Jeshi la wananchi laonywa lisivunje katiba ya nchi kwa kufanya majukumu yasiyo yake kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi

Ujumbe mzuri kasoro tu hilo neno 'hiko wapi'..maana yake nini mkuu?
 
Kwa hiyo jeshi likipekuwa likakuta chupi za mabakamabaka nayo itakuwaje sasa?

Jeshi lisilo na kazi linapekuwa nguo za watu. Huu ni ujinga mtupu.

Wanataka kuliguza jeshi letu kuwa below vikundi vya ulinzi shirikishi. Ni aibu sana
 
Ujumbe mzuri kasoro tu hilo neno 'hiko wapi'..maana yake nini mkuu?
Na maanisha wale wanao lalamika jeshi kutoa tamko kuwataka walio na magwanda kurejesha. Mbona ni jambo la kawaida tu. Unagwanda rejesha.
Mara ngapi watu wamerejesha siraha walizo nazo isivyo kihalali bila kuchukuliwa hatua?
Jeshi wamesema usiporejesha watakuja wao wenyewe kuchukua kwani wanajua. Sioni shida jeshi kutoa tangazo. Kinachotakiwa watu waatii.
 
Silaha huwa zinarejeshwa polisi, sio jeshini.
 
Huko shuleni mlisomea ujinga?

Mahakama ya jeshi ni maalumu kwa ajili ya wanajeshi!.Military police wanahusika zaidi jeshini.

Unapohalalisha wanajeshi kuingia mtaani "kusaka sare zao " inamaanisha

1)Polisi hawatekelezi majukumu yao
Ama 2)Wanaamua kuingilia mipaka ya polisi.

Kazi ya jeshi ni kutulinda wananchi ndiyo maana linaitwa LA WANANCHI
,na jukumu la polisi ni kulinda raia na Mali zetu.

Mwenye akili na asikie
 
Nadhani hujui pengine demokrasia ni nini na Governance ni nini? Wazungu walio kudanganyeni na demokrasia jiulize huko kwao kuna demokrasia? Je Rais wa Marekani anachaguliwa na nani? Ni nani hutoa maamuzi kuwa sasa huyu ndo Rais? Na hiyo demokrasia inataratibu zake. Unajua Marekani kuna maeneo Jeshi ndo wanatumika kuzuia vitendo fulani. Mfano kuna maeneo uwezi piga picha. Na hayajaandikwa. wakikukamata wanauwezo kuchukua hatua yoyote.
Kwanini wasiite polisi wafanye wao jeshi? Si Marekani tu ni katika nchi nyingi duniani. Military domain uwezi ukaichanganya na polisi au demokrasia.

Sijaona wapi raia kanyanyaswa. Tangazo limesema wenye uniform za jeshi rudisheni. Huo ni unyanyasaji? Huko ni kuharibu demokrasia? Tena wakasema msiporejesha tutakuja wenyewe kuchukau. Unyanyasaji huko wapi?

Unadai raia ni jeshi la akiba kwani polisi si jeshi la akiba? Hivyo kwa maelezo yako polisi akihusika si nae atakuwa anamnyanyasa jeshi la akiba aliye raia? Ha ha ha ha!

Jeshini tu wanajeshi akikosewa anashitakiwa na anauwezo kufungwa au kuvuliwa ujeshi si wangesema wananyanyasa jeshi? Yaani raia ahatarishe amani ya nchi muwache ati ni jeshi la akiba! Ha ha ha!

Si kweli kwamba raia ni jeshi la akiba. Kwa sababu ajachukua mafunzo yoyote ya kijeshi na kuthibitishwa kuwa mwanajeshi kwa kiapo.
Nadhani hujui maana ya jeshi la akiba. Hakuna raia aliye pigana vita ya Iddi Amini. Ili upigane vitani kwanza lazima upokee mafunzo ya kijeshi, kukuwezesha kujua mbinu za kivita. Kulinda na kujilinda kisha unapelekwa vitani. Hapo utakuwa umekuwa mwanajeshi.

Hata wakati wa Idd Amini watu waliingia Mgambo wakafundishwa. Ndo maana Mgambo ni jeshi la akiba ambalo liko chini ya JWTZ. Uwezi sema kila raia ni jeshi la akiba. Ndo maana kuna raia na jeshi.
 
Katukana tusi gani?kwanini wasimchukulie hatua?Jeshi lifuate sheria za nchi,mambo ya kukaa kambini bila kazi ndio matokeo yake haya.
 

Hakika!
 
90% Kwa wanaopinga operations nguo jeshi wanahisia za uharifu! Ni zoez la kawaida sanaaaa kwahy unahitaji polisi ndio wafanye kazi hiyo kwakuwa mnawamudu? Ukumbuke vazi la jeshi la ulinzi la wananchi hata hao polisi wanavaa na nikosa pia, kwahyo tuache watu wafanye kazi tupunguze uraiya ambao hauna afya Kwa taifa letu,,, tusitete uharifu ukumbuke hata mwanajeshi akivaa uniform/ Kombat nje ya muda wa kazi ni kosa ,, Sasa Kwa raia inakuwaje? Tuache kuiga mataifa mengine!
 
Kupekuliwa nyumba kwa nyumba ni maisha fulani ya kikomunisti yaliyopitwa na wakati.

Sheria za nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwa na vipengele vya kukataza "unreasonable search".

Yani mpaka nyumba yako isachiwe, inatakiwa iwepo warrant ya mahakama, jaji kaitoa kwa kuridhika kuwa kuna sababu maalum ya kui convince mahakama kutoa ruhusa nyumba yako isachiwe. Nyumba yako kama nyumba moja, si katika fungu la mkumbo wa kutafuta nguo za polisi.

Na warrant inatakiwa iwe specific kinachotafutwa ni nini, warrant ya kutafuta nguo za jeshi hairuhusiwi kukamata madawa ya kulevya.

Mwabukusi anaelimisha jamii kwamba, kadiri tunavyotoka kwenye mifumo ya kipolisi inayoongozwa na sheria na mahakama na kupeleka habari za search kwenye jeshi, ndivyo tunavyoondoka kwenye hiyo due process iliyowekwa kisheria na kwenda kwenye mfumo wa shaghalabagala ya kuendeshwa kijeshijeshi.

Watu wanaoishi nchi zenye kufuatilia sheria dhidi ya unreasonable search, kama Marekani, watamuelewa sana Mwabukusi hapa.
 
Hutakiwi kuwa na hofu kama sio muarifu!
 
Acha bang3 wewe. Unadhani tungekua na serikali ya mseto na mpinzani akiwa ameshikilia ile nafasi ya VP huyo Mkuu wako wa Majeshi angetoa ule msimamo? Jeshi ilikua enzi za Nyerere, hawa wasasa ni wachumia tumbo na VIBARAKA WA CCM. Kazi yao ni kuhakikisha chama twawala kinaendelea kusalia madarakani bila bugdha
 
Kwa sababu wewe unajihesabu kama unajua basi hufundishiki. Jeshi kwenye vita huwa ni watangulizi tu; nchi ikiwa kwenye vita raia ye yote anakuwa mpiganaji ila nani na anakwenda kwa kipindi kipi jeshi ndilo linaratibu. Hiyo demokrasia nyeusi au nyeupe unayotaka kutuambia Tanzania inaweza kuigundua sasa unarudia tu propaganda za watu wasiofikiri au wanaotaka kuturubuni. Demokrasia ilikuwepo hata kabla ya Wagriki waliisemea. Hiyo demokrasia ya Tanzania unayoijua wewe ni ipi? Ya kuwaacha watu wabaki wajinga ili uendelee kuwatawala? Unakumbuka Tanzania ilifikia kiwango cha demokrasia kiasi cha wasomi wa kimataifa kuja kujifunza hapa. Sasa ile demokrasia bado ipo? Ndiyo maana huelewi kuwa Jeshi letu lilianzishwa kama Jeshi la Wananchi na ndiyo maana tunasema lichukue hadhari linapokuja kwa wananchi kwa sababu mafunzo ya namna ya kushughukikia jinai au madai ni polisi ambao wamefunzwa, siyo Jeshi. Ni sawa vita itokee ukasema IGP ndiye atakayepiganisha vita. Kama huelewi ninachosema basi nimekata tamaa; bila shaka wewe una uzoefu na ni msomi kupita wote hawa ambao wana maoni tofauti na wewe.
 

Ushamba na akili za kitumwa! Bora muendelee kuwa masikini wa kutupwa maana mnastahili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…