Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lasitisha mafunzo ya kujitolea

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lasitisha mafunzo ya kujitolea

JKT YASITISHA MAFUNZO

DODOMA
: JANUARI 19, 2021

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza kusitisha kwa muda mafunzo ya jeshi hilo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 mpaka hapo itakapotangaza tena.

Kutokana na kusitishwa kwa Mafunzo hayo JKT imewataka vijana walioripoti makambini kurejea majumbani na wale ambao hawajaripoti wasiende kuripoti.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena, wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.

Nami All - Rounder nasema kuwa huenda kwa Kurejeshwa Kwao hawa na Ajira kuwa ngumu Vitendo vya Kiuhalifu vikaanza Kuongezeka nchini.

Taarifa: Uhurudigital

---
Siyo mbaya kusema safari hii Pesa hakuna ( Kibajeti kuliko Kuficha, lakini pia hata haya Mafunzo yanahitaji Mabadiliko makubwa sana ya Kimfumo.
Tumeficha korona sasa tunaficha na ukata wa fedha, kweli tunaongozwa na vilaza!
 
Natumai wapo kufanya tafiti na watakuja na majibu ya kuwa walelopitia hayo mafunzo je nifaida gani wameiachia Tanzania na Watanzania kwa ujumla ikiwa hiyo programu kama imeingiza faida itaendelea na kama itia hasara ndo bye bye.
 
Nashangaa sana kwanini Mtu anatoka jeshini halafu anakuja kuwa jambazi au kibaka wakati jeshini tunafundishwa nidhamu na uzalendo
Anza kumshangaa yule afande aliyekutwa na viroba na vitu vyenye ncha kali.
 
Mafunzo ya JKT yamesitishwa na wanafunzi wameambiwa warudi nyumbani, na wale ambao walikuwa hawajaripoti wameambiwa wasiripoti hadi hapo itakapotangazwa tena.

Je, ni sababu za kiuchumi, COVID-19 au?
 
Nidhamu na Uzalendo feki haulipi BILL.
Unataka nani akulipie bill mkuu.

Jeshini watu wanafundishwa pia ujasiriamali ukitoka hapo unaweza kuwa mkulima na mfugaji mzuri tu ila vijana wanataka waoneshane nani mbabe mjini hapa.
 
Uzalendo ni ukipata kilichokupeleka jeshini, sio upewe mafunzo kisha utelekezwe.
Jeshini watu wanafundishwa ujasiriamali pia mkuu ukitoka hapo unaweza mkulima na mfugaji mzuri tu

Kwanini mtu atumie mafunzo aliyopata ya kutumia silaha tu ila asitumie mafunzo aliyoyapata ya ujasiriamali
 
Back
Top Bottom