Mbombo ngafu.....jidanganye kwamba maandamano yamekubaliwa!!!!
======
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limekutana na Viongozi wa CHADEMA na kuwahoji kuhusu maandamano waliyopanga kuyafanya January 24,2024 na wamekubaliana kuwa watawapa majibu kimaandishi kesho January 23,2024 kama maandamano yawepo au yasiwepo na kusisitiza kuwa hadi kufikia sasa Polisi hawajakubali wala kukataa uwepo wa maandamano hayo.
Akiongea na TBC, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Baada ya kuwaona Katibu Mkuu wa CHADEMA akitangaza kwa kutumia Vyombo mbalimbali kwamba tarehe 24 lazima atafanya maandamano suala hili tumelifuatilia kwa ukaribu na leo January 22,2024 tulimuita Katibu Mkuu wa Chama hicho lakini akatuma ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu akiwa na wenzake na tumefanya nao mahojiano mbalimbali kwa kina kulingana na suala walilotangaza”
“Mimi nikiwa na Maofisa wa Kamisheni mbalimbali baada ya kuwasikiliza kwa kina na sisi kufuatilia kwa kina dhamira yao na kwasababu walituletea taarifa yao kimaandishi sisi hatujakubali au kukataa maandamano yao, majibu yao tumekubaliana kwamba tutawaapa kimaandishi kesho January 23,2024”
“Hatujaawambia maandamano yapo au hayapo kwasababu walituandikia barua kwenye Himaya zao na sisi majibu watayapata kwenye Himaya walizoandika barua hizo ambapo utakuwa ndio mwongozo wa nini kinafanyika huku tukizingatia masuala ya kiusalama na Maslahi ya Taifa kwa ujumla, tumezingatia suala la amani na majibu yao watayapata kesho”
Pia Soma;
Mbowe: Makubaliano na Jeshi la Polisi yamefikiwa kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa
Pia Soma;
CHADEMA yatangaza Maandamano Kupinga Miswada ya Sheria za Uchaguzi iliyowasilishwa Bungeni