Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Hatujakubali au kukataa maandamano, tutawapa majibu tarehe 23

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sheria ziko wazi kuhusu taratibu za kufuata kufanya maandamano, lakini kwa kwakuwa jeshi la polisi letu ni unprofessional, linasubiri maelekezo kutoka kwa wanasiasa walioingia madarakani kwa wizi wa kura. Hakuna kipindi nchi imekosa uongozi na muelekeo kama awamu ya sita
 
DJ ni DJ tu, sasa alikuwa anawahi wapi huyu jamaa,kawajaza ujinga wafuasi wake,maandamano hayapo,labda yafanyike kitandani
Yaani, anataka kuwaingiza chaka vijana wakavunjwe miguu badala ya kufanya shughuli zao za kiuchumi
 
Mbowe kaona hana jipya kaamua kutunga uongo eti polisi wemekubali bila hata kuwaonesha nyumbu kibali. Sasa watalalamika kwamba wamenyang'anywa kibali. Kumbe hakukuwa hata na mtu wa kuandamana.
FYI maandamano hayahitaji kibali.
 
ila maandamano yakikataliwa wakati ya Bawacha yalikubaliwa watakuwa wanalenga kumwangusha mama kidiplomasia na kisiasa. wacha waandamane imjenge mama kidemokrasia na 4R zake. CDM hata wakiandamana hawafanya lolote
 
Huu ndio ukweli wenyewe , Nimemhurumia sana Mulilo , yaani hana uwezo wa kuamua chochote !
Hivi chadema akili yenu huwaga iko sehemu gani ya mwili? Eti mtaandamana hadi ofisi za umoja wa mataifa (UN) ili umoja huo wa mataifa uiondoe hiyo miswada ya sheria za uchaguzi na za tume ya uchaguzi tunazotarajiwa kupelekwa bungeni?

Hivi hamjui taratibu za kufikisha suala lo lote kwa Umoja wa Mataifa na ni mtu gani au kikundi gani kinaruhusiwa kufikisha suala hilo ili likajadiliwe na umoja wa mataifa na kupigigiwa kura ya kuwa azimio la umoja wa mataifa?

Kama hamjui si mungalimuliza hata hata Zelenski au yule kiongozi wa Palestine namna walivyofikisha masuala yao Umojawa Mataifa? Kwani walifanya maandamano kuyafikikisha masuala yao huo UN?

Hivi mbajua kweli maana ya demokrasia? Kwa kifupi demokrasia maana yake ni wengi wape hata kama hukubaliani nao. Walio wachache kamwe hawawezi kushinikiza mambo yao yakubaliwe na walio wengi kwa kuandamana au kwa namna nyingine yo yote ile la sivyo mtaumia na baadhi kubaki kilema au hata kupoteza uhai kabisa.

Ushauri kwenu ni kwamba kazaneni kupata kuungwa na wengi kwa chaguzizi zijazo ili mkamate dola. Mkishakamata dola hayo mambo ya katiba mpya mnayoitaka, ya serikali tatu, serikali ya majimbo, tume huru ya uchaguzi mnayoitaka na kadhalika, mtayapata bila shida yo yote.
 
Mbowe kaona hana jipya kaamua kutunga uongo eti polisi wemekubali bila hata kuwaonesha nyumbu kibali. Sasa watalalamika kwamba wamenyang'anywa kibali. Kumbe hakukuwa hata na mtu wa kuandamana.
😂😂
 
Huu ndio ukweli wenyewe , Nimemhurumia sana Mulilo , yaani hana uwezo wa kuamua chochote !
Mbona mapendekezo ya Kamati ya Haki Jinai iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe Othman ilishauri Jeshi la Polisi liundwe upya! Ila utekelezaji wake naona . ni mgumu kwa sababu: ya kusemwa na ya kutendwa ni mambo mawili tofauti. Kwa hiyo usishangae juu ya uwezo wa polisi wa leo kutenda mema yanayostahili kwa mujibu wa wajibu wao. Ila baadhi ya polisi wanapoamua kufanya yasiyostahili, ubunifu wao hauna kifani! Kuna siku Mwenyezi Mungu atatupa kiongozi mtekelezaji atakayewezesha utawala bora hapa nchini. Inshallah!
 
Mbowe anataka kuwatoa chambo nyumbu wake itakuwa kama ya lipumba kilichomkuta maana hii nchi sio ya vyama vingi vya siasa ni ccm 4rever
 
Zigzaga Crew 🐒
 
Ccm huwa ni waoga mno, CHADEMA yenyewe mmeivunja vunji miguu lakini mnaigopa balaa
kama CHADEMA hawana woga si waendelee na masndamano January 24 kuliko hii kwenda kushoto kulia yaani hamjielewi kabisa....
Useless kabisa 🐒
 
Katibu mkuu ameogopa nn kwenda kituo cha polisi.?
 
..kamanda polisi atakuwa amepigiwa simu na kutishiwa kuyazuia.

..kungekuwa hakuna makubaliano Chadema wangeanza kupiga makelele bila kuchelewa.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa Chalamila atakuwa amempigia simu baada ya majadiliano na vyombo vya usalama.
 
Kwa akili zetu ndogo hao polisi ndio wanaokuaga chanzo cha vurugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…