenye kiti cha ufalme wa nchi

Hawakumsubiri hata ajitangaze, wakamwambia NO WAY


Hapa kwetu, Samia na wahuni wenzake ameponea chupuchupu tarehe 29/10. Lakini tayari yupo na ameshajaa kwenye radar. Hatoboi 2026, ataitema mbunga lazima☹☹☹☹!!
 
Haizimi hoja za vifo vya raia wasio na hatia. Haizimi hoja za EU
Haizimi hoja ya ICC mpaka kigagila asahau kupaka hina mwaka huu
Uchome moto mali na miundombinu ukose hatia!?
 
27 November 2025
Bissau, Guinea Bissau

JESHI LACHUKUA NCHI, RAIS UMARO SISSOCO EMBALÓ AWEKWA KIZUIZINI


View: https://m.youtube.com/watch?v=Sv9d1Lv6RTI

Taifa la Guinea Bissau koloni la zamani la Portugal, lililopata uhuru wake kutoka ukoloni mkongwe wa Mreno mwaka 1974

Rais Umaro Sissoco Embaló , pia waziri wa usalama na viongozi wakuu wa jeshi yaani mkuu wa majeshi na mnadhimu kuu wa jeshi wote wamewekwa kizuizini...

Maofisa wa kijeshi waliotekeleza Mapinduzi hayo operesheni yao ilikwenda haraka huku wakichukua maeneo yote nyeti nchini humo
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=KZ6dIVolshU

22 Juni 2024 — Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro .

1764205289014.jpeg

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru kutoka ukoloni mkongwe wa Wareno .

 
Dakka chache kabla ya kutangazwa kwa mapinduzi ya kijeshi, Rais anayemaliza muda wake, Umaro Sissoco Embaló, aliripoti kukamatwa kwake akiwa Ikulu ya Guinea-Bissau.
Duuh Similarity and congluence
Jeshi la Guinea-Bissau limechukua uongozi wa nchi kutoka kwa uongozi wa kiraia baaada ya chama tawala kuharibu taratibu za uchaguzi na kumzuiaa mgombea wa chama kikuu cha upinzani asishiriki uchaguzi.
 
Huko wanajeshi wanaenda shule sio hizi takataka ambazo hazijielewi wengi ambao ni standard 7 na form four failures
 
Back
Top Bottom