PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Ni zamu ya Israel kwenda kuweka Kambi zake mpakani na Iran.Kwa sasa Israel ana mkono juu maana hana upinzani wa radar pale Syria, atapita atakavyo hadi karibu na mpaka wa Iran
Kitendo cha Israel kuendelea kuangamiza sila za kijeshi za syria ambazo karibu 60% amezinunua kutoka Russia huku 30% akizinunua kutoka Iran na China.
Ni makubaliano ya awali kati ya waasi na US, UK na Israel. Baada ya Israel kumaliza safishasafisha yake, Israel na US watakamata tender ya kufunga mitambo ya Ulinzi nchini Syria na kuwauzia silaha.
Upande mwingine UK akichukua kazi ya kulisuka upya kabisa Jeshi la Syria na baadhi ya mafunzo wakipewa na Israel.
Syria inabadilshwa kabisa huku ikakabidhi baadhi ya maene ya kihistoria ya wayahudi kwa Israel.
Urusi anakua ameshapoteza mteja muhimu sana wa silaha zake, pia hatakuwa na tender ya ukarabati wala kuendesha hizo silaha. Ndivyo Urusi alivyon'olewa pale middle east.
Bomba la gas kutoa Qatar, kupitia syria kwenda Ulaya litajengwa na hapo gas ya Russia inakwenda kupoteza soko la Ulaya.