GE2025 Jeshi la Polisi yakanusha video ya Wamasaai Kuandamana kudai haki zao Arusha

GE2025 Jeshi la Polisi yakanusha video ya Wamasaai Kuandamana kudai haki zao Arusha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi juu ya picha mjongeo (video clip) inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikisema "Wamasai waanza maandamano kudai haki zao Arusha".

Ukweli ni kwamba picha hiyo mjongeo ilikuwa ni wakati wa sherehe za jando/tohara mwezi Juni 2025, zilizofanyika katika eneo la msitu wa Tanapa Arusha.

Jeshi la Polisi lina toa wito kwa wananchi kupuuza taarifa hiyo yenye upotoshaji inayosambazwa na watu wenye nia chochezi ya kujaribu kuleta taharuki. Kama Jeshi la Polisi lilivyo wapa taarifa jana Oktoba 28,2025 kwamba kuna vijana na watu walioandaliwaa ili kuchukua picha mjongeo za matukio ya nyuma na kubadilisha maudhui yake na kuweka maudhui tofauti ya uongo kama walivyofanya katika picha mjongeo hiyo ya tukio la jando la huko Arusha mkitumiwa picha kama hizo zifuteni.

Jeshi la Polisi kama lilivyowahakikishia usalama upo wa kutosha hivyo, jitokezeni kupiga kura kutimiza haki yenu ya kikatiba ya kuchagua viongozi mnaowataka kwani hali ya usalama ni shwari na hakuna jaribio lolote la uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025 Kura Yako Haki Yako Jitokeze

1761725442576.png
 
Back
Top Bottom