Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lasitisha mafunzo ya kujitolea

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lasitisha mafunzo ya kujitolea

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
JKT YASITISHA MAFUNZO

DODOMA
: JANUARI 19, 2021

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza kusitisha kwa muda mafunzo ya jeshi hilo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 mpaka hapo itakapotangaza tena.

Kutokana na kusitishwa kwa Mafunzo hayo JKT imewataka vijana walioripoti makambini kurejea majumbani na wale ambao hawajaripoti wasiende kuripoti.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena, wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.

Nami All - Rounder nasema kuwa huenda kwa Kurejeshwa Kwao hawa na Ajira kuwa ngumu Vitendo vya Kiuhalifu vikaanza Kuongezeka nchini.

Taarifa: Uhurudigital

---
Siyo mbaya kusema safari hii Pesa hakuna ( Kibajeti kuliko Kuficha, lakini pia hata haya Mafunzo yanahitaji Mabadiliko makubwa sana ya Kimfumo.

Jan 19 2021
Jeshi la kujenga taifa (JKT) limetoa tamko ya kusitishwa kwa mafunzo kwa muda usiojulikana mpaka watapotoa taarfa kwa vijana wanaojitolea. Hivyo vijana walioripoti katika makambi mbalimbali wanatakiwa kurudi na ambao walikua hawajaripoti wameelekezwa kubakia majumbani mwao. Yamesemwa na kaimu utawala Kanali Hassan Mabena.

Uhuru%20Media%20Group%20on%20Instagram_%20_JKT%20YASITISHA%20MAF(JPG).jpeg
 
Tujiandaeni tu Kukabwa sasa Mitaani tena kuliko hata tunavyokabwa Kistaarabu kwa sasa. Na walivyo wengi Mitaani safari hii tutawakoma sana!!!
Acha kupotosha Mkuuu.

Utakabwa na Nani wakati hawa watoto hata Mafunzo hawajaanza kupatiwa kumbuka waliripoti Makambini tarehe 8/01/2021 na kwa sasa wana takribani siku 10 huko Kambini na hata wengine walikuwa bado hawajaripoti kama taarifa inavyosema kwamba ambao hawajaripoti Wasiende kuripoti.

Lkn kwa masikitiko makubwaa, Expert member wa JF anaaanza kuzusha taharuki kwamba tujiandae kukabwa! Tuache kukurupuka na kuwapa Raia taharuki ambazo hazipo maaana kwanza hao Vijana bado hawana mafunzo yoyote ya Kijeshi, pili tumeishi nao mtaani kwa wema kwa Vipindi vyote hadi majuzi baada ya sherehe za Mwaka mpya walipoondoka.

Kwa dhana yako na mawazo yako unaweza kusababisha Vijana hao kutoaminika Mtaani au hata kushambuliwa kwa vitu very minor. Change ur mind broo tunakuheshimu hapa JF.
 
Wakuu naona hamjaelewa habari
Kuna kundi la vijana lilitakiwa kuripoti katika makambi mpaka tar 15 January kama OP mpya kupata mafunzo ya kiseshi hilo bogi ndo limepigwa azwea warejee makwao na walokua hawajaripoti wasiendee
Wale askari waliofuzu mafunzo hayo yani OP Makao makuu bado wataendelea kuhudumu katika taifa katika makambi yao husika
 
Acha kupotosha Mkuuu.
Utakabwa na Nani wakati hawa watoto hata Mafunzo hawajaanza kupatiwa kumbuka waliripoti Makambini tarehe 8/01/2021 na kwa sasa wana takribani siku 10 huko Kambini na hata wengine walikuwa bado hawajaripoti kama taarifa inavyosema kwamba ambao hawajaripoti Wasiende kuripoti.
Lkn kwa masikitiko makubwaa, Expert member wa JF anaaanza kuzusha taharuki kwamba tujiandae kukabwa! Tuache kukurupuka na kuwapa Raia taharuki ambazo hazipo maaana kwanza hao Vijana bado hawana mafunzo yoyote ya Kijeshi, pili tumeishi nao mtaani kwa wema kwa Vipindi vyote hadi majuzi baada ya sherehe za Mwaka mpya walipoondoka.
Kwa dhana yako na mawazo yako unaweza kusababisha Vijana hao kutoaminika Mtaani au hata kushambuliwa kwa vitu very minor. Change ur mind broo tunakuheshimu hapa JF.
Pesa zinajengwa miradi ya Chato
 
Back
Top Bottom