Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.

"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!

Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.

Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.

Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.

Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.

Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!

Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.

Boniface Kajunjumele Mwabukusi!
Yani hizo wanazoita ni sare za jeshi zinaagizwa china na uturuki sa sijui hizo sare ni za kwao au ni za majeshi ya nchi ya wenzetu.
 
Eti jeshi kazi yake kusaka sare teh teh teh hili litakuwa Jeshi la zama za mawe za kale.

Wanaacha mambo ya msingi kama vile research and development linakwenda kusaka sare. Ndiyo maana lilikuwa likitoa show za kuvunja tofali kwa vichwa badala ya kuonyesha limegundua au kutengeneza sialaha gani
Siku hiyo nilicheka na kusikitika sana. Mwanajeshi anavunja tofauli kwa kichwa.
Kwa zama hizi za teknolojia, watu wanavumbua silaha zitakazowezesha kujilinda na kushambulia kwa muda mfupi sana.
 
Haya manguo kuna mahali pale kawe immediately baada ya Jeshi yanauzwa, mengi tu ya kutosha, wasogee pale wakamate.
 
Mwambukusi yuko sahihi sana...

JWTZ waheshimu katiba ya nchi....

PT wetu ni kazi yao hiyo....

Tusilibagaze jeshi la polisi....mbona tunafika mbali sana na wakati tuna taasisi husika?!!! [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]


#SiempreJMT[emoji120]
 
JWTZ msititutishe, Mwanasheria upo sahihi. Kama tulivyosema jikiteni kwenye ubunifu, pamoja na ujasusi wa kidola. Upekuzi kwenye majumba yetu waachieni Police, hawa ni rafiki zetu tushawazoea.

Kila mtu atimize majukumu yake kisheria, Katiba ipo wazi unless hamjasoma vifungu vinavyowahusu. Kuanza kusaka matambara vyumbani kwetu its pure wastage of resources za Jeshi letu la wananchi.
 
Watanzania tuache kuchekea ujinga. Jwshi linapaswa kufanya mambo serious na sio kuanza kusumbua raia. Jeshi linapaswa kuwa sehemu ya raia kukimbilia pale ambapo vyombo vingine vyote vimeshindwa
Ni sheria gani inaylsema kwamba endapo vyombo vyote vimeshindwa inatakiwa raia kukimbilia kupata msaada kwa jeshi la wananchi. Kuna kitu kinaitwa distribution of labour. Ka taasisi inayo majukumu yake ya msingi.
 
Ni sheria gani inaylsema kwamba endapo vyombo vyote vimeshindwa inatakiwa raia kukimbilia kupata msaada kwa jeshi la wananchi. Kuna kitu kinaitwa distribution of labour. Ka taasisi inayo majukumu yake ya msingi.
Nchi inapo ingia vitani maana yake wanaobaki kutegemewa ni jeshi huku vyombo vingine vikiwa vimeufyata
 
Watanzania uzuzu wetu umeanzia kuonekana hapa hapa kwenye huu uzi. Yaani kabisa kuna watu wanamdhihaki na kumwona Mwambukusi kama amekosea. Watu kama hao unatarajia kuna siku watakomboka na kuwa huru kifikra???
Watanzania wao katiba hata hawaielewi inasimamia nini
 
Sio jukumu lao bali kazi ya polisi.

Tatizo unaamini matumizi ya nguvu kulkko akili kwasababu ya ufinyu wa elimu.

Sasa mtu anaajiriwa jeshini kwa kupata div four kidato cha nne utdgemee matumizi ya akili kweli?
Sasa jamani sisi wa div four tumewakosea nini hadi mnazarau div four zetu!? Jikiteni kwenye Hoja Kuu Wakuu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Anachokitafuta atakipata[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sana tu, katukana viongozi kimyaa, kamtukana Rais kimyaa, Kawatukana police kimyaa sasa anataka kutest maji, Nadhani atawataja walioko nyuma yake very soon. Ana act kama vile ndio kahamia Tanzania juzi wakati jitu lina miaka 60 huko. Nchi zote duniani watakosoana lakini siku zote wanalipa jeshi lao heshima hata kama kuna mapungufu. USA walisema hakuna mwanajeshi wao atashtakiwa kwa kuvunja haki za binadamu japo wao ni machampion wa mambo hayo. Israel alikataa wanajeshi wake kushtakiwa.. na wengine wengi. Hawa sio wajinga. Sasa huyu kafika sehemu anataka kuhatarisha amani ya nchi. shida hapa ukiwakashifu jeshi au police na wakakulia kimya unafungua mlango na kufunga itakuwa too late. Mshughulikieni huyu haraka.
 
Back
Top Bottom