Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
Kama wana umoja wao hao wafanyabiashara wa kkoo wasijichangishe?

Kwani serikali si kila bajeti huwa wanatenga fungu kwa ajili ya mfuko wa maafa sasa wanachangisha nini tena hela zilizotengwa ziko wapi mpk waanze kuwaonea wivu wengine wanaochangisha?

Mambo mengine ni aibu sana hasa yanapotendwa na kiongozi mkubwa hivyo
Bila shaka kuna mambo ya msingi hujaelewa, ni Sheria ndio inayozuia watu kuchangisha pesa bila kuwa na kibali. Hivyo kosa lake ni kuchangisha pesa bila kibali kwa mujibu wa Sheria, hii imewekwa ili kulinda wachangiaji kutapeliwa. Halipo suala la serikali kuwaonea wivu
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kuchangisha fedha kufuatia tukio la ajali ya kupomoka kwa grorofa la Kariakoo.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuzungumza katika eneo hilo akasema JENIFER JOVIN maarufu Niffer atafutwe ili aeleze nani ambaye alimpa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia tukio hilo kwa sababu Serikali ina utaribu wake katika mafaa kama haya.

Pia, Soma: Maafa Kariakoo: Usichangishe fedha tumia akaunti ya Serikali

Aidha baada ya agizo hilo majibu yakatolewa eneo la Kariakoo wakati Waziri Mkuu anazungumza kwamba Mfanyabiashara Niffer ameshapatikana.
Hivi kuchangisha fesha watu mpaka mamlaka ikupe ruhusa?
 
Una IQ ndogo sana. Alichofanya ni utapeli na utakatishaji pesa.
Acha umbumbumbu wako huyo binti hana makosa hayo fedha aliyochangisha unakuta anayo na hajaitumia ukute alikuwa anafanya utaratibu wa kuwafikishia wahusika. Utasemaje amefanya utapeli?
Kuhusu utakatishaji fedha , nahisi hujuhi hata maana na dhima ya neno utakatishaji fedha.
 
Ujue serikali hii, unaona kabisa kuna watu ni zero brain, mtu akitumia umaarufu wake kuraise michango kuna shida gani, mie huyo niffer simjui, lakini mfano kama mwakinyo, akiraise michango kuna watu watapata msukumo sababu ya mwakinyo, kuna fans wa Diamond, simba sc ama yanga sc wakianzisha kuna watu watavutika kuchanga sababu ya simba ama yanga.

Huenda kukawa kuna kaupigaji kweli, mie sikatai mjini kila mtu anaweza tumia matatizo kama fursa, lakini jinsi walivyochukua hatua sio vizuri, kesho kutwa litatokea janga, mtu maarufu akaogopa kulivalia njuga.
Kati ya huyo binti niffer na serikali nani wa kwanza kuweka utaratibu wa kuchangia.
Kama ni huyo binti serikali ilikuwa wapi kutoa muongozo?
Serikali ilishaweka muongozo. Huyu akaingia katikati. Halafu hili suala la utakatishaji fedha waliangalie vizuri. Zaidi ya hii michango ya maafa kuna kila dalili kuwa huyu binti anatumika na watu fulani kufanya hiyo kazi ya kutakatisha hela. Watumie hii chance kumbana. Huyu kuna zaidi ya hizo biashara..
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Ni money laundering kwa sababu pesa za madawa ya kulevya zinaweza kupitishiwa humo na zikatoka humo zikiwa pesa safi na halali..

Ukichukulia hivyo money laundering basi yeye hausiki manake yeye anachangisha.
Na money laundeing haipo hivyo inatumika mtu anapojifahidisha .
Sasa mtu anakusanya fedha kwa ajili ya kuwapelekea wahanga utasemaje amejinifahisha amefanya money laundring .
Kama ni hivyo basi makanisa na misikiti viongizi wao nao wakamatwe kwani wanapokea fedha /sadaka hata za wauza unga .
Money laundring doesnot apply in this issue
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kuchangisha fedha kufuatia tukio la ajali ya kupomoka kwa grorofa la Kariakoo.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuzungumza katika eneo hilo akasema JENIFER JOVIN maarufu Niffer atafutwe ili aeleze nani ambaye alimpa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia tukio hilo kwa sababu Serikali ina utaribu wake katika mafaa kama haya.

Pia, Soma: Maafa Kariakoo: Usichangishe fedha tumia akaunti ya Serikali

Aidha baada ya agizo hilo majibu yakatolewa eneo la Kariakoo wakati Waziri Mkuu anazungumza kwamba Mfanyabiashara Niffer ameshapatikana.
Duh!!
 
Viherehere kwenye mitandao sio kitu kizuri.

Hata hivyo hatua zimechelewa kuchukuliwa. Sijui jeshi letu ni wazee sana wamejazana huko hadi wanashindwa ku ‘catch up’ na mambo ya kwenye mitandao upesi?

Mtu ameshakusanya mamilioni ya pesa tokea jana na alitangaza kila hatua wao walikuwa wapi?
Duh nilikua najua ni wewe eti😅
 
Niffer Yuko mbele ya serikali kwa sababu serikali ilitakiwa kuanzisha utaratibu huo,ili wahanga wasaidiwe.
Ninampongeza kwa ubunifu huo na WA haraka
 
Niffer Yuko mbele ya serikali kwa sababu serikali ilitakiwa kuanzisha utaratibu huo,ili wahanga wasaidiwe.
Ninampongeza kwa ubunifu huo na WA haraka
Avatar yako ndio ubongo wako ulipo...
🚮🚮🚮💩💩💩
 
Uwe na akili ya kutofautisha vitu.
Hakuna utofauti yeto ni michango, mbona hamna vibali vinavyoombwa na wanaochangisha hawakamatwi.
Yule dogo aliyechoma bendera ya rais ambaye ameamua kusafiri wakati nchi ina majanga mbona tulimchangia na hatukusikia waliochangisha wamekamatwa .
Wagonjwa mbalimbali godlisten malisa anawapost tunawachangia mbona hatusikii ishu ya kibali.
Huyu Waziri Mkuu atakuwa hayupo sawa
 
Ok wakuu, tuwe serious, tuache mihemko na ushamba

Tukihararisha namna hii ya ufanyaji kazi matapeli wengi watatumia njia hii kujipatia pesa kwa majanga yetu.

Tuseme hapo mtaani kumetokea janga ghafla boda boda mmoja maarufu hapo mtaani anaanza kuchangisha pesa kwa ajili ya waliokubwa na tabu hio.

Kama wewe ni timamu lazima uone process anayofanya haipo katika mpangilip ulio na utaratibu na uratibu.

Hata kama ni kwa nia njema anafanya , una uhakika ataleta kweli hizo milioni 10 alizochangisha au kuna mbili atapitanazo.
Kabisa mkuu. Imagine kila celebrity anachangisha kivyake.
 
Wahanga hawana sababu ya kuchangiwa. Mosi ni wafanyabiashara wangetakiwa kuwa na bima kwa ajili ya wafanyakazi na Mali. Pili mwenye jengo anatakiwa kuwa na bima kwa ajili ya tenant's and should give compensation for his wrongdoing. City Father's should have been following what is happening ie building permits if the construction is being done according to specification. Hao Contractors je wako registered na CRB wanafanya inspection.
 
Taifa tumefika hapa kweli! Tunawafundisha nini watoto wetu kwakweli?

Nifah ni nani kwenye taifa hili, amefanya nini ambacho kinatutambulisha kama taifa kiasi cha kawafanya vijana watamani kufika alipofika huyo mtu, kaandika kitabu gani ambacho vizazi vijavyo vitajifunza kupitia nacho!

CCM laana hii mtaibeba nyie na vizazi vyenu! Nilikuwa sijuhi kwanini kuanzia huku ngazi za chini Hadi taifa watu wenye weredi, wabunifu, wenye maono huwa hawapewi nafasi na huwa hawapedwi!
Hata Mimi nahisi hadi waziri mkuu kama anamuonea gere binti mdogo tu.. kweli Niffer ana ushawishi wa ajabu sana
 
Hakuna utofauti yeto ni michango, mbona hamna vibali vinavyoombwa na wanaochangisha hawakamatwi.
Yule dogo aliyechoma bendera ya rais ambaye ameamua kusafiri wakati nchi ina majanga mbona tulimchangia na hatukusikia waliochangisha wamekamatwa .
Wagonjwa mbalimbali godlisten malisa anawapost tunawachangia mbona hatusikii ishu ya kibali.
Huyu Waziri Mkuu atakuwa hayupo sawa
Kasome kifungu cha 34 cha sheria ya maafa
 
Back
Top Bottom